Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Nimejenga kibanda changu vyumba 3, sebule ndogo, jiko dogo, store, choo na bafu la ndani kwa Sh 12,000,000

Kama somo linavyojielewa hapo juu

Wakuu, wale wataalamu wa ujenzi. Kwa pesa hiyo naona kama sijafikia lengo kwa sababu sijaweka madirisha (drill) kati dirisha 08 mbili tayari mlango (drill) tayari. Lakini kitu kinachoniuma sijapiga hesabu vizuri.

Nilitegemea kibanda japo niwe nimehamia.

Floor bado, blandaring, je sijapoteza?

Asante sana
bila kuweka picha hapa utakuwa umepoteza
 
Mkuu unaweza kuta nyumba ramani ile ile na ukubwa ule ule moja imetumia mil 50, nyingine imekula mil. 200 kutegemea na eneo, ubora wa materials na aina za mafundi au injinia.
Inashangaza watu wengi hawajui kitu rahisi kama hiki. Mfano mtu katumia vifaa vya finishing kutoka Dar Ceramica tiles za bafuni 50,000 per square metre ni bei ya kawaida,vyoo kimoja hadi 500,000, kuna taa za ndani moja tu 65,000 ya kawaida kabisa,kuna taa za nje moja hadi 100,000 kitchen unit metre moja 500,000. Rangi kuna zile rangi za ndani ukiingia utafikiri ukuta umepigwa tiles sebuleni tu unaweza kutumia 500,000. Boma zinaweza kufanana bei ila finished house zikatofautiana mamilioni.
 
kweli. muhimu katika yote kujenga ni akili sana. Unatakiwa wewe mwenyewe ushiriki kikamilifu. Lakini jambo lingine la Msingi ni Rational use of resources. Engineer mwingine kwa kutaka sifa anakupangia vitu vyenye gharama kubwa ambavyo sio lazima. Mfano hata hospitali unaweza kwenda una maumivu ya mguu ukapewa dawa za elfu 30 wakati panadol ya elfu moja na miatano zilikuwa zinatosha kuondoa maumivu hayo hayo na bila madhara yoyote
finishing utakayofanya ndio itapanga bei ya nyumba yako.
 
Inashangaza watu wengi hawajui kitu rahisi kama hiki. Mfano mtu katumia vifaa vya finishing kutoka Dar Ceramica tiles za bafuni 50,000 per square metre ni bei ya kawaida,vyoo kimoja hadi 500,000, kuna taa za ndani moja tu 65,000 ya kawaida kabisa,kuna taa za nje moja hadi 100,000 kitchen unit metre moja 500,000. Rangi kuna zile rangi za ndani ukiingia utafikiri ukuta umepigwa tiles sebuleni tu unaweza kutumia 500,000. Boma zinaweza kufanana bei ila finished house zikatofautiana mamilioni.
Watu wanabisha tu, kisa yeye kaokoteza material reject na dili dili nyingi anafikiri gharama za ujenzi ziko uniform...
 
Inashangaza watu wengi hawajui kitu rahisi kama hiki. Mfano mtu katumia vifaa vya finishing kutoka Dar Ceramica tiles za bafuni 50,000 per square metre ni bei ya kawaida,vyoo kimoja hadi 500,000, kuna taa za ndani moja tu 65,000 ya kawaida kabisa,kuna taa za nje moja hadi 100,000 kitchen unit metre moja 500,000. Rangi kuna zile rangi za ndani ukiingia utafikiri ukuta umepigwa tiles sebuleni tu unaweza kutumia 500,000. Boma zinaweza kufanana bei ila finished house zikatofautiana mamilioni.
Nakubaliana na wewe
 
Siyo "DRILL"ni GRILL,halafu kwa 12,000,000/= na umepaua basi unawezakuwa umejenga mchanga mtupu,hiyo ni hela ya kujenga kabanda ka room mbili bila finnishing kuanza,hata mfumo wa maji safi ndani hujaweka,na hapo utakuwa umepaua na bati za gauge 30,mbao zilizokuwa treated na oil chafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sijakuelewa kabisa[emoji23][emoji23]

Aliyekusimamia mjengo wako alipata pesa nzuri sana aisee

Maana mm kwa 12M nilitegemea kiongozi awe umesogeza pakubwa tu maana hiyo nyumba ya room tatu na kama alivyosema room za kawaida seble ya kawaida ingetakiwa iwe imesogea sana maana kunyanyua structure tu ya mjengo sio inshu

Gharama zinaanza Kwenye usafi(finishing and decoration)ndio changamoto ilipo
 
Ninyi vijana wa mjini kujifanya kujua kwingi ndio maana kila siku mnamaliza mtaa kwenye nyumba za kupanga,miezi sita tabata,inayofuata sinza,kimara hamjengi.
Wakati mwingine mkija mikoani mnaona aibu kwakuwakuta vijana wa umri chini yenu wapo kwenye nyumba zao na maisha yanasonga.
Hii ni kwasababu ya kujifanya wajuaji wakati kiuhalisia haimna isue kazi kuzurula na vibegi mjini hamna dira yoyote.
Ujenzi kama utausimamia mwenyewe na ukajua namna sahihi yakukwepa gharama utatumia pesa yakawaida.
Sio mbaya ninyi endeleeni kugombania na kujisifia kupanga nyumba za wenzenu zenye tiles nzuri,aluminium,uzio na ma geti mpaka mstuke mvi kichwani.
Mbona kama unanisema mimi kabisa mkuu?
 
Vijana wa hovyo sana..
Ukioa unakuja na uzi..
Harusi..uzi...
Kazi...uzi...
Mtoto...uzi...
Kununua pc simu usafiri.. uzi ..
Kuwanja, kujenga uzi ...
Kuumwa kidogo tuuu uzi ....

Huu ni ugonjwa tunaoulea kwa sasa.
Ushauri TOZO IONGEZWE kuna watu bado dawa haijawaingi
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla na rejareja :-
2*2 fut12=2500
2*3 fut 12=3500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=4500
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=14000
1*10fut 12 fisher board( treated)=15000
2*4 fut18(treated)=10000
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu pia Tunafanya delivery kwa wakazi wa Dar es salaam
Ofisi zetu zipo Tegeta kibaoni-Bagamoyo road
 
Mimi nimejenga nyumba ya kawaida yenye vyumba vitatu, sebule, dining, jiko na vyoo vya ndani kama hiyo ya kwako. Kwenye paa pekee nimetumia milioni 15 na kidogo. Hapa ilipo imeshatafuna almost milioni 50 na bado sijakamilisha finishing za tiles, gypsum, skimmimg/plaster, kupiga rangi, milango na kuweka madirisha ya aluminium. Inawezekana upo sahihi unaposema umejenga kibanda...
[emoji3]
20220906_213011.jpg
 
Kama somo linavyojielewa hapo juu

Wakuu, wale wataalamu wa ujenzi. Kwa pesa hiyo naona kama sijafikia lengo kwa sababu sijaweka madirisha (drill) kati dirisha 08 mbili tayari mlango (drill) tayari. Lakini kitu kinachoniuma sijapiga hesabu vizuri.

Nilitegemea kibanda japo niwe nimehamia.

Floor bado, blandaring, je sijapoteza?

Asante sana
Drill imehusikaje kwenye madirisha na milango mkuu?
 
Back
Top Bottom