Nimejiridhisha: Wana-Kagera ni 'nshomile' kweli. Waliyoyaamua dhidi ya Dkt. Magufuli mioyoni mwao ni mazito!

Nimejiridhisha: Wana-Kagera ni 'nshomile' kweli. Waliyoyaamua dhidi ya Dkt. Magufuli mioyoni mwao ni mazito!

Hawana uhakika hata wa mlo mmoja kwasabb ya Magufuli. Ndiyo maana wanachanga ili 28/10/2020 aondoke mazima waanze kula milo 3. Kumchagua Magufuli ni kuchagua kifo.
Mkuu unadhani hii michango itafanikisha kile mnachotamani na kukiota?
 
Acha uongo ,ww mzee.Tupe statistics umeongea na watu wangapi?Ili taarifa zako ziwe significant. Au JF ni kijiwe cha uongo tu.
Kwa upande wako Magufuli alichowafanyia wana Kagera wakati wa tetemeko ni sawa?
 
Katibu mkuu wa CCM nilimuokota kemondo alikuwa anauza ndizi, process ana amestahafu Ila kwangu mimi ajihesabu hajastahafu serikalini Kuna nafasi nyingi sana siwezi kukubali profesa mzima Tena Dada yangu hastahafu, Masilingi aliyekuwa mbunge wenu kabla ya profesa nilimteua kuwa balozi Marekani.

Kuna huyu alikuwa diwani wenu muleba anaitwa milanga alikuwa upinzani akaamia CCM Sasa hivi nimemteuwa kuwa katibu wa CCM uko kigoma. Alafu kuna graduate na akili zake timamu anasema Magufuli mitano Tena. Yani Kuna watu sijui ubongo wao una virus basi tu.
Kwahiyo prof Tibaijuka atapewa kazi tena.!! Kama ndivyo hivyo, Kwanini nafasi kama Hizo wasipewe Vijana wetu wasomi waziri tu wanaohangaika kutafuta kazi!?

Huyu prof alishafanya Sana kazi, amezeeka, amestaafu. Ndiyo taratibu za utumishi zilivyo. Kwanini mh Magu analazimisha arudi kazini? Amekosa kabisa mtu msomi mwingine Anayeweza kumpa hiyo kazi anayotaka kumpa Tibaijuka??
 
Ndio pa kujiuliza kama nchi haichukuliwi kwa pesa hii michango ya nini?
Nyerere alichukua nchi kutoka kwa waingereza kwa pesa? Alikuwa ana pesa kuliko wakoloni wa kingereza? Ila nauli ya kwenda UN alichangiwa sumni sumni, tuache bwana hatuna hazina wala mafisadi wote wamerudi kuunga mkono juhudi
 
Acha kumfananisha Nyerere na batiki la kibelgiji. Ruzuku za chama zinaenda wapi ikiwa makao makuu Ufipa haifana ninhata na ofisi ya Rungwe?
 
Magufuli anaponzwa na uwezo wake mdogo wa kuelewa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hivyo kumfanya adeal na petty issues ndo maana akadhani kumuahidi cheo Prof Tiba ndo yaweza kuwa njia ya kupata kura kagera. Lakini pia uwezo wake mdogo ndo unamfanya aamini kuwa maendeleo yanapelekwa sehemu na rais na CCM yake. Shame on him.

Wewe mwenye uelewa mkubwa wa mambo mbona hujagombea urais ili tukupe? Au wewe ni kiongozi gani?
 
Acha kumfananisha Nyerere na batiki la kibelgiji. Ruzuku za chama zinaenda wapi ikiwa makao makuu Ufipa haifana ninhata na ofisi ya Rungwe?
Una mihemko ya ki Lumumba isiyokupa nafasi ya kutumia ubongo badala yake utumie tumbo, mikono, sehemu nyeti nk. Hawana mafisadi wa kuwamwagia hela wote wamerudi kuunga mkono juhudi kwa anayetumia hela ya hazina kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake Chato.

Kama anachukua hela ya hazina bila bunge kuidhinisha atashindwa kuchukua afanyie kampeni? Hana tofauti na Mobutu
 
Huo uwanja wa ndege amejenga chumbani kwake? Kwani wananchi wa Chato hawastahili kuwa na uwanja wa ndege?
 
Huo uwanja wa ndege amejenga chumbani kwake? Kwani wananchi wa Chato hawastahili kuwa na uwanja wa ndege?
Mbona huulizi wananchi wa Butiama hawastahili? Wa Kipayo Songea hawastahili? Wa Msoga hawastahili? Kwa akili yako hata Mobutu alivyojenga uwanja wa ndege kijijini kwake Ghabolite alikuwa sahihi, tatizo naweza kuwa nazungumza na robot wanaoliprogram wako Lumumba huwezi kureason
 
Akimaliza Chato ataenda kwenye hayo maeneo uliyoyataja mpe mitano mengine.
 
Huo uwanja wa ndege amejenga chumbani kwake? Kwani wananchi wa Chato hawastahili kuwa na uwanja wa ndege?

Kwa nini atumie fedha za wananchi bila idhini ya wawakilishi .?
Alitakiwa aje kutuomba kwanza na atuambie kwa nini anaujenga, manufaa yake ni yapi na gharama yake ni upi
 
Kwa nini atumie fedha za wananchi bila idhini ya wawakilishi .?
Alitakiwa aje kutuomba kwanza na atuambie kwa nini anaujenga, manufaa yake ni yapi na gharama yake ni upi
Hamuwezi kuambiwa kila kitu kwani hata mkiambiwa mtapinga tu. We huoni Fly over, Standard gage, barabara za kutosha kila kona na bado mnapinga. Muambiwe nyie nani kwani?
 
Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.

Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.

Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.

Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)
Acha uchuro wee kwani wana kagera wote walibomokewa kwenye tetemeko lile? Alichofanya jpm tu ni kugeuza sehemu kubwa ya rambirambi kujenga majengo ya umma yaliyoharibika kama vile shule ofisi za serikali na hospitali. Kila muathirika alifidiwa kwa kiasi fulani. Nchi nzima walitoa rambirambi tena mashirika na idara za serikali ndio zilitoa mamilioni. Wewe ulitaka walioathirika watajirike kwa rambirambi? Isitoshe kuna mengi serikali ya jpm imefanya kwa mkoa. Watu kama wewe wanachotaka ni kulitia tembo maji.
 
Acha uongo wewe mzee. Tupe statistics umeongea na watu wangapi? Ili taarifa zako ziwe significant. Au JF ni kijiwe cha uongo tu.
Vp dawa imeingia ndipo??
 
Hata wakimkataa
Sisi maccm tutatafuta kura feki za kujazilizia kwa mgombea wetu
Nadhani labda hujaelewa vizuri. Safari hii tutakula sahani moja.

1600355643033.png

SASA BASI
 
Back
Top Bottom