Nimejifunza pakubwa kuhusu elimu ya fedha baada ya jamaa yangu kuchukua mkopo wa Milioni 10 kazini kwake ili anunue gari

inasikitisha sana asilimia kubwa ya watumishi hawana elimu na uelewa wa fedha kinachotuponza watanzania wengi tunaishi kwenye macho ya watu zaidi kuliko uhalisia wetu..... tunateswa sana na maisha ya wengine hatuishi kufanya makosa yale yale tunayoona wenzetu wamekosea
 
Yaani mtu ajenge nyumba halafu useme ametumia mkopo kwenye vitu visivyo na faida?

Anyway siwezi kukulaumu sana maana inawezekana unaishi maeneo ya ndanindani huko ambako thamani ya nyumba haionekani ila kwa mtu aliyepo kwenye miji iliyochangamka hawezi kutamka hii kauli nyumba eti ni matumizi mabaya ya mkopo.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Watumishi msiogope kukopa. Kopa Kwa malengo mazuri yenye faida hata Kwa baadae( uwekezaji), Usikope mkopo wa Muda mrefu ishia miaka mi tatu. Usikope Kwa riba kubwa.
Maisha ya ajira ni mafupi Sana.
 
 
Ila Kuna muda walimu tunazingua,

Kuna mjinga mwingine tulikuwa naye school moja, ameajiriwa baada ya kupata baria ya uthibitisho tu kakopa kachukua RAUM

Wakati huo amenumua gari anakaa kwenye nyumba za walimu hapo hapo shuleni, maana shule ni ya boarding

Ameendesha gari mwaka tu akapata ajali (alikuwa amelewa)

Pesa ya matengenezo hana, akaamua kuiuza
 
Waalimu huwa wanafundishwa kozi ya ujinga kwa siri wakiwa vyuoni? Hakuna mtu makini atachukua mkopo bila kupiga vizuri hesabu za riba. Na inajulikana ukilipa mapema ndo riba inakuwa ndogo. 10m kuilipa kwa 6yrs ni umaskini uliokithiri.
Ujinga huo afundishe nani?

Shida kubwa walimu wengi wametoka mazingira ya kimaskini ( automatically umaskini upo ndani ya comfort zone na kutoka humo ni shida nyingine)

Kesi hizo zipo sana kwa watumishi wengi ila walimu ni representative tu kwa kuwa wapo wengi
 
Watumishi wengi wamekuwa masikini sababu ya mabenk.
Bank si msaada ni mfumo wa kifreemason wa kuchukua pesa bila jasho toka kwa watu masikini.
 
Bora angebeti,mabenk yapo kwa ajili ya kuwafilisi watumishi.
Nmb na crdb bila watumishi wa serikali zingeshajifia.

watumishi wao wana hasara gani. kwani wao wanfanya biashara gani hadi useme wanafilisiwa.

kuna mwl flani ana likizo ya ugonjwa mwaka wa tatu sasa Yuko nyumbani mwisho wa mwezi anakwenda kuzikinga kunako ATM Machine
 
Hii chai kama chai nyingine 😂😂
Ukikopa 10M kwa miaka 5 unalipa roughly 15M sio hio 20M yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…