Nimejikaza ila nimeshindwa

Nimejikaza ila nimeshindwa

didy muhenga

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
861
Reaction score
1,476
Wakuu nimeliweka moyoni na jaribu kulificha ila ngoja tushee labla mawazo chanya yatapatikana. Inshort natarajia kuoa japo ndoa yenyewe inapingwa kama katiba mpya na CCM na mpingaji ni mama yangu akidai hataki nimuoe huyu binti kutokana na shughuli yake.

Huyu binti ni mwanasiasa wa chama fulani na yupo na cheo fulani kwenye vijana kikubwa tu sitopenda kushea. Sasa mama yangu ni conservative anadai wanasiasa ni washirikina pia anaona kama kwenye kauli ndani ya nyumba na masuala ya mali atanisumbua.

Sasa inanisumbua kutokana mimi na mawasiliano mazuri na familia ya mwanamke na wananijali kinipigia sana hata kwenda kupata msosi ila mama yangu hajawahi hata kumpigia smu huyu mchumba wangu na akipigiwa anaweza asipokee au akipokea hataki kuongea kwa ushirikiano yaan kizungumkuti japo binti bado ana imani tutaoana tu.

MODS huu uzi usitumiwe kweny mtandao wowote tofaut na humu kwasababu mwenzangu atauona huko X na Instagram ila humu hana account na wala hajawahi ingia.
 
Ukiona mwanamke ni mwanasiasa na haijui jamii forums basi ni mnafki na mshirikina tu chawa wa ccm

Ushauri wangu....ongea na Maza vizuri kabisa mwambie kwann unampenda chawa wa mama mwambie jinsi gani chawa anakuelewa Nina uhakika mama yako ni muelewa sana.

Maendeleo hayana chama.
 
Ndoa ni maamuzi ya watu wawili kama mnapendana huyo binti atakusikiliza.Hayo ya mama yachuje kwa umakini maana mwenye kuoa ni wewe.Kama mama ana vigezo vya msingi vichunguze.Pia tafuta watu wachunguzi au watu wazima wenye ufahamu wakushauri kabla ya uamuzi wa kufunga ndoa.Pia waongee na mama ili mjue shida ilipo
 
Nilimpemda sana binti mmoja pamoja na kuzaa nae lakini maza alikuwa hataki, nilidumu. Sana na binti na tulikuwa tunapendana sana..

Mahusiano mama alikuwa haingilii ila suala na kuishi nae alilipinga sana, nikajifanya mjanja nikaanza kuishi nae, haijapita miezi6 kilichonikuta.. nashukuru nime recover na life inaendelea..
 
Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu ,sikio lakufa halisikii dawa .endelea kushupaza shingo sehemu ambayo mzazi anaona unaenda kuangamia ,kuna siku utayakumbuka maneno ya mama yako .

Sikiliza nyimbo ya LUCKY DUBE _ MAMA itakufunza mengi , Lucky dube alipata mpenzi wakapanga kuoana , Dube akaona siyo mbaya ngoja amshilikishe mama yake ,Dube akampigia simu mama yake akamwelezea jambo lake huku akimmwagia mpenzi wake sifa kedekede kwa mama yake mzazi , mama Dube alimjibu mwanae "kuwa umechukua muda mzuri wakumsoma mwenza wako ? Dube akamwitikia mama yake nakusema ndiyo kwanza ni mtu mwema sana, basi buana akaoa ile kuishi wakapeana talaka ,Dube akarejea kwa mama kumweleza ila mama alimfariji mwanae tu huku Dube akijutia.

USHAURI FANYA MAAMUZI SAHIHI NDOA INAWEZA KUWA NDOANO BAADA YAKUPATA MTOTO MMOJA AU BAADA YAKUDHOEANA.
 
Huyu binti ni mwanasiasa wa chama fulani na yupo na cheo fulani kwenye vijana kikubwa tu sitopenda kushea. Sasa mama yangu ni conservative anadai wanasiasa ni washirikina pia anaona kama kwenye kauli ndani ya nyumba na masuala ya mali atanisumbua.

Sasa inanisumbua kutokana mimi na mawasiliano mazuri na familia ya mwanamke na wananijali kinipigia sana hata kwenda kupata msosi ila mama yangu hajawahi hata kumpigia smu huyu mchumba wangu na akipigiwa anaweza asipokee au akipokea hataki kuongea kwa ushirikiano yaan kizungumkuti japo binti bado ana imani tutaoana tu.
- Jipe muda

- Kaa na mama kwa Nyakati tofauti,

- Ongea naye kwa kina mara zote hizo, Usioneshe kuwa kama unamlazimisha , bali iwe ni sehemu ya maongezi kawaida.

- Hakikisha Mahusiano yako na huyo mpenzi wako haya haribu ukaribu wako na Mama .

- Hakuna Kama Mama , (Na pia hakuna kama Baba).

- Ikishindikana kufikia muafaka wewe na Mama basi waweza anza kuangalia baadhi ya Viongozi wa dini ambao utashare nao hili linalokuumiza kichwa na wao watasaidia kuzungumza na Mama.

- Muhimu ni Mama alidhie kwa Moyo Mweupe, Na hakika furaha ya Ndoa itapatikana na utafurahia.

- Narudia Tena, Usilazimishe mambo, Nenda taratibu Na Mama.

- Sikilziza kwa umakini huu wimbo.
 
Natumaini akili unazo tena ambazo ni timamu,,,pima anachokisema mama,kwa jinsi unavyomfahamu vyema kiundani huyo binti na uzoefu kutoka kwa vijana wenzio na wazee utapata kitu kikubwa cha kujua nini ufanye ila usije ukaoa kabla ya kumaliza tofauti na mama mzazi kama ni muelewa
 
Back
Top Bottom