Nimejifunza mengi kutoka kwenu, lakini bado nahitaji ushauri

Nimejifunza mengi kutoka kwenu, lakini bado nahitaji ushauri

roselyn2

Member
Joined
Jun 7, 2022
Posts
86
Reaction score
388
Hello JF members,

Ilibaki kidogo tu nijiengue ndani ya JF baada ya kupondwa na wengi kuhusu tatizo langu lililousumbua moyo wangu, lakini ntafanya nini, sikuwa na mtu wa kumlilia, ndo maana niliamua kuanika dukuduku la moyo wangu kwenu nikiamini ningepata kutiwa moyo, lakini ilikuwa tofauti

Labda utoto still unanisumbua, ni mgeni katika mapenzi, mwanaume pekee ambaye hajaumiza moyo wangu ni aliyenifunza mapenzi, tuliachana kwa amani pasipo maumivu yoyote yale na kwa sababu maalumu

Kwamba pesa ya mwanaume hailiwi bure [emoji3][emoji3] Nalijua hilo, lakini sijui niwaeleze vipi kumhusu huyu mwanaume ili muone kuwa mimi ni mwenye haki
Sikutegemea kwakweli [emoji3064][emoji3064]

Nilimkuta kapuku, hakuwa na pesa, nikam offer mpaka pesa ya chakula na nauli kutoka kazini kwake kwa miezi miwili, alikuwa ni wa kuniheshimu sana, kiukweli nilimpenda sana

Sasa amepata vicent, anashindwa hata kurudisha fadhila, anahitaji tufanye mapenzi ili anipatie pesa zake alizozitengeneza kwa msingi wangu, najua leo kwangu kesho kwake, kwani nami kipindi cha nyuma nilikuwa hivi?

Mbona penzi nilimpatia bure kabisa? Tena kwa upendo wote? Tena kwangu? Leo hii kumuomba pesa kwa dharura ananipa masharti ya kwenda kwake na jua lote eti tufanye mapenzi kwanza? Kwani kigeni kwake kutoka kwangu ni kipi mpaka awe na tamaa ya ajabu kiasi icho? Kwani haniamini tena? Thamani yangu anaifananisha na nini kwa sasa? Mwanaume pekee niliempenda, nimeacha wangapi mimi mwenzenu, nimekataa wangapi ili kumtunzia heshima? Na ninyi mnafungua midomo yenu kutetea upuuzi?

Sasa napata kuamini kuwa hakuna mwanaume mwaminifu, hata hawa ninaowaona mtaani wakijifanya kuniulizia na kunitupia macho ya tabasamu na bashasha wananidanganya, huenda wamo humuhumu na ndio wachangiaji wakubwa kunitusi na kunikebehi

Nilimpenda bure jamani, hakuwa na kitu, leo hii nakatiliwa namna hii? asante mungu, ipo siku [emoji24][emoji24]

MSAADA NINAO UHITAJI KUTOKA KWENU
Kwa sasa sitaki kutegemea tena pesa za mwanaume yeyote yule, hata za boss wangu (mshahara) sizihitaji tena maake inaelekea atakuja tu kunitaka kimapenzi nikose cha kufanya kwa kuhofia kupoteza kazi, kisha nimkabidhi penzi, aumize moyo wangu, nirudi kwenu kulia, mnishushue tena

Kwa kiasi hiki cha laki moja nilichonacho mkononi sasa hivi, natamani kukifanya mtaji kiasi kwamba hata kesho nianze biashara yangu mwenyewe nikiwa huru, niachane na mambo ya ku supply bidhaa za watu, una drive gari zao wanaishia kukusimanga kuwa pesa za mafuta unakula, mara unachelewesha mizigo, at the end taarifa zinafika kwa boss, badala atake action utamsikia anakwambia "tulia Rose, achana na maneno ya watu" mwanaume hajawahi kuwa mwema kiasi hiki, kuna kitu anakitafuta kwangu, na ni mume wa wake watatu, anakesha club nnavyosikia, siku nyingine anakuja ananukia k vant

Hivyo itapendeza kama mtanishauri biashara ya kufanya kwenye hili jiji la watu kwa kiasi hicho cha laki ili nitengeneze pesa zangu, niishi maisha yangu mwenyewe

Pindi ntakapopokea mshahara tarehe 8 July ntatenga kiasi cha laki mbili ili nifungue biashara nyingine, au nikuze biashara mtakayonishauri kufanya

Sintojari status yangu mtaani, urembo ntatupa kule, aibu nitaitoa machoni mwangu ili mradi najua ninachokitafuta ni kipi, malengo yangu ni yapi

Please, nahitaji ushauri wenu

NB: Samahani kwa mwandiko wangu mbovu
 
Hello jf members,
Ilibaki kidogo tu nijiengue ndani ya jf baada ya kupondwa na wengi kuhusu tatizo langu lililousumbua moyo wangu, lakini ntafanya nini, sikuwa na mtu wa kumlilia, ndo maana niliamua kuanika dukuduku la moyo wangu kwenu nikiamini

NB: Samahani kwa mwandiko wangu mbovu
Rose mbona naona kama vilr uko after our comments tyu huna ukweli wa kile usemacho hasa kuacha kazi dada ? Sorry

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Pole sana.

Ila nasikitika kukwambia kwamba huwezi zikimbia tamaa za wanaume kama unavutia.

Unauza bidhaa ya sh. 100 mtu atataka kuinunua kwa 10k, unauza mgahawa kibali ni kiasi kadhaa plus usumbufu au bure plus mbususu bila usumbufu!!

Ila mkuu komaa na ukomae sana, wanawake mnasumbuliwa mno huku mtaani aisee, ila komaa utataoboa.
 
Rose mbona naona kama vilr uko after our comments tyu huna ukweli wa kile usemacho hasa kuacha kazi dada ? Sorry

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Kuacha kazi ni long plan kaka, sina imani na wenzangu, ukizingatia wengi ni wakina dada kama mimi, unafiki unakuwa mwingi, masimango na kejeli, ukizingatia wenyewe wana vyeo kunizidi

Wivu tu kwa kweli
 
Hebu muulize mzee Halima anafanyaje maana sijawahi kumuona na boyfriend. Kama yeye anaweza kuishi bila mwanaume na ni mrembo mzuri tu halafu kijana mdogo, iweje wewe ushindwe?
 
Wanaumeme wenzangu mnaniwakilisha vema.nilijuaga ni hela yangu tu ndio hailiwi bure kumbe wengi mko kama mimi! Hawa wanawake siku hizi wengi ni omba omba hivo akipiga kizinga ela afate geto.akija kama hataki kuliwa arudi aliko toka.tena ikibidi arudi na miguu,akate mtaa kwa mtaa
 
SHERIA zipo komaa na kazi...huku ukifanya biashara...lakini ukikurupuka kuacha kazi utaangukia kwenye mikono ya wanaume ambao wewe umeanza kuwachukia...ila kikubwa mimi ninachokiona ni kuwa moy wako wote upo kwa mwanaume wako wa kwanza ndio maana kila utakacho fanyiwa na mwanaume mwingine unaona kama anakulipisha.
 
Yaani uanzishe biashara ili kuepuka wanaume.!??... hao wateja hawatakutongoza.!??... Hio mizigo utakuwa unanunua kwa madada pekee.!??...

Sababu yako ya kuanza biashara haina Mashiko,,, sitegemei kama biashara itastawi...

Kwa Laki moja,,, Kanunue KUKU shekilango,,, wakaange,,, kawauze kwa MWAMPOSA siku ya ibada..,,,au kachukue Dagaa Ferry uje uwauze mtaani kwa mafungu...

Usikurupuke,,, tuliza Akili....
Na ukitaka hela ya Mwanaume tena,,..Epuka kutaka mzigo upewe bei cheee au mikopo,,, ,kutaka hela za haraka,safari za bodaboda za mikopo,, ...tofauti na hivyo BASI MWENDO NI ULEULE.... UTATIWA TU,,, so hujatuepuka kwa 100%,,,tuepuke kuanzia kichwani mwako(Msimamo na Jifunze kujitegemea) .. sio Maneno maneno..

Barikiwa
 
Yani nakufananisha na mchepuko wangu mmoja anaitwa irene. Kwa jinsi unavyoandika.

Akituma sms kama gazeti Najikutaga namfikiria badala ya kufikiria sms aliyotuma.

Huwa kuna mda akili mnaziazimaga?

Ushauri wangu. Jaribu kuorodhesha vipaumbele vyako.

Mmu
hoja mchanganyiko
biashara

Thread yako kote inaingia.
 
Back
Top Bottom