Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Hongera kwa hatua hiyo. Mimi mwenyewe mpaka hatua hii nimetumia 13M. Vyumba 4, sebule kubwa(4*5m) dining, toilet moja ndani. Inawezekana ikiwa Kuna usimamizi wa karibu na siyo wa kuagiza
IMG_20191215_190301_515.jpg
 
Mil 7 atamaliza kila kitu? Unajielewa kweli wewe? Hivi unajua gharama ya finishing ni mara 2 hadi 3 ya gharama ya boma? Au u anazungumzia kumaliza kila kitu kwa namna gani

Sent using Jamii Forums mobile app

Twende kwa fact usilalamike, eleza nieleze hivyo tutawezana Mkuu. Vinginevyo tuishie hapa hapa.


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
..........Mkuu umemaanisha au?hata hivyo sikubishii inawezekana ulipo wewe gharama zikawa kubwa zaidi but kwa ujenzi wa nyumba standard Dar gharama zipo juu kiasi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

Nyumba hiyo hiyo standard kujenga mkoani ni gharama sana.


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
................Sawa sawa brother ila usi-panic sana mpaka ukafikia kutoa kauli zisizofaa!

Mimi kwa upande wangu nahitimisha kwa kusema kwamba “wewe ni changamsha genge tu huna popote ulipoweka hata msingi wa nyumba so huna idea na masuala ya ujenzi ndo mana umeshindwa kutetea hoja zako kwa facts”

Nimemalizana na wewe,sitakurudia tena hapa.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Naunga hoja mkono mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa hatua hiyo. Mimi mwenyewe mpaka hatua hii nimetumia 13M. Vyumba 4, sebule kubwa(4*5m) dining, toilet moja ndani. Inawezekana ikiwa Kuna usimamizi wa karibu na siyo wa kuagizaView attachment 1307621
Hongera sana, hii ipo mkoa upi? Natarajia kuanza ujenzi naona namna ya ujenzi yaendana na huku nilipo so nataka pata picha kamili ya kujiandaa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu makini anayejua kucheza na pesa kwenye ujenzi kama nyumba ya ukubwa huo imeshakula 50millions na hujafikia hata kupiga plaster basi amini usiamini fundi wako au unayemwamini kukusimamia ujenzi atahamia kwenye nyumba yake akuache ukiwa bado kwenye nyumba ya kupanga.

Materials unaagiza kwa container kutoka ulaya au?sipo hapa kubishana nimekupa tahadhari tu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Mkuu kweli aisee mafundi hawaaminiki kabisa.
Hiyo kitu uliyosema ilinitokea hata Mimi.
Nilitumia milioni 50 na nyumba ikawa haijaisha.
Baadae kushtuka naona huyo fundi kashajenga nyumba yake na kahamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi mdis mtu, ila huu ni uongo wa kiwango kikubwaaa, cement, mbao, bati, grill, milango....bado sanaaa
Sitaki kusema uongo wala kubishana na mtu.Kiwanja nilipewa (sijanunua)nikatumia Milion tatu kujenga msingi mpaka bati nyumba ya vyumba vitatu na sebule.
Nimetumia milioni mbili kumalizia finishing mpaka tiles.
Nimetumia milion moja kujenga choo nje na septic tank.nimeingia kibishi nikaweka umeme after two years
NB:Matofali nimefyatua mwenyewe,
*fundi nimempata mtaani nikampa ramani tu.Nilimlipa Milion moja na nusu vyote mpaka mtu wa kupaua alimleta mwenyewe.
*Septic nimechimbiwa kwa elf 70 na kujengea nimechajiwa laki moja jumla laki na 70.Iliobaki ni kuunganisha choo ndani na cha nje coz septic tank ni moja.
Kwa hiyo,milion 3 msingi +milion 2 finishing + milion moja septic na choo nje+hela ya fundi milion moja na nusu+ rough extra milion moja( usafiri na matumizi madogo madogo pale site) nikijumlisha na gharama za wiring mpaka kuingiza umeme na kisima nje nimetumia roughly milion kumi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la kupaua, nshaona mtu kapaua kwa m27, bati flan hv za kigae, juu kama zimemwagiwa mchanga wa rami, kipande kimoja kizito balaa, mbao, zilipangwa nyingi sana,
Nliambiwa kigae kimoja kinacost 15000 mpaka 25, ujenzi unatofautiana na material

Material size ya kati, m50 unahamia nyumba ya kisasa kabisa
Maana nachoshangaa maana bati za migongo mipana or maxcover lazima huezekaji huende kwny 15m ,na hukigusa versatile,romanitile lazima ufike 30m hapo kuezeka tu maana haina hiyo ya huezekaji inahitaji mbao nyingi labda tuwaulize

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mil 7 atamaliza kila kitu? Unajielewa kweli wewe? Hivi unajua gharama ya finishing ni mara 2 hadi 3 ya gharama ya boma? Au u anazungumzia kumaliza kila kitu kwa namna gani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Mimi watu wengine hunishangaza kujifanya ujuaji wakati ni mbumbumbu kabisa.
Milioni 7 ni kitu gani kwenye ujenzi wakati ukipiga plaster tu milioni 4 au 5 inakatika unabakiwa na milioni 2 au 3.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
50m ulitakiwa uhamie, na ww umepigwa
Kwa vyovyote hizi reply zinahusu post zangu nilizo-post kwenye huu uzi,hata utumie material gani kutoka Tanzania hakuna nyumba ya chini ya room tatu even nne inajengwa boma tu bila kuezekwa kwa million 35 msiwatishe watu na kuwakatisha tamaa kwa vitu vyenu vya kubuni.

Hapo chini nitaonekana kama natafuta kick but siyo lengo langu nataka mkuu Nyumisi utuwekee hilo paa lililo-cost ml15 kwenye nyumba ya rooms zisizozidi tano,hapa nimeambatanisha picha bati ni ALAF order kiwandani moja nilinunua Tsh28,580 zimeingia bati 120,kuna kofia hesabu za mbao nk haijafika mill12 fundi 1.3mill nyumba ina master bedroom,vyumba viwili vya kulala,choo&bafu public,store,jiko dinning na sitting room kubwa inaenea set mbili za sofa na baraza mbili ya mbele kubwa na nyuma ya wastani,msingi wa hii nyumba chini ya ndugu yangu engineer ulikata mil8 na cent kadhaa.

Nimejengea tofali Nch 6,imekula tofali 4,170 cement sikuinyima nondo sikuinyima na kwa sababu pana kama kilima ina nguzo tano permanently za zege zilizosimama kutoka kwenye kiuno mpaka kwenye lintel zizolinigharimu cement ya kutosha sasa nimeshaipiga plaster iliyopimwa kwa TIMANZI cement tu nje na ndani mifuko 73,frame za milango nimeweka mbao Mninga nyumba nzima milango ipo saba frame moja 190K tayari nimeshafunga milango mitatu mkubwa umeni-cost 475K midogo @270K,nimepiga brandering na rough floor kwa ajili ya kupokea tiles napo nimeingiza mchanga na cement za kutosha,grills nimeweka chuma mml6 zipo dirisha 11 vyooni na store 4 ila nimepiga hesabu imegota kwenye Tsh46,475,000/=.

Huu ujenzi nimejenga Dar,naweza kusema nipo zaidi ya %70 nyumba kuimaliza it means kutoka sasa nikiwa na na 20mill nitakuwa naongea mengine halafu nyie mpo hapa mnadanganya jamii mnajenga maboma kwa mil50...siyo vizuri haipendezi kuna watu wanatamani waanze ujenzi ila wakikutana na haya mambo ya kuambiana habari za mamilioni wanaogopa hela wanaenda kuichoma bar au kununua magari wakiamini muda wao wa kuanza ujenzi bado kumbe hata million 10 inafaa kuanza.View attachment 1305931View attachment 1305932View attachment 1305933View attachment 1305934

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kama unaweza kujenga, msingi, ukuta, paa kwa Milioni 12.... Labda uwe fundi wewe mwenyewe wa kila kitu, usilipe vibarua, tofali uandae mwenyewe, nyumba ujengee udongo wa tope... Hapo at least takuamini japo nyumba haitakua na viwango stahiki.
 
Back
Top Bottom