Nimekamatiwa pikipiki nikiwa naikokota kwenda kwa fundi

Nimekamatiwa pikipiki nikiwa naikokota kwenda kwa fundi

bab-D

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
1,215
Reaction score
322
Nikiwa barabarani nakokota pikipiki nikielekea kwa fundi, gafla akatokea jamaa kavaa kilaia, na kuniomba anikague, nikamruhusu, akabaini bima imeisha na element haikuwepo, nikaahilisha kwenda kwa fundi tukaenda polisi baada ya kuniamrisha hivyo,tulipofika wakaniomba leseni ikawa imekwisha mda wake,nikawaambia mbona nilikuwa nakokota nilikuwa siendeshi? wakajibu, hayo hatujui lipa faine tu, wanadai niripie sh 90,000/ nimeondoka kituon nitarudi kesho ili twende mahakamani,mnanishauri nini?, swali, je inaruhusiwa kukamata pikipiki inayokokotwa kwenda kwa fundi?
 
We kwanini ukubali kukaguliwa wakati unaipeleka kwa fundi. Woga wako ndio umaskini wako, we unajua pikipiki mbovu unaipeleka kwa fundi alafu unakubali kukaguliwa. Jiamini aisee!, hilo kosa lisingekuwa kubwa hivyo. Waambie ilikuwa ndani ndio ulikuwa unakwenda kuifufua na uipeleke kwa Insurance kulipia.
 
mbona makosa yapo wazi.....leseni haina uhusiano na ubovu bila pia haina uhusiano na ubovu
 
kwani wanauhakika km ww ndiye uliendesha usingekubali .kwani ilikuwa sio redhanded
 
We lipa faini makosa hayo hakikisha unapewa risiti yenye kiasi hicho.
 
Mimi sijaendesha na sijaandika popote kuwa niliendesha, wao nimefika tu akachukua kitabu na kuandika mapungufu,bila kujali kuwa nilikuwa nasukuma
 
We lipa faini makosa hayo hakikisha unapewa risiti yenye kiasi hicho.
Kwa nini nilipe wakati ilikuwa ndani na sijaendesha? mi nazani mahakamani ndo kutakuwa na haki.
 
Mimi sijaendesha na sijaandika popote kuwa niliendesha, wao nimefika tu akachukua kitabu na kuandika mapungufu,bila kujali kuwa nilikuwa nasukuma
Kutoka kwa fundi ingerudije home kwako? Lipa faini mkuu, mfuko wa Magufuli utune.
 
kusukuma unapaswa kuwa na leseni ndio na pikipiki inapaswa kuwa na bima muda wote
 
We sijui nikuiteje,mtu kaja kiraia anakukagua unakubali bila kujua ye ni nani,bado tena anakuambia twend kituon unakubali,hivi nikikupa katusi simple ntakua na makosa
 
Kitu cha muhimu ulichotakiwa kufanya(na kama kikotokea tena tukio kama hilo unatakiwa kufanya) yafuatayo( 1)kumuomba kitambulisho chake cha kazi kwamba anakukagua kama nani kisheria,kwa sababu kama ni kukagua pikipiki wenye mamlaka kisheria ni Polisi au trafiki chini ya sheria ya Trafick Act of Tanzania.(2)Kama alikufikisha kituo cha polisi hakufanya kosa na kwa kuwa wewe mwenyewe uliridhika/ulihakikisha kuwa pikipiki yako haina leseni na kama hao polisi wanamamlaka ya kukulipisha faini basi ingebidi wakwambie wanakutoza faini chini ya sheria gani na wangetakiwa kukupa nakala ya faini ili iwe ni kama kielelezo.(3)Kisheria kila raia anaeishi Tanzania yupo chini ya sheria na anatakiwa kuhakikisha havunji sheria hususani wamiliki wa vyombo vya moto lazima muhakikishe kuwa usajili wa leseni au bima uko sawa kisheria hata baada ya kuisha muda kwani kumbuka ukikiuka utakuwa unafanya kosa la jinai kwa kuwa sheria imeshaelezea na kukataza kosa hilo na adhabu dhidi ya muhusika,pia kutokujua sheria hakuna msamaha kwa kuwa kila raia anawajibu wa kujua sheria mbalimbali za nchi yake.
 
Ndo naelekea kituoni nitawapa feedback
 
Nimewaomba nilipie kosa moja (Tsh30,000) wamekubali, nimelipa na wamechukua particulars zangu, nasubiri risiti hazipo.
 
ishakula kwako hiyo... risiti hakuna unawapaje hela??? wewe kweli boya...
 
Jamaa aliyenishika yupo ana kamata sio mchezo, wako wawili wanatumia toyo, na wako kilaia vilevile, yaani toka nije tayari washaleta pikipiki zaidi ya 15
 
Back
Top Bottom