Nimejiondoa kwenye makundi sogozi ya harusi

Ifike wakati harusi ziwe simple tu ,wawe wahusika(mke na mume) na wapambe wa maharusi then ndugu wawili wa upande wa kike na wa kiume pamoja na mashahidi wa upande wa kike na wakiume basi.

Siyo Bonge la sherehe baada ya miezi 6 wanaachana.
Na haya mambo yameanza kubadilika baada ya watu kuanza kugeuza ndoa za watu miradi ya kibiashara.
 
Michango noma sana..
Huwezi ni add kwa group hadi niruhusu, na huwa sikubali magroup ya harusi na sichangii harusi yoyote hata iwe ya ndugu.. kama hamuwezi kujigharamia au kwenda mkafunga ya kawaida mkala ugali na nyama basi..
 
Huwa ni kero sana kusema ukweli!!! Hii mambo tubadilike..... inatosha kama familia mna changiana kimya kimya maisha yanaendelea
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ifike wakati harusi ziwe simple tu ,wawe wahusika(mke na mume) na wapambe wa maharusi then ndugu wawili wa upande wa kike na wa kiume pamoja na mashahidi wa upande wa kike na wakiume basi.

Siyo Bonge la sherehe baada ya miezi 6 wanaachana.
Huko nyuma,1990s harusi lilikua suala la familia na ukoo,huu ushenzi wa kuchangisha watu unakuta bajeti 13m sijui alianzisha nani!? Kama huwezi gharamia harusi yako kwanini usingoje utapoweza!? lazima kwenda ukumbini!? fanyia kwenu, watu wale pilau suala liishe.
 
Mimi Huwa napima uzito wa mahusiano na wahusika


Kama mahusiano yetu mepesi sana Wala sichangii
 
Elfu 50 ndiyo inakufanya useme yote haya mkuu?
Haelewi kazi ya magroup ya harusi anadhani ni harusi tu alivyo mjinga

Mle mna kufahamiana, hata msiba ukipata magroup hayo ndio ya kukubeba, bado connections za kibiashara, ajira nk

Watu wengine hadi hupata kura wakigombea kupitia hayo magroup nk

Uliza wagombea uongozi nyadhifa mbalimbali wanavyopenda hayo magroup nk

Nafikiri hajielewi na haelewi group ni nini?
 
Njia nyingine ya kidiplomasia ya kugoma kuchanga ni kwamba wakiku-add kwenye group, we tulia watatoa orodha ya ahadi we tulia, watahamasisha wee wala usijibu chochote, watamaliza kuchangishana, harusi itafanyika, watu wataanza kuleft we umetulia tu, baadae unabaki peke yako ndio hapo utaanza kutamba kutuma chochote kwenye group kiroho saaaaafi [emoji23][emoji23].
 
Huwa ni kero sana kusema ukweli!!! Hii mambo tubadilike..... inatosha kama familia mna changiana kimya kimya maisha yanaendelea
Kwa waafrika ni sehemu ya utamaduni.

Nenda vijijini huko mtu hata awe ndugu wa karibu pesa hana atakuja na chakula.

Rafiki ndio kabisa anaweza leta mbuzi au ng'ombe au gunia la mchele sababu pesa hawana huenda na vyakula mtu hawezi tu kwenda harusi ya mtu kijijini bila kutoa chochote.

Ni utamaduni wa kiafrika na umeanzia mbali mfano vijijini mtu ukisafiri kwenda kuona ndugu au rafiki lazima utabeba walau maharage, mboga au chochote.

Mijini ndio unasikia mgeni hodi yuko, mikono mitupu anakuja kula kwa mwenyeji.

Hiyo culture ya kwenda harusi au msiba wa mtu bila kuchangia chochote sio mila hasa za kiafrika ni za kizungu na haziko sahihi.
 
Kwani ujui sikuizi MA-MC wanakula wapi [emoji849][emoji849] kama ujui mtafute MC mwenzako mashuhuri MC-MBOWE atakuambia sikuizi kuna MA-MC WALAMBA ASALI

Huyo ni DJ sio MC
 

MC ni kazi hata serikali inaitambua na ndio maana serikali ilipanga kuanza kutukata kodi...

Kwa habari ya madalali siwezi wasemea, maana kuna utofauti mdogo sana kati ya dalali na tapeli...
 
M/kiti wa kamati ndo wanakuaga Wana shobo afu usiombe awe mlezi kila muda anawaza michango tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…