Nimekua Tabora, pazuri ila nimelishwa vumbi, Afrika tusichekane

Nimekua Tabora, pazuri ila nimelishwa vumbi, Afrika tusichekane

Sikonge pako poa kabisa. Gongo na nyama mwitu kwa wingi.

Mashombe wa Kiarabu na Wanyamwezi wenyewe wamependeza kabisa. Karibu tu wewe.

Inabidi nimtishe kidogo ili nione kama kweli kapenda au mpiga bakora na kulala mbele. Heheheee
Nilishafika huko.Jamaa alinipeleka ukumbi mmoja hivi,nili-enjoy sana na live band
 
Huwa unakuja Tabora mara kwa mara mkuu??

Nategemea kuja mara moja baada ya kila kama miezi miwili hivi, nitakuPM nikija, pazuri sana pale.
 
Hongera kwa safari yako ya tabora, ata mimi nilipitia huko wiki kazaa zimepita na nikapiga picha chache
158527_5ac886c35c5171ffc3ea591a0c7b4bba.JPG
 
Huo mkoa unaunganishwa
kwanza barabara inakalibia kukamilika
Mpanda-Sumbawanga
Inayo fuata ni Mpanda-Tabora kupitia Sikonge
pia ni Mpanda -Uvinza
hizi zote zipo kwenye Mpango huo
Ok, ni vema kama MPANGO huo upo.
Ila tukubali kwamba bado "haujaunganishwa" maana barabara za vumbi ndiyo tunamaanisha kusema haujaunganishwa.
Vipi hiyo ya Sumbawanga-Mpanda lami yake imefika maeneo gani?
Naamini hizo nyingine (Mpanda-Tabora na Mpanda-Uvinza) bado ni mipango na hatua za awali.
 
Ile barabara ya tokea nzega mpaka tabora haijawekwa lami tu?
 
Kuna watu wanaishi Nakuru na wanafanya kazi Nairobi, yaani gari ukiichezea kwenye 100km/h halafu bararabara yenyewe imenyooka mbona Nairobi unafika ndani ya muda mchache sana.

Aisei Tanzania ni kubwa, binafsi nimetembelea mikoa yenu mingi, yaani nalala na kuamka na kulala mara kadhaa na hatufiki, madereva wenu wa mabasi wana nguvu sana, halafu huwa naona kuna polisi wana zile radar za kukamata taarifa za kasi, hivyo inabidi dereva asafiri taratibu kwenye chini ya 80km/h.
Hivyo vifaa mpaka vifike Kenya zinahitajika karne si chini ya 7
 
Wewe ni mwongo nahisi hujafika huko umesimuliwa,
Hicho kipande ni km80, halafu sio kuanzia manyoni, ni mbele ya Itigi ndio hicho kipande kimeanzia,
Halafu kama huftaki vumbi ungepita Singida-Nzega-Tabora, ungefurahia mkeka saaafi kabisa.
Uachage majungu.
Nizaidi ya 80
 
Ndio maana nikasema kwenye title yangu kwamba Afrika tusichekane, najua kuna maeneo Kenya yenye barabara ya vumbi hususan kaskazini ambapo kuna watu wachache huko. Japo hiyo yenu niliona kama ni 'National Trunk Road' au type B. Sidhani kama Kenya tuna type A, B na C ambazo bado ni murram, I stand to be corrected.
Nilikua najua ile ya Kitale-Lokichar lakini imeshughulikiwa kwa ajili ya mafuta ya Turkana.

Anyway tutafika tu.
Mk nadhani umepita muda mrefu sana barabara hiyo zimebaki 20km tu kutoka manyoni mpaka tabora mjini
 
Hehehehe!! Mbona mimi mstaarabu siku zote...
Tatizo mkitembelewa na mgeni mnataka ataje mazuri yote bila doa hata moja, nikitaja doa mnatiririka povu.
Nchi za kiafrica zinafanana sana sana hakuna kuchekana thats true coz utaona nchi moja ina miji miwili au mitatu iliyochangamka the rest inakuwa hovyo tu ilimradi wanaitwa watu wa taifa hilo mambo yanaenda
 
Wewe unasifia msosi wa Tabora? kwa heri mwalimu Kenya hutokaa tena kila siku utakuwa unawaza kurudi tabora a.k.a Mboka inaonekana umekutana na shughuli ya demu wa kinyamwezi bado hujalowekewa nguo.
 
Tunauliza hivi mbona leo umekuwa mstaarabu??? Lazima uufyate kwa sababu barabara ya Nairobi-Nakuru ina lami ya zamani na mashimo kibao, niliwahi fika huko nikalala pale Bontana Hotel, Nakuru padogo vipi unalinganishaje Nakuru na Tabora????

Wewe hujui unachosema....
 
Back
Top Bottom