Nimekubali kurudisha muamala wa mpesa kiasi cha shillingi 1.4M uliotumwa kwenye namba yangu kimakosa

No Internet

Member
Joined
Dec 1, 2024
Posts
30
Reaction score
73
Habari wana jamvi

Jana jioni mida ya saa 12 katika mtaa mmoja ninaoishi nilikuwa nimekaa na washikaji zangu tukibishana kuhusu kanuni za mpira baada ya bodi ya ligi kuahirisha mechi ya watani wa jadi simba na yanga

Simu yangu mfukoni ika,vibrate kuashiria kwamba kuna sms imeingia, sikuifungua haraka kutokana na mabishano kuhusu kanuni kunoga, nilitulia kama dakika tatu hivi ndio nikaifungua, nikakuta sms ni ya mpesa ikionyesha nimepokea kiasi cha shilingi million moja na laki nne kutoka kwenye namba ambayo sikuifahamu, nikarudisha simu mfukoni nikaendelea na mabishano na washikaji zangu

Baada ya dakika kama tano hivi nikapigiwa simu kucheki ni namba ngeni ambayo sikuifahamu, nikapokea baada ya salam akajitambulisha kuwa yeye anaitwa Saidi Ramadhan (Hili sio jina lake halisi) akaniambia kuwa amekosea kutuma pesa hivyo anaomba nimrudishie pesa yake kwani alikuwa anatuma ada kwa binti yake chuoni.

Binafsi nilikiri kupokea kiasi hicho cha pesa na mimi sikuona shida yoyote nikamwambia awasiliane na mtoa huduma wa mtandao husuka (huduma kwa wateja) amwambie arudishe muamala huo tukawa tumekubaliana hivyo akakata simu, baada ya kama dakika kumi muamala ukawa umerudi.

Leo asubuhi mda wa saa mbili nikapokea tena muamala wa mpesa kiasi cha shilingi laki mbili kutoka kwa namba ile ile iliyonitumia pesa jana, nikapiga simu kwenye hiyo namba baada ya salam jamaa akaniambia kuwa hiyo pesa laki mbili amenitumia kama shukurani kukubali kurudisha pesa, pia akaniomba tuonane ili tufahamiane nikamwambia hapana maana sioni umuhumu wa kufanya hivyo, hata hivyo haitawezekana maana tupo mbali yeye yupo Dar mimi mkoani.
 
H
Hongera kwa uaminifu
 
Uma roho nyepesi sana. Ķuna watu wana roho ngumu angetoa, anavunja laini anabonda na kitofali halafu anatumbukiza chooni.
Kuna watu wanabadili laini kwa sababu ya 40,000 tu kmmk.

Mimi nisharudisha kama mara nne ila muamala mkubwa ulikuwa 170,000.
Huo muamala aliyekosea aliripoti, ila kutokana na nature ya muamala wenyewe wahudumu waligoma kurudisha mpaka wanipate mimi na bahati mbaya nikawa sipatikani kwenye ile namba.

Walijiongeza wakanitafuta kwenye namba nyingine hapo tayari ni siku ya tatu ndio nikacomfirm irudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…