Nimejificha baada ya kumuona Ex girlfriend anaendesha V8 new model

Nimejificha baada ya kumuona Ex girlfriend anaendesha V8 new model

V8 new model ndio gari gani?
images (57).jpeg
 
Kwema ndugu zangu?

Jamani haya maisha yaacheni tu yaitwe maisha.

Kuna sehemu nina kabiashara kangu ka kuzugia ili siku ziende hapa mjini.

Sasa kikawaida asubuhi huwa namuacha kijana wangu anasimamia haka kabiashara then jioni kama hivi nikiwa nimetoka kwenye mishe zangu zingine naungana na kijana kusaidiana majukumu ya dukani.

Leo nimerudi zangu toka kwenye mizunguko,wakati nashuka kutoka kwenye bajaji ya kushare ili nielekee dukani kwangu,nikamuona mtu kama ex wangu anatoka kununua bidhaa ofisini kwangu bana, ikabidi nijifiche mahali kwanza nimpimie kama ni yeye au siye,kwa kweli yule dada ni ex wangu kabisa,kilichonisikitisha nimemuona anaingia na ku-drive v8 new model hapo ndipo nilipoona aibu kujitokeza hata kumsalimia coz binafsi sina hata usafiri,kaduka kenyewe mtaji ni milioni moja na ushehe.

So baada ya ex kuondoka nimeenda dukani,nikamuuliza dogo yule dada mnafahamiana,dogo kaniambia hawajuani ila toka mwanzo wa week hii anamuona kawa mteja wetu mzuri anakuja dukani anatuungisha vitu hata vya 30k kwa wakati mmoja.

Sasa wasiwasi wangu ni kwamba,huyu ex siku akinikuta mimi dukani itakuwaje maana for sure kipindi tunaachana nilikuwa vizuri sana kiuchumi,ila sasa ndiyo hivi niko juu ya mawe nimeyumba, nitamuangaliaje siku hiyo wakuu?
Hapo huna cha kufanya labda akumbuke mapigo yako Kama ulikuwa unapeleka Moto,
 
Usimkimbie tena, kuwa imara kama mwanamume na sio mwanaume. Hiyo ni hali ya katika harakati za mapambano.
 
Eti V8[emoji2960][emoji2960][emoji2960]

Yaan jf bana
 
Asikutishe we mwanaume unaogopaje? Mademu wananijia nyingi simple sometimes ovu sana kupata vijimali kama hivyo Anakuchezesha tu psychologically mpuuze! Move on
 
Kweli v8 new model alfu aje kila siku kununua sukari na chumvi jmn acha story zako Kam nikweli mbona ujasema bidhaa alizonunua eti 30 alfu Ni kaduka tu

Hata dompo kila siku hawez kuw ndio ananunua kila siku
Nani kasema kila siku?
 
Humu kunatafutwa likes, comments, na attention basi...mtu anajifungulia uzi tu, vitu havina hata uhalisia[emoji1787][emoji1787]
Na wewe fungua upate hizo likes kama ni dili kwa upande wako.mbona rahisi tu!
 
Ukute kapelekeza, anakuja kukuonyeshea jeuri, dawa akija usimpongeze Wala kushoboka, salama inatosha Sana, na Wala husitangaze shida zako.
 
Mkuu lako dogo mimi nilikutanaga na ex wangu wa advance alikua na BMW X6 akanambia yake yani amebadilika amekua kisu hatari. Tukapiga piga stori kilichoniuma kuona dada wa kazi anakuja na mtoto anaita mama yaani daah niliishiwa pozi hapo nmemaliza chuo sina kitu nimepigika hatari.

Dada akachukua namba yangu hata mzuka wa kuomba kurudiana ulinikata coz nilijua ni mke wa mtu tayari naweza harib ndoa yake coz me nisingeweza kumwoa. Wanasema hakuna anayejua ya kesho.

Uzuri tuliachanaga vizuri na alikua anaonesha kunionea huruma na alikua tyr kunisaidia ila mimi jeuri nisaidiwe na dem? Hapana nilikaza hata simu zake nilikua sipokei namwonaga kwa mainsta tu anakula maisha mara hyatt, mara dubai maisha haya tupendane aseee
 
Back
Top Bottom