Nimejikuta nawaonea wivu mkubwa mno Wakenya

Ki Mun

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
3,442
Reaction score
4,388
Namtazama John Kerry anavyowasifu kwa kuendesha uchaguzi kistaarabu na kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kukusanya na kujumlisha matokeo na kukamilisha process nzima ndani ya siku 2 tu za uchaguzi, observers wote kutoka UE, Africa Union, EAC wanaonesha kuridhika mno na uchaguzi...nakosa la kusema zaidi tu ya kuwaonea wivu hawa jamaa wa taifa hili lililostaarabika na lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki;

Hakika ndugu zetu hawa wako level nyingine kulinganisha na Dictators Club ya akina Kagame, Museveni, Nkurunzinza, Kabila na huyu mwenzao bendera fuata upepo asiyejua kama jua hukucha na kuchwea...chaguzi katika nchi zetu hizi ni political nonsense, nothing short of that!

Hongereni Wakenya, endeleeni kuijenga nchi yenu kuwa mfano wa taifa la kistaarabu kabisa katika Africa, taifa lenye uchumi imara, taifa lenye wasomi wanaojitambua...hongereni sana Mazee!
 
Kuna uraia wa watanzania unamashaka, Kumwingiza Rais mwenye miaka 2 na genge la dictators ni chuki dhahiri binafsi. Maoni mazuri sana umetoa ila generalisation huwa sio nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namtazama John Kerry anavyowasifu kwa kuendesha uchaguzi kistaarabu na kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kukusanya na kujumlisha matokeo na kukamilisha process nzima ndani ya siku 2 tu za uchaguzi, observers wote kutoka UE, Africa Union, EAC wanaonesha kuridhika mno na uchaguzi...nakosa la kusema zaidi tu ya kuwaonea wivu hawa jamaa wa taifa hili lililostaarabika na lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki;

Hakika ndugu zetu hawa wako level nyingine kulinganisha na Dictators Club ya akina Kagame, Museveni, Nkurunzinza, Kabila na huyu mwenzao bendera fuata upepo asiyejua kama jua hukucha na kuchwea...chaguzi katika nchi zetu hizi ni political nonsense, nothing short of that!

Hongereni Wakenya, endeleeni kuijenga nchi yenu kuwa mfano wa taifa la kistaarabu kabisa katika Africa, taifa lenye uchumi imara, taifa lenye wasomi wanaojitambua...hongereni sana Mazee!
Ngoja kwanza liishe suala la Form34A na B
 
hiyo club ya dikteta tusipoangalia huyu mchattle atakua mwenyekiti

kwa mwenye uwezo atutaftie ile katuni ya GADO tuangalie ancole maguri akijifunza kwa mfalme wa BUGANDA
 
Namtazama John Kerry anavyowasifu kwa kuendesha uchaguzi kistaarabu na kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kukusanya na kujumlisha matokeo na kukamilisha process nzima ndani ya siku 2 tu za uchaguzi, observers wote kutoka UE, Africa Union, EAC wanaonesha kuridhika mno na uchaguzi...nakosa la kusema zaidi tu ya kuwaonea wivu hawa jamaa wa taifa hili lililostaarabika na lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki;

Hakika ndugu zetu hawa wako level nyingine kulinganisha na Dictators Club ya akina Kagame, Museveni, Nkurunzinza, Kabila na huyu mwenzao bendera fuata upepo asiyejua kama jua hukucha na kuchwea...chaguzi katika nchi zetu hizi ni political nonsense, nothing short of that!

Hongereni Wakenya, endeleeni kuijenga nchi yenu kuwa mfano wa taifa la kistaarabu kabisa katika Africa, taifa lenye uchumi imara, taifa lenye wasomi wanaojitambua...hongereni sana Mazee!
Tusipo kubali kupambana na hali yetu sisi kama Tanganyika, na kuendelea kukikumbatia ama kung'ang'ania Kisiwa cha Zanzibar (kama sehemu ya Muungano) wakati wenyewe hawana haja wala nia ya dhati katika kuulinda na kuuenzi Muungano wenyewe, tusitarajie Muujiza wa Chaguzi ya Haki na Amani Daima....!!

Tazama/fuatilia kumbukumbu ya Chaguzi zilizo pita....

Wazanzibari siku zote ndio jamii/sehemu ya watu wanatia dosari katika Uchaguzi wa Tanzania, na yote hii ni kwa sababu ya kulazimisha kutaka kuwatawala watu wanaohisi hawana faida na Muungano uliopo....!!

Achia Zanzibar ijitegemee, huku Bara tupambane wenyewe kuuondoa Utawala utakao onesha dhahiri hauendani sambamba na matakwa ya wananchi.

Kwa hatua na maamuzi haya, lazima katika nchi yetu, itapatikana Demokrasia na uchaguzi wa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli lazima usemwe! Kwa habari ya uchaguzi Kenya wako sayari nyingine kabisa ukilinganisha na nchi zingine za afrika ya mashariki! Haitofaitiani sana na ulaya! Uchaguzi wao uko wazi mno! Matokeo unayapata kwa SMS wakati wowote! Pia matokeo ya rais ni ruksa kuyapinga mahakamani!
Tatizo la Kenya ni ukabila! Raila na ngome yake ya kikabila Kisumu na Kenyatta na ngome yake ya kikabila rift valley!
 
Kenya wapo vizuri kila idara kulinganisha na hii nchi ya kusadikika ..
 
Back
Top Bottom