Nimekanyaga chungu kilichovunjwa njia panda, sina amani kabisa mpaka sasa

Imeisha hiyo baba...jiandae na majanga kwako, nduguzo au familia yako!!
Ishara mbaya sana... kichwa kikianza kukuuma ujue shughuli imeanza
 
Ahahahahahahahahaha....ni noma sana
 
Nimeamka kwa ndoto kali sana mkuu. Naendesha gari kali sana iko full tenki.

natoka kijijini kwetu narudi mjini.

Hii ndoto imenipa mawazo sana maana sina gari wala pikipiki.

alafu hii tabia ya kuendesha speed 120 sinaga😅😅😅
Hii ni dalili ya kifo.....pole sana
 
Hivyo vyungu sherit la kwanza ni kupeleka ukiwa uchi usiku wa manane! [emoji23]

But jisikie amani hakukulenga wewe
Yakikufika mbona utaenda,kuna jamaa yangu aliambiwa akaoge feri enzi zile hakuna uzio tena mchana kweupe na alioga😀😀.
 
Achana nayo endelea na harakati zako mkuu,usiwe na wasiwasi tayari hapo risasi ishatolewa...Kuna mahali Tanga kila siku wanavunja vyungu njiapanda huku wakimwaga Mchele mwingine mikate,karanga Basi huo Mchele watu huukusanya kwenda kuupika au kutengenezea vitumbua na hizo karanga huchukuliwa kwenda kutengenezea kashata ambazo huuzwa na baadhi yao pale mjini,vyungu navyo huokotwa na kutupwa...ukiweka mawazo hasi kuhusu Hilo utajikuta tumbo linaendesha ndo utaanza kusema wamenipiga mshindo...
 
Kama umekanyaga kweli nisikufiche umkanyaga kitu kibaya kina madhara makubwa sana na muda siyo mrefu utakuwa katika matatzo makubwa ambayo hujawahi kukutana nayo
Kama unahitaji msaada nichek sihitaji hata 100 yako ila nataka kuku mmoja tu chumvi na nazi 1 na mafutaa ya alizet kikombe 1½
 
Hiyo huwa analengwa mtu muhusika...kama ni wewe imekula kwako kama sio wewe mlengwa hakuna madhara....zamani walikuwa wanatupa nazi na sarafu za 50,100,mpaka 200 ila kwa sasa haipo tangu vyuma vikazwe hakuna kutupa hela hata majini yenyewe yanaelewa kama uchumi ni mgumu sana.
 
Unapotembea jifunze kuscan njia unayopita.

Kuna watu kama wewe wanatembea kwa uzoefu macho juu kama wanatarajia mana
 
Hii isikupe taabu na wala using usiogope kabisa mimi nilishawakuta wanaoga usiku njia panda. Nikasema nikirudi nitakuwa nimewapa credit kwa hiyo nikasonga mbele nikawafikia nikipita pembeni huku nawaangalia mmoja anaoga mwingine amesimama
 
Duuuu mkuu wamekusagia kunguniiii, kila Kona unaonekana masokoni hata kama ni tajiri
 
Jitakase kwa Damu ya Yesu Kristo. Hayo yote hayana nguvu mbele ya Yesu Kristo tena unasagasaga kabisha uchafu huo na kuutupa mbali hakuna kitu hapo kama upo na Yesu.
Makafiri bana!!
 
Mwanangu aliokotaga hela njiaa panda tulienda kubomoka konyagi bapa na ijawahi tufanya kitu
 
Usiwe na wasiwasi.Ni kachungu kadogo tu.Je,ungekanyaga mtungi?Si ungefariki kwa sonona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…