Nikiwa barabarani nakokota pikipiki nikielekea kwa fundi, gafla akatokea jamaa kavaa kilaia, na kuniomba anikague, nikamruhusu, akabaini bima imeisha na element haikuwepo, nikaahilisha kwenda kwa fundi tukaenda polisi baada ya kuniamrisha hivyo,tulipofika wakaniomba leseni ikawa imekwisha mda wake,nikawaambia mbona nilikuwa nakokota nilikuwa siendeshi? wakajibu, hayo hatujui lipa faine tu, wanadai niripie sh 90,000/ nimeondoka kituon nitarudi kesho ili twende mahakamani,mnanishauri nini?, swali, je inaruhusiwa kukamata pikipiki inayokokotwa kwenda kwa fundi?