Nimekatandika

Nimekatandika

Yaani huo usumbufu ndo raha ya kubaki na mtoto, hukutakiwa kukatandika hako ni bado kamalaika
Mkuu haka kadogo sijawahi hata kukagombeza...maza Ake kila siku wanacharurana kanakimbilia kwangu...sasa ni kama kameanza kujifunza kudeka ndugu zake sikuwalea hivyo,so leo nimeka surprise na mabao ili kajue mshua nae anaweza kuwa discipline master...Ila kanapendwa Sana tu,suala kasinyimwe mapigo maana yanasaidia kufundisha sometimes,...mabao unayapima kulingana na umri...
 
Kanazingua...
KENYEWE: pipi
MIMI: haya kachukue kwenye friji
KENYEWE: taaki (yaani sitaki) kana 2yrs ka kiume
MIMI : Unataka nini
KENYEWE: ua (maana yake nivue nguo joto)
MIMI: Nimekavua nguo
KENYEWE:tuuni (maana yake niwekee katuni)
MIMI: Nimekawekea Disney Jr
KENYEWE🙁Tena) tuuni
MIMI: Si hizoo
KENYEWE: taaki
MIMI: Sasa unataka nini
KENYEWE : Pipi, huku kanalia
MIMI: kachukue kwenye friji...Nikanyanyuka nikachukulie
MIMI: Haya shika
KENYEWE: taakii
MIMI(Kimoyomoyo) : unazingua...Nimekandandika mabao ka mawili hivi hali hakajavaa nguo...nikakalazimisha kalale...

Heshima kwa wanawake wote na mabeki tatu kwa kazi ngumu ya kulea hawa binadamu wadogo,haki! ni wasumbufu sana...Love has its limitations.

Kama kuna housemaids wanatafuta kazi kwangu ipo nafasi moja...

Nikiwa off Bora kushinda bar mambo ya kuachiwa mtoto Haya sio
aisee!!
 
Back
Top Bottom