Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu ,sikio lakufa halisikii dawa .endelea kushupaza shingo sehemu ambayo mzazi anaona unaenda kuangamia ,kuna siku utayakumbuka maneno ya mama yako .
Sikiliza nyimbo ya LUCKY DUBE _ MAMA itakufunza mengi , Lucky dube alipata mpenzi wakapanga kuoana , Dube akaona siyo mbaya ngoja amshilikishe mama yake ,Dube akampigia simu mama yake akamwelezea jambo lake huku akimmwagia mpenzi wake sifa kedekede kwa mama yake mzazi , mama Dube alimjibu mwanae "kuwa umechukua muda mzuri wakumsoma mwenza wako ? Dube akamwitikia mama yake nakusema ndiyo kwanza ni mtu mwema sana, basi buana akaoa ile kuishi wakapeana talaka ,Dube akarejea kwa mama kumweleza ila mama alimfariji mwanae tu huku Dube akijutia.
USHAURI FANYA MAAMUZI SAHIHI NDOA INAWEZA KUWA NDOANO BAADA YAKUPATA MTOTO MMOJA AU BAADA YAKUDHOEANA.