Nimekaripiwa kazini leo, kwa uzembe wa kusababishiwa

Miaka 3.
Bado uko premature?
 
Kama wew ndo ulitakiwa kuwa Mtu wa mwisho kuwasilisha kazi na upo juu ya wenzako kwa boss bhasi Boss akufukuze kazi. Uzembe wa wengine usiufumbie macho kama unajua kesho kikiumana kitarudi kwako pia.
 
Hizi dalili tayari hilo eneo limeshanza kukuchosha...
Labda una mpango wa kuacha/kuhama hapo ndo maana moyo wa kupigania kampuni unashuka na unahisi unaonewa...

Kwa maelezo yako ni kweli Kuna uzembe uliufanya maana kama Kuna watu walikukwamisha ulitakiwa uwaripoti mapema kwa kiongozi wako Ili wawajibishwe ila kwa kua ulikaa kimya lazima ulaumiwe wewe ..

Ngoja kwanza ..
Fikiria ndo umeanza kazi mwezi uliopita unadhani ungefungua uzi kuhusu hilo tukio?? Hapana maana ungekua unachapa sana kazi sahivi hamu/morali ya kazi ipo down trust me wewe na hiyo kampuni Kuna "misunderstanding" zinzoendelea thus y unahis "wanakuzingua"....

Ushauri wangu
Tathimini chanzo cha tatizo mfano unashirikiana vipi na hao wafanyakazi wenzio, au kama kuna changamoto hapo job kwako tafuta namna ya kuitatua... Vinginevyo nikutakie Kila la kheri kwenye harakati zako..

By experience
 
Mkuu ishu ya kuwaripoti unaonekana unawachongea wenzio wanaweza timuliwa kazi ukaonekana wewe ndio chanzo
 
Sikiliza siku nyingine,kila kitu kifanye kwa maandishi sio kupiga simu,hivyo kama kuna document ambayo iko kwa mwingine mwandikie email kuomba hiyo document,na pia uwe unamkumbusha,na ukiona hakuna majibu toka kwake na imebaki siku moja,repoti kwa mkuu wako wa kazi,hapo hakuna wa kukuangushia banda bovu
 
asante mkuu japo kumripot mtu unaonekana sniich
 
nimejitetea boss ila ukishakaripiwa ndo tayari maneno sumu boss
Kumbe mnakaripiana maofisni kwenu, poleni sana. Sisi hauruhusiwi kumkaripia mtu, hata kusema wewe ni mzembe ni lugha ya kuudhi.
 
Ndio maana nimekupa pole. Kazini kwetu hakuna stress za kazi hata kidogo. Hawa watu wanathamini sana wafanyakazi na mazingira ya kazi kwa ujumla.
Kwa scaniro kama yangu ofis inareact vip
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…