Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Hata akisema bati 200 na mbao 400 misumari gunia 3 haifiki hiyo 15M .... Jamaa muongo ana mahesabu kama ya CHAKUBANGA
Kuna bati za bei mbaya chief. ALAF versatile, romantile, na kuna bati za kigae zile ziko coated na mchanga kwa juu. So usibishe, pia room tatu zipo za ukubwa tofauti unakuta mtu kajenga room kubwa say 4 by 4meters na vyumba vyote ni self contained.

Sebule unakuta ukubwa 6by6 mters so huyo lazima atumie gharama kubwa. Binafsi nilitumia 10.8M kwenye foundation na kujaza kifusi. Zingatia eneo lilikua na slope kubwa iliyonigharimu kuweka mikanda/beam mbili. Na niliweka nguzo sita upande wenye slope na kati.
Na nilikuwepo site mwanzo mwisho hakuna kilichoibwa.

Msimbishie mtu hesabu zake muulizeni mchanganuo wa project yake.
 
Tena shukuru hukupewa madirio pengine ungekuwa hujaanza hayo unataka kujua hayakusaidii chochote ndugu
 
Ipo sahihi lakini hujasema Kama mfumo wa choo je ni pesa hiyohiyo au la. Kwa 12 hujapoteza cha msingi ukiweza maliza vyumba 2 ili uhamie na mengine yatajitokeza ukiwa hapo kwako tena utayakamilisha kwa umakini zaidi. Niwazo langu unahihari ya kuchagua uwazavyo.
 
Ninyi vijana wa mjini kujifanya kujua kwingi ndio maana kila siku mnamaliza mtaa kwenye nyumba za kupanga,miezi sita tabata,inayofuata sinza,kimara hamjengi.
Wakati mwingine mkija mikoani mnaona aibu kwakuwakuta vijana wa umri chini yenu wapo kwenye nyumba zao na maisha yanasonga.
Hii ni kwasababu ya kujifanya wajuaji wakati kiuhalisia haimna isue kazi kuzurula na vibegi mjini hamna dira yoyote.
Ujenzi kama utausimamia mwenyewe na ukajua namna sahihi yakukwepa gharama utatumia pesa yakawaida.
Sio mbaya ninyi endeleeni kugombania na kujisifia kupanga nyumba za wenzenu zenye tiles nzuri,aluminium,uzio na ma geti mpaka mstuke mvi kichwani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji122][emoji122]
 
Hawa vijana wa Daslama ni wapuuzi sana yani wakishakua na uwezo wa kupanga kachumba kamoja Sinza tv flat screen,kasofa,kafliji na kitanda cha 6x6 basi wanamuona kila mtu ni fala.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sitaki kusema uongo wala kubishana na mtu.Kiwanja nilipewa (sijanunua)nikatumia Milion tatu kujenga msingi mpaka bati nyumba ya vyumba vitatu na sebule.
Nimetumia milioni mbili kumalizia finishing mpaka tiles.
Nimetumia milion moja kujenga choo nje na septic tank.nimeingia kibishi nikaweka umeme after two years
NB:Matofali nimefyatua mwenyewe,
*fundi nimempata mtaani nikampa ramani tu.Nilimlipa Milion moja na nusu vyote mpaka mtu wa kupaua alimleta mwenyewe.
*Septic nimechimbiwa kwa elf 70 na kujengea nimechajiwa laki moja jumla laki na 70.Iliobaki ni kuunganisha choo ndani na cha nje coz septic tank ni moja.
Kwa hiyo,milion 3 msingi +milion 2 finishing + milion moja septic na choo nje+hela ya fundi milion moja na nusu+ rough extra milion moja( usafiri na matumizi madogo madogo pale site) nikijumlisha na gharama za wiring mpaka kuingiza umeme na kisima nje nimetumia roughly milion kumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu akubariki kwa kututia moyo sio hawa makuz kazi kutukatisha tamaa[emoji122][emoji122]
 
Best hueezi kuwa na kalio zito namna hiyo ukose hata kibanda cha kuhongwa[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Ha ha ha ha[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787] umeanza ungese na wewe!

We haribu uzi wa watu wakutoe baruuu, watu wenyewe wamevurugwa humu[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Unaambiwa msingi tu mtu katumia 50m na ni nyumba ya chini vyumba vitatu just normal tu[emoji15][emoji15][emoji15][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119]
 
Kama somo linavyojielewa hapo juu

Wakuu, wale wataalamu wa ujenzi. Kwa pesa hiyo naona kama sijafikia lengo kwa sababu sijaweka madirisha (drill) kati dirisha 08 mbili tayari mlango (drill) tayari. Lakini kitu kinachoniuma sijapiga hesabu vizuri.

Nilitegemea kibanda japo niwe nimehamia.

Floor bado, blandaring, je sijapoteza?

Asante sana
Inategemea unataka kufuga nini kwenye hiko kibanda chako ila kwa hapo ulipofikia nguruwe unaweza anza kufuga bila matatizo
 
Siyo "DRILL"ni GRILL,halafu kwa 12,000,000/= na umepaua basi unawezakuwa umejenga mchanga mtupu,hiyo ni hela ya kujenga room mbili bila finnishing kuanza,hata mfumo wa maji safi ndani hujaweka,na hapo utakuwa umepaua na bayi za gauge 30,mbao zilizokuwa treated na oil chafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upuuzi..tofali inunue Tsh 2000 moja room 2 zipe tofali 2000...jenga na cement ya 1m weka bati za m2 fundi mpe 2m=sawa na m5...m2 mchnga sawa na m7
 
Back
Top Bottom