kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,275
- 3,316
Kwema ndugu zangu?
Jamani haya maisha yaacheni tu yaitwe maisha. Kuna sehemu nina kabiashara kangu ka kuzugia ili siku ziende hapa mjini.
Sasa kikawaida asubuhi huwa namuacha kijana wangu anasimamia haka kabiashara then jioni kama hivi nikiwa nimetoka kwenye mishe zangu zingine naungana na kijana kusaidiana majukumu ya dukani.
Leo nimerudi zangu toka kwenye mizunguko, wakati nashuka kutoka kwenye bajaji ya kushare ili nielekee dukani kwangu, nikamuona mtu kama ex wangu anatoka kununua bidhaa ofisini kwangu bana, ikabidi nijifiche mahali kwanza nimpimie kama ni yeye au siye, kwa kweli yule dada ni ex wangu kabisa, kilichonisikitisha nimemuona anaingia na ku-drive v8 new model hapo ndipo nilipoona aibu kujitokeza hata kumsalimia coz binafsi sina hata usafiri, kaduka kenyewe mtaji ni milioni moja na ushehe.
So baada ya ex kuondoka nimeenda dukani, nikamuuliza dogo yule dada mnafahamiana, dogo kaniambia hawajuani ila toka mwanzo wa week hii anamuona kawa mteja wetu mzuri anakuja dukani anatuungisha vitu hata vya 30k kwa wakati mmoja.
Sasa wasiwasi wangu ni kwamba, huyu ex siku akinikuta mimi dukani itakuwaje maana for sure kipindi tunaachana nilikuwa vizuri sana kiuchumi, ila sasa ndiyo hivi niko juu ya mawe nimeyumba, nitamuangaliaje siku hiyo wakuu?