Nimekubali kurudisha muamala wa mpesa kiasi cha shillingi 1.4M uliotumwa kwenye namba yangu kimakosa

Ishawahi kunitokea, nilitumiwa laki 8 na nusu namba siijui na wala sina makubaliano na mtu kunitumia iyo hela. Nikajua kuna mtu kakosea namba mpaka kufika asubuhi kimya, kwa sababu njia ya kuelekea kazini napitia ofisi za voda nikaingia ofisini kwao nikawaambia nimepokea hela ambayo sijui inatoka kwa nani. Wakafanya mambo yao mhamala ukarudishwa, mchana wake napigiwa simu sikuweza kupokea kwa muda huo ilivyokata nikamwambia alienipigia atume text. Ndio jamaa aliekosea mhamala akatuma text kushukuru
 
Na kwanini mkaamua kuwasumbua huduma kwa wateja ilihali angeweza tu kujirudishia muamala mwenyewee??
 
Mtu akikosea muanala hurudishi wanakushauri umwambie aende kwenye menu aurudishe mwenyewe. Wewe la kufanya hutoi huo muamala unamwacha yeye aurudishe mwenyewe.
Mitandao ya simu inashauri jambo hili kwa sababu ya utapeli unaoendelea wa watu kupokea sms fake wakakuta wanatuma pesa yao wenyewe wakidhani wanarudisha miamala.
Nikupongeze pia maana uaminifu ni bidhaa ya bei rahisi lakini adimu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…