Nimejifunza kitu kutoka kwa Zelensky

Nimejifunza kitu kutoka kwa Zelensky

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
Kuna KITU Cha kujifunza Kwa Rais wa Ukraine. Mwanzoni mwa uvamizi wa Russia nchini Ukraine, niliona Jeshi kubwa ambalo Kwa mategemeo yangu niliona kabisa mwisho wa zelensky na Ukraine.

Hata pale alipo wahamasisha wananchi kutoogopa niliona kabisa kwamba jamaa anajidanganya. Wote tulishuhudia ule msafara wa zaidi ya km 50 wa jeshi la Russia ukielekea Kyiv Kwa lengo la kuichaza kabisa. Lakini wote hatujui ule msafara uliisjia wapi.

Kile KITU kinanikumbusha msafara wa jeshi la pharaoh Kwa wa Israel lakini ukaishia kuzamishwa ndani ya bahari. Hakika ujasiri wa zelensky unatupa haya matokeo.

Huyu mtu ni wakupongezwa kabisa hata kama sisi ni pro Putin tujifunze KITU hapa. Ndugu zangu Siri ya mafanikio Iko Kwenye ujasiri
 
Kuna KITU Cha kujifunza Kwa raisi wa Ukraine. Mwanzoni mwa uvamizi wa Russia nchini Ukraine, niliona jeshi kubwa ambalo Kwa mategemeo yangu niliona kabisa mwisho wa zelensky na Ukraine.

Hata pale alipo wahamasisha wananchi kutoogopa niliona kabisa kwamba jamaa anajidanganya. Wote tulishuhudia ule msafara wa zaidi ya km 50 wa jeshi la Russia ukielekea Kyiv Kwa lengo la kuichaza kabisa. Lakini wote hatujui ule msafara uliisjia wapi.

Kile KITU kinanikumbusha msafara wa jeshi la pharaoh Kwa wa Israel lakini ukaishia kuzamishwa ndani ya bahari. Hakika ujasiri wa zelensky unatupa haya matokeo. Huyu mtu ni wakupongezwa kabisa hata kama sisi ni pro Putin tujifunze KITU hapa. Ndugu zangu Siri ya mafanikio Iko Kwenye ujasiri
 
Kuna KITU Cha kujifunza Kwa raisi wa Ukraine. Mwanzoni mwa uvamizi wa Russia nchini Ukraine, niliona jeshi kubwa ambalo Kwa mategemeo yangu niliona kabisa mwisho wa zelensky na Ukraine...
😂😂
Wakati ule msafara wa kutisha wa vifaru na mizinga wa Putin wa urefu wa km 64 ukiwa unajongea Kyiv kwa mbwembwe, Zelensky alipewa ofa ya kusaidiwa kutoroka akagoma!

Wapiganaji wa Putin waliobahatika kuondoka wakiwa hai baadaye, walisepa kimyakimya bila yale mamitambo baada ya kugeuzwa screpa!
 
bila NATO Kyiv ingekuwa mikononi mwa jeshi la Putin ila Putin nae siku nyingine ajipange vizuri kabla ya kuanzisha vita maana anatukatisha sana tamaa team Kiba
Huwezi weka full scale war wakati hujajua katumwa na nani na mwisho ni nini hivyo Russia ni kama kaweka pose kuusoma mchezo pia vita kamili haikuwepo ndio maana wanaokufa ni wakuhesabu
 
Mkuu umeongeza pilipili km 50 siyo ndogo mkuu
Pengine hufatilii, jamaa yupo sahihi. Ule msafara ulipukutika saana, Russia alipeleka vijana wa kawaida tu mwanzoni mwa vita ila hata sasa bado ngoma ipo ngumu kuikamata Ukraine.
 
[emoji23][emoji23]
Wakati ule msafara wa kutisha wa vifaru na mizinga wa Putin wa urefu wa km 64 ukiwa unajongea Kyiv kwa mbwembwe, Zelensky alipewa ofa ya kusaidiwa kutoroka akagoma!

Wapiganaji wa Putin waliosalimika kuondoka wakiwa hai, walisepa kimyakimya bila yale mamitambo baada ya kugeuzwa screpa!
Armed vehicles na tanks nyingi viliachwa wakaondoka wao kama wao. Waligundua kuwa Ukraine ana silaha za kuangamiza ule msafara, sana sana drones na anti tank missiles kama javeline, wakaona ili kutoka salama ni kutoka kwa migui tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kupongweza kwa kuwaskiliza wamagharibi huku nchi yake ikigeuzwa vifusi, endeleeni kujichekesha huku mkijitekenya wenyewe, babu yenu mkuu wa umoja wa mataifa kaenda Moscow kuomba Urusi astopishe kichapo huku akilia kwahio nyinyi mnajua zaidi kuliko wao [emoji16][emoji23][emoji23] sawaaaa
 
😂😂
Wakati ule msafara wa kutisha wa vifaru na mizinga wa Putin wa urefu wa km 64 ukiwa unajongea Kyiv kwa mbwembwe, Zelensky alipewa ofa ya kusaidiwa kutoroka akagoma!

Wapiganaji wa Putin waliosalimika kuondoka wakiwa hai, walisepa kimyakimya bila yale mamitambo baada ya kugeuzwa screpa!
... hapajawahi kutokea msafara mrefu wa kijeshi wenye kila aina ya zana na majemedari kama ule tangu kuumbwa dunia hii! Ila ulivyoyeyuka kama umande wa asubuhi isisalie hata bunduki moja iliyobaki nzima pasi na kuharibiwa Mungu pekee anajua! Ajabu hili lisipoingia kwenye Guinness Book of Records itakuwa ajabu lingine!
 
Back
Top Bottom