"Nimekosa sana, Nimekosa Mimi" - Hii ni dhihaka kwa Kanisa Katoliki na wana-CCM. Ingawa ni udhaifu wa Bunge, tutafika tu

"Nimekosa sana, Nimekosa Mimi" - Hii ni dhihaka kwa Kanisa Katoliki na wana-CCM. Ingawa ni udhaifu wa Bunge, tutafika tu

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Nukuu ya Prof Assad wakati akiwa CAG "Kama Bunge linashindwa kusimamia serikali huo ni udhaifu wa Bunge". CAG Assad aliitwa na Ndugai kibabe Bungeni ajieleze

Swali la Pascal Mayalla: Je, Bunge linatumika kama muhuri au rubber stamp kupitisha mambo ya serikali?

Pascal Mayalla aliitwa Bungeni kibabe na Ndugai ajieleze

Unaweza ukacheka na kukasirika kwa wakati mmoja lakini kinachowafanya waumini wa katoliki kila jumapili kabla ya sala na mahubiri kutubu kwa kutamka maneno haya: Nimekosa Mimi, Nimekosa sana ndio maana nakuomba.

Kwa wasiofahamu hapa JF, Kila jumapili kwa Wakatoliki ni sherehe kubwa sana, Na sio dhihaka hata kidogo

Kila Jumapili wakati wa Misa Wakatoliki wanaadhimisha nguzo kuu ya Ukristo yaani sherehe ya Kufa na Kufufuka kwa kristo, Hivyo wanoamini kama Wakatoliki kuwa kuna ufufuo baada ya haya maisha wanatakiwa kuishi kwa toba au kutubu wakati wote yaani Nimekosa Mimi, Nimekosa sana.

Dhihaka iliyofanyika leo mbele ya waandishi wa habari na yule mheshimiwa haikubaliki hata kidogo,

Unawezaje kutubu ukweli ambao kila mtu anaufahamu ni ukweli wa mambo kuhusu deni la Taifa?

Unawezaje kutubu na kukana kauli sahihi ambayo ulitamka mbele ya umati na maelfu ya watu?

Dhihaka kuu kabisa ni kuomba radhi wananchi kwa mambo ambayo hatujawahi kushiriki bungeni au kushirikishwa kuhusu nchi hii

Sio mara ya kwanza mheshimiwa Spika kufanya dhihaka mbele ya jamii

Aliwahi fanya dhihaka juu ya maslahi ya Tundu Lissu na hakuomba msamaha mpaka Leo hii

Aliwahi fanya dhihaka kwa CAG Prof Assad, hajatubu mpaka leo

Aliwahi fanya dhihaka kwa tangazo kuwa atawashughulikia wanatoa maoni tofauti hajawahi tubu mpaka wakati huu

Wakatoliki wanapoomba toba hata siku moja hawatamki kauli kwa sauti kwa mambo walioyafanya na wala hawatangulizi risala ya kujisafisha kwanza ndio watubu makosa yao

Kitendo cha Ndugai kutanguliza hotuba na risala ndefu ili kukana kauli zake sahihi na kujisafisha haikuwa toba wala kuomba msamaha bali ilikuwa ni dhihaka kwa wana CCM na Mamlaka iliyojichimbia mzizi zaidi

Ni busara Ndugai akaachana na uspika wa Bunge au akajivua uwanachama wa CCM ili kujenga heshima yake uzeeni

Ndugai kutamka nimekosa sana, Nimekosa Mimi. Alikuwa anatubu dhambi na kujuta kwa nani?

Ndugai kwa kutamka Nimekosa sana. Alikuwa anahitaji nani amuombee na kumsamehe, kuna binadamu anaweza toa msamaha na hata akitoa msamaha kwa kibali gani alichopewa wakfu wa kutoa msamaha?

Tuache dhihaka kwenye imani za watu daima tusimamie ukweli tunaouamini
 
Ni sawa tu cha msingi kajishusha kama pilitoni Kaomba msamaha
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
 
Nchi Ina vituko sana hii na kila wakati tunasikia mapya

Kuna watu waliitwa miungu na mwingine kujiita sijui kiranja huko juu

Na sasa ni muendelezo tu kwani tunajua huko nyuma walikuwa na kauli gani
 
Ni sawa tu Cha msingi kajishusha kama pilitoni Kaomba msamaha [emoji3][emoji3][emoji3]
Wajibu wa Ndugai na bunge ni kuisimamia serikali, aliisimamia kwa kusema iache kuchukua mikopo isiyoeleweka, alikuwa sahihi Kama kazi yake ilivyo KUISIMAMIA SERIKALI. Sasa anavyoomba nimekosa, amekosa nini wakati alikuwa anatimiza jukumu lake la kuisimamia serikali? Huyu kwa kifupi sasa hafai kuongoza mhimili wa kuisimamia serikali.
 
Nonsense, hao kina matonya akili zao zipo tumboni tu. Aibu iliyoje
 
Alafu ukimwambia ukweli kwamba ni dhaifu anamaindi...kumaindi huko nako ni udhaifu.
Huyu amekuwa akifanya udhaifu unaofanya bnge lidharaulike na kulifedhehesha...

1. Kupiga watu fimbo kwenye uchaguzi
2. Kukiri kulala sheria mbaya zikapita
3. Kugombana hovyo na viongozi tens
hadharani
4. Kuzuia uwazi na habari zabunge live.
5. Kubadilisha/ kuedit hotuba za
wapinzani
6. Kumdhihaki raid
8. Kunyanyasa sana wapinzani bungeni
na kuwatangazia hawatorudi
9. Kulazimisha wabunge kuitika ndio
kuhusu bajeti
10. Kulazimisha ubunge kwa wasaliti
wasio na chama
Pamoja na meeengi mengine,huyu ni kiongozi asiyefaa kabisa kuongoza taasisi yoyote!!
 
Ndiyo Maana Wagogo Wanadharaulika Kwa Mambo Kama Haya
 
Sidhani kama kanisa katolliki lina complications za kishamba hivyo, usitufananishe na wale wengine.
Kiufupi ndugai kachekesha, nimecheka sana jana
 
Nukuu ya Prof Assad wakati akiwa CAG "Kama Bunge linashindwa kusimamia serikali huo ni udhaifu wa Bunge". CAG Assad aliitwa na Ndugai kibabe Bungeni ajieleze

Swali la Pascal Mayaalla"Je Bunge linatumika kama muhuri au rubber stamp kupitisha mambo ya serikali? "Pascal Mayalla aliitwa Bungeni kibabe na Ndugai ajieleze

Unaweza ukacheka na kukasirika kwa wakati mmoja lakini kinachowafanya waumini wa katoliki kila jumapili kabla ya sala na mahubiri kutubu kwa kutamka maneno haya:Nimekosa Mimi, Nimekosa sana ndio maana nakuomba...........

Kwa wasiofahamu hapa JF, Kila jumapili kwa Wakatoliki ni sherehe kubwa sana, Na sio dhihaka hata kidogo

Kila jumapili wakati wa Misa Wakatoliki wanaadhimisha nguzo kuu ya ukristo yaani sherehe ya Kufa na Kufufuka kwa kristo, Hivyo wanoamini kama Wakatoliki kuwa kuna ufufuo baada ya haya maisha wanatakiwa kuishi kwa toba au kutubu wakati wote yaani Nimekosa Mimi, Nimekosa sana........

Dhihaka iliyofanyika Leo mbele ya waandishi wa habari na yule mheshimiwa haikubaliki hata kidogo,

Unawezaje kutubu ukweli ambao kila mtu anaufahamu ni ukweli wa mambo kuhusu deni la Taifa?

Unawezaje kutubu na kukana kauli sahihi ambayo ulitamka mbele ya umati na maelfu ya watu?

Dhihaka kuu kabisa ni kuomba radhi wananchi kwa mambo ambayo hatujawahi kushiriki bungeni au kushirikishwa kuhusu nchi hii

Sio mara ya kwanza mheshimiwa Spika kufanya dhihaka mbele ya jamii

Aliwahi fanya dhihaka juu ya maslahi ya Tundu Lissu na hakuomba msamaha mpaka Leo hii

Aliwahi fanya dhihaka kwa CAG Prof Assad hajatubu mpaka leo

Aliwahi fanya dhihaka kwa tangazo kuwa atawashughulikia wanatoa maoni tofauti hajawahi tubu mpaka wakati huu

Wakatoliki wanapoomba toba hata siku moja hawatamki kauli kwa sauti kwa mambo walioyafanya na wala hawatangulizi risala ya kujisafisha kwanza ndio watubu makosa yao

Kitendo cha Ndugai kutanguliza hotuba na risala ndefu ili kukana kauli zake sahihi na kujisafisha haikuwa toba wala kuomba msamaha bali ilikuwa ni dhihaka kwa wana ccm na Mamlaka iliyojichimbia mzizi zaidi

Ni busara Ndugai akaachana na uspika wa Bunge au akajivua uwanachama wa ccm ili kujenga heshima yake uzeeni

Ndugai kutamka nimekosa sana, Nimekosa Mimi....... Alikuwa anatubu dhambi na kujuta kwa nani?

Ndugai kwa kutamka Nimekosa sana.... Alikuwa anahitaji nani amuombee na kumsamehe, Kuna binadamu anaweza toa msamaha na hata akitoa msamaha kwa kibali gani alichopewa wakfu wa kutoa msamaha?

Tuache dhihaka kwenye imani za watu daima tusimamie ukweli tunaouamini
 
Sidhani kama kanisa katolliki lina complications za kishamba hivyo, usitufananishe na wale wengine.
Kiufupi ndugai kachekesha, nimecheka sana jana
Hujui historia ya hizi dini wewe, Tafuta jisomee acha kusikiliza mapadei peke yake fanya utafiti

Utagundua yafuatayo:
Nani alitoa ardhi pale Vatikani na kwa maslahi gani utayajua hayo

Waraka wa kusema mapadri wasioe wakati hapo awali mapadri Wakatoliki walioa

Leo hii kuna kitu kinaitwa sinodi ya maaskofu, Yaani ushirika, ushiriki na umisionari unafahamu malengo yake nyuma ya pazia

Hizi dini zilikuja Afrika wakati huo kwa malengo maalum makuu mawili Rasilimali na kubadili uelekeo mpya wa utumwa toka utumwa wa mwili mpaka utumwa wa akili

Kwa sasa kanisa katoliki lina fanya reform na lina malengo hayo tangu Papa Benedikto

Hizo reform unazifahamu, Kuna makundi yanakubali na mengine yanapinga

Hoja kama kutoa mimba

Hoja za mapadri kuoa

Kuna mambo yanafukuta wewe hujui kilatini ndio tatizo

Tatizo lako hujui kilatini, Nyaraka za Vatikani nyingi huandikwa kilatini na Misa mara nyingi huongozwa kwa kilatini
 
Back
Top Bottom