Nimejikuta nawaonea wivu mkubwa mno Wakenya

Nimejikuta nawaonea wivu mkubwa mno Wakenya

Kenya na uchaguzi wao ni kitu ingine kabisa mno................ kwa kweli mbona wale wa ile club nao si walifanya uchaguzi tar sijui 2 au ngapi na sijasikia nani kashinda........ rally inafanyika week3 subamishi
 
Namtazama John Kerry anavyowasifu kwa kuendesha uchaguzi kistaarabu na kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kukusanya na kujumlisha matokeo na kukamilisha process nzima ndani ya siku 2 tu za uchaguzi, observers wote kutoka UE, Africa Union, EAC wanaonesha kuridhika mno na uchaguzi...nakosa la kusema zaidi tu ya kuwaonea wivu hawa jamaa wa taifa hili lililostaarabika na lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki;

Hakika ndugu zetu hawa wako level nyingine kulinganisha na Dictators Club ya akina Kagame, Museveni, Nkurunzinza, Kabila na huyu mwenzao bendera fuata upepo asiyejua kama jua hukucha na kuchwea...chaguzi katika nchi zetu hizi ni political nonsense, nothing short of that!

Hongereni Wakenya, endeleeni kuijenga nchi yenu kuwa mfano wa taifa la kistaarabu kabisa katika Africa, taifa lenye uchumi imara, taifa lenye wasomi wanaojitambua...hongereni sana Mazee!

😱 😱 😱 Haa! kwa posti hii lazima ukapimwe mkojo...
 
Ki ukweli kuna vitu hawa jamaa wakenya wametupiga gap, ila hulka zetu tu binadamu kukubali inakuwa ngumu.... Hongera kwao kwa zoezi la uchaguzi tangu campaign hadi hitimisho kwenye box la kura.

"A voice of one calling in the wildernes"
Na huu ndo ukweli,
Matanzania ni ya kubuluzwa tu.
Badilikeni matanzania mnaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusipo kubali kupambana na hali yetu sisi kama Tanganyika, na kuendelea kukikumbatia ama kung'ang'ania Kisiwa cha Zanzibar (kama sehemu ya Muungano) wakati wenyewe hawana haja wala nia ya dhati katika kuulinda na kuuenzi Muungano wenyewe, tusitarajie Muujiza wa Chaguzi ya Haki na Amani Daima....!!

Tazama/fuatilia kumbukumbu ya Chaguzi zilizo pita....

Wazanzibari siku zote ndio jamii/sehemu ya watu wanatia dosari katika Uchaguzi wa Tanzania, na yote hii ni kwa sababu ya kulazimisha kutaka kuwatawala watu wanaohisi hawana faida na Muungano uliopo....!!

Achia Zanzibar ijitegemee, huku Bara tupambane wenyewe kuuondoa Utawala utakao onesha dhahiri hauendani sambamba na matakwa ya wananchi.

Kwa hatua na maamuzi haya, lazima katika nchi yetu, itapatikana Demokrasia na uchaguzi wa haki.



Sent using Jamii Forums mobile app

Duh Toyota escudo
 
Back
Top Bottom