Sitaki kusema uongo wala kubishana na mtu.Kiwanja nilipewa (sijanunua)nikatumia Milion tatu kujenga msingi mpaka bati nyumba ya vyumba vitatu na sebule.
Nimetumia milioni mbili kumalizia finishing mpaka tiles.
Nimetumia milion moja kujenga choo nje na septic tank.nimeingia kibishi nikaweka umeme after two years
NB:Matofali nimefyatua mwenyewe,
*fundi nimempata mtaani nikampa ramani tu.Nilimlipa Milion moja na nusu vyote mpaka mtu wa kupaua alimleta mwenyewe.
*Septic nimechimbiwa kwa elf 70 na kujengea nimechajiwa laki moja jumla laki na 70.Iliobaki ni kuunganisha choo ndani na cha nje coz septic tank ni moja.
Kwa hiyo,milion 3 msingi +milion 2 finishing + milion moja septic na choo nje+hela ya fundi milion moja na nusu+ rough extra milion moja( usafiri na matumizi madogo madogo pale site) nikijumlisha na gharama za wiring mpaka kuingiza umeme na kisima nje nimetumia roughly milion kumi.
Sent using
Jamii Forums mobile app