Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Asante kaka
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mdau sidhani kama amejenga, kwa haya maelezo yake hii ni chai.
 
Kila kitu kinawezekana chini ya jua hivyo nakupongeza sana mtoa mada kwa hatua uliyofikia.
Binafsi nipo naendelea na ujenzi na kwa sasa nipo kwenye hatua za mwisho. Nyumba yangu ina vyumba 3 vya kulala, sebule, jiko, dining, store na studying room.
Nimefanya yafuatayo:
Grill kwenye madirisha yote pamoja na mlango wa mbele na nyuma;
Frame za milango yote;
Plasta ndani na nje;
Nimefunga Gypsum za Tanzania double elephant @15,000;
Plumbing nyumba nzima total ~800,000 pamoja na fundi;
Wiring nymba nzima nimetumia wire za single aina ya Euro total ~1.2m pamoja na fundi (nimeshaomba kuunganishiwa umeme, survayer ameshafika site).

Kiujumla hadi sasa nimetumia approximately 45m. Pumzi imepungua nataka kumalizia chumba kimoja nihamie, mengine nitaendelea nayo nikiwa ndani.
Nilianza kujenga nikiwa na pesa taslim 10m. Hata sielewi mpaka nilipofikia zimetoka wapi. Nilianza ujenzi February 2019.
Ambacho naweza kushauri ni kuwa usijenge kwenye makaratasi, anza na kile ulichonacho, Mungu atakufanikisha tu taratibu ukiwa na nia. Ujenzi una vigharama vya ajabu sana vinavyotokea hivyo mtu akikuambia katumia kiasi fulani cha fedha wala usishangae, huenda kuna gharama kakutana nazo ambazo wewe hujakutana nazo.
 
Twende kwa fact usilalamike, eleza nieleze hivyo tutawezana Mkuu. Vinginevyo tuishie hapa hapa.


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
Tafuta fundi akuchanganulie kwa mujibu wa hiyo nyumba ya mtoa post,anzia kuweka mifumo ya wiring (gharama ya vifaa na ufundi) kisha lipu kutandika jamvi ,blandering, gypsum board, gypsum powder, fisherboard ,pvc board,misumari,tiles, cement ya kukazia tiles, fedha ya mafundi( fundi lipu,fundi tiles ,fundi blandering,fundi gypsum board, fundi pvc board)
Hapo ni kwa uchache tu ndugu yangu
Hapo bado hujaweka na yale madirisha yetu ya siku hizi yale wala milango ya ndani kwa kila chumba,hapo vioo vya juu ya partition ya milango bado wala hujamuita fundi rangi aje aanzie skimming mpaka apake rangi yake kuanzia kuta mpaka dali
Upo hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
50m ulitakiwa uhamie, na ww umepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
..............Yah sikatai inawezekana kwa hesabu zako ukawa upo sahihi ila mimi ambaye nipo kwenye mchezo bado sijauona upigwaji wowote na hiyo gharama inakuwa kubwa kutokana na naweka vitu vizuri vya kudumu ambavyo vina-cost hela nyingi,kwa sasa nina nguvu naweka vitu sitegemei baada ya miaka miwili nivibadilishe kisa vimeanza kuchoka.

Umri unasogea majukumu yanaongezeka haya mambo ya ujenzi ukisema uweke vitu temporary siku vinaharibika vyote na mfukoni hakutoshi nyumba inahitaji maintenance kama siyo kuiacha ionekane kama pango la njiwa utafanyaje!ndo ninachokikwepa hicho.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Ila vifaa jaribu kununua wewe maana hizo gypsum ni 13500 Jumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Appreciate. And noted ni kweli yaani umelenga
mle mle.
 
Mkuu hizi gharama anazotaja mpaka meogopa eti 200milion na bado haijaisha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizi gharama anazotaja mpaka meogopa eti 200milion na bado haijaisha


Sent using Jamii Forums mobile app
Mjanja mjanja huyo,kwa sababu yupo nyuma ya keyboards anadhani hakuna watakaong'amua uwongo wake na
watu dizain hii wanapenda sana kuwakatisha wenzao tamaa kwa kujibunia vitu ambavyo havipo.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mkuu ujenz unaongezeka garama kutokana na quality za material unayotaka kujengea ivi unajua square meter moja ya kigae cha romantile ni almost 18500 usibishe mkuu akikuambia ametumia 50m ni kutokana na aina ya materials alizotumia ww ukiezeka na simba dumu na mwenzio akiezekea roman tiles hamtakuwa na garama sawa za kupaua.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni shida, na hapo umebananabanana na mafundi wa mitaani, umezunguka maduka kupata material za bei nafuu hadi karikaoo umeenda, ingejengwa na injinia hadi sasa ingekuwa inasoma milioni 100.
Mkuu si kweli kwamba ukijenga na injinia basi garama ya nyumba inaogezeka hii dhana tumenijengea tu kutokana na baadhi ya wataalamu wetu kutokua na intergrity yakutosha lkn cost za ujenz ni very common na realistic. Kwamfano square meter moja ya plaster ni 2500 mpk elfu 3000 tofali moja kujenga ni almost 400 mpk 550( km sijakosea i am not sure kuhusu current makert price)km mmepigiana hesabu vizur na materials umenunua ww na bei za labour charge ni common zina range ktk kiwango flan hapa utapigiwa wap?. Tena ukijenga na engineer unatakiwa ujenge at a low price zaidi tena yeye anafaa kukushaur the most economic way ujenge bila kuharibu quality ya nyumba yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mainjinia nasikia wanaweka gharama kubwa ili wabaki na faida ya kutosha, labda matajiri ndo wanamudu aina hiyo ya ujenzi ya kuwatumia mainjinia
 
Fundi wa Gypsum kakutoza ngapi kama waweza nisaidia namba za fundi PM
Kila kitu nanunua mwenyewe mkuu, yani fundi labda atanipiga kwenye ufundi tu.
Pia kumbuka bei zinatofautiana kulingana na sehemu ulipo. Mimi sehemu nilipo hiyo ndio bei yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…