Nimekataa kulipa Pesa ya Taka na ulinzi kama hawatanipa risiti za EFD. Nimepewa barua ya wito serikali za mitaa

Nimekataa kulipa Pesa ya Taka na ulinzi kama hawatanipa risiti za EFD. Nimepewa barua ya wito serikali za mitaa

Kwema Wakuu

Nimeletewa barua ya serikali za mitaa ikiwa na wito WA kutaka niende ofisi za serikali za mitaa.
Kisa na mkasa NI kugoma kulipa Pesa ya taka na ulinzi àmbayo haizidi elfu Tano. Yàani taka 3,000/= ulinzi 2000/=

Walijaribu kunipa risiti za kawaida nikawakatalia nikawaambia waje na EFD mashine au wanipe control number. Vita ikawa kûbwa.
Wakaniambia oooh! Machine NI Moja sijui eneo NI kûbwa
Nikawaambia hiyohiyo moja waje nayo Siku wakija kuchukua Pesa kwangu.
Ñàona wakaniona mtata wakaishia kunitisha.
Sijui niogope!

Nikawaambia wakamwambie mtendaji kuwa kuna kijana hataki kutoa Pesa ya taka na ulinzi Bila kuwa risiti za EFD au kulipia control number.

Hapa ndîo nimeletewa barua, nafikiri mchana nitaenda.

Nimewaambia sina tatizo na kutoa Pesa za ulinzi na Taka ila ninachohitaji EFD machine wanipe risiti au wanipe control number. Vinginevyo sitatoa

TRA Tanzania
Tunaomba muongozo katika suala hili la Pesa za ulinzi na taka zinazokusanywa huku mitaani. Je ni Halali Watu watoe Pesa za taka na ulinzi pasipo risiti za EFD?

Nataka kuuliza serikali za mitaa na serikali Kuu. NI Kwa nini hawa wanaochukua Pesa za takataka na ulinzi hawatoi risiti za EFD?

Robert Heriel
Sokomokoni
Mbona tumekuletea umeikataa na kusema haisomeki vizuri na imeandikwa kwa kiinglish?
NB;Hivi,DSM mkikatiwa risiti za makaratasi za EFD huoni kwamba mji wote utajaa uchafu wa makaratasi na kufunika anga lote?Tii mamlaka,mpe Kaizari yaliyo ya Kaizari.
 
Dogo acha ujuaji ujuaji. Kuna mambo mengine unapotezea tu kuepukana na sintofaham za hapa na pale.

Kila mtu Tanzania ni mwizi na mpigaji kwenye nafasi yake.

Huo muda wa kuitikia wito ungefanya mambo mengine muhimu.

Potezea tu.
We' ndugu ni mnufaika wa hizo hela nn...!?
 
Nilibishana na wakusanya kodi ya taka na ulinzi shirikishi. Tena walikua mbaba na mmama, had mmama akasema mtoto mbishi wee.

Nilimjibu pesa yangu itatoka kihalali, na huo uhalali uwe halisi.
Sitakii utanii kabisaa, khaaaaah
Ni pale kwenu mpitimbi?
 
Back
Top Bottom