macdemelo Leo, Septemba 06, 2025 nimemuandikia rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya uamuzi wangu kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Niliteuliwa Desemba 18, 2023 na nimehudumu kikamilifu majukumu yangu. Natoa shukrani nyingi kwa Wizara, Tume, na wajumbe wenzangu kwa ushirikiano mzuri walionipa katika kipindi chote.
Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili.