Nimejiuliza sana hili Swali, ila sijapata Jibu sana sana naona najikuta Nacheka tu kila nikilifikiria Kichwani mwangu

Nimejiuliza sana hili Swali, ila sijapata Jibu sana sana naona najikuta Nacheka tu kila nikilifikiria Kichwani mwangu

Sura zetu tutaficha wapi sijui, wengine nadhani tutakuwa tayari tushabook tiketi za kwenda ughaibuni na kuukana kabisa uraia wa Tanzania, maana unawaza nitarudi vipi Mimi?
 
Hivi Siku mara paaaaap kwa bahati mbaya Sura zetu zote zikaonekana kwa dakika kama tano ( 5 ) katika Simu na Laptops zetu ambazo tunazitumia Kuchati au Kuandika mambo yetu mbalimbali hapa halafu Wote tukajuana kuwa kumbe ID ya fulani ni fulani itakuwaje baada ya hapo?

Ninayoyahisi........

1. Kuna ambao Gari za Polisi zitawafuata moja kwa moja Makwao kwani watakuwa wameshajulikana

2. Kuna ambao Ndoa zao Siku hiyo hiyo zinaenda Kuvunjika

3. Kuna ambao watapoteza Ajira zao huko Maofisini waliko Kwani Boss atajua nani anayemtukana JF

4. Kuna ambao watalazimika Kumalizia upesi Madeni yao kwa Kuogopa Aibu

5. Kuna ambao tutajua hata Matokeo yao ya Kitaaluma kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu

6. Kuna ambao Wauza Bangi / Bange watawajua na huenda kuwapa Habari za Mzigo mpya ulioingia

7. Kuna ambao watajulikana kuwa kumbe si Wanaume au Wanawake au ni Wapiga Miluzi wakuu Mijini

Naomba tu hii Bahati mbaya isije kutokea hapa kwani nina uhakika 99% ya Watu Wataumbuka au Tutaumbuka balaa.

Kama unajijua ni mwana Simba au Yanga halafu bado huna Tiketi ya Simba Day na Wananchi Day usichangie Uzi Ok?
Leo Most talented charsma fella umesema jambo,vipi wewe binafsi utaenda kujificha wapi?
 
Back
Top Bottom