Nimekubali Mpira wa leo ni PESA

Nimekubali Mpira wa leo ni PESA

Mahesabu yako hayako kiuhalisia.. unajua idadi ya watu 50,000,?

Mtu kashindwa kulipia 20k kitambulisho cha biashara atoe ac30k ya jezi?
acha ubishi wa kijinga, hivi kabla ya hamasa ya Simba Day kubuniwa ulitegemea kwamba washabiki wa Simba au Yanga wanafikia 60,000 wa siku moja wakajaza uwanja?
 
wewe unayejua elimu ya biashara endelea kubisha kwamba huwezi kuuza jezi 50,000 kwenye Taifa lenye watu milion 60. Biashara ya vitabuni inawatesa watanzania sana na wewe ni mfano tosha.
We huna ujualo ww umesema kila mkoa jezi 50,000 so ukizidisha na 30 unapata jezi 1,500,000... hapo ukizidisha na TZS 30,000 unapata pesa kubwa mno. WAHINDI WANGEDEAL NA HII ISHU.
 
,,
unataka kuniambia jezi 50,000 haziwezi kuuzika kwa msimu mmoja?

Swali dogo tu, Je unakubali kwamba washabiki na wanachama Simba leo wapo 60,000 pale Taifa? Kama unakubali hivyo sasa hizo jezi 50,000 unashindwaje kuziuza kwa msimu mzima?
Ticket bei yake ni elfu 30 ?, quality ya jezi na mafanikio yanaendana na hio bei ?, replicas zikianza kuja zitakuwa na bei gani ? Kumbuka mara nyingi kuna watu wanapewa contract ya kutengenza na kuuza hizo jezi.., je hao watu mapato yao ni kiasi gani ? na Timu inachukua percent ngapi ?
 
kaka basi nibishie kwamba duniani hakuna mchezaji analipwa $650,000 kwa wiki...ukisema hayupo ntakubali... Mpira ni weka pesa upate pesa.

Watanzania tulikuwa tumelala kwenye sekta ya uchumi kwenye michezo - M0 kaona fursa katuamsha, Yanga watafuata sababu pia wana mtaji mkubwa (Brand) ila hawajui namna ya kuwekeza.
Sawa uko sahihi ila sio bongo labda karne ya mia mbili
 
wewe unayejua elimu ya biashara endelea kubisha kwamba huwezi kuuza jezi 50,000 kwenye Taifa lenye watu milion 60. Biashara ya vitabuni inawatesa watanzania sana na wewe ni mfano tosha.
Mzee unachanganya madesa kasema jezi elfu hamsini kila mkoa sio tz nzima
 
Marekebisho kidogo ya typo nimesema jezi 50,000 Tanzania nzima, lets say tuna mikoa 20 sasa gawanya kwa mikoa utapata kila mkoa jezi takribani 2500
 
Watanzania hamjielewi kaeni hivyo hivvyo, kuwa na timu yenye washabiki na wanachama approx 100,000 Tanzania ni mtaji mkubwa sana. Capital huwa si hela tu bali hata Brand ni capital.
Kudhihirisha kwamba hamjui kitu ni mtu eti anabisha kwamba huwezi kuuza jezi 50,000 katika Taifa lenye watu zaidi ya Mil 50.

Kinachohitajika ni marketing strategies,,,kwisha habari.
Kama zipi?
 
Matunda yote haya yote ni kutokana na uwekezaji mdogo wa Simba msimu uliopita, leo tunaona watani wetu nao wakifaidi matunda.

Sasa leo ntapiga hesabu ndogo tu kukuhakikishia kwamba mpira wa leo ni PESA yaani unaweka PESA unapata PESA.

Tuseme tuna mikoa 20 Tanzania nzima, kila mkoa upangiwe jezi 50,000 tu. Kila jezi ya Simba ni 30,000,
i
Twende kazi:-

20 x 50,000x 30,000 = Billion 30. Hii ni kwa JEZI tu.

Kweli, Weka PESA upate PESA, huna PESA kaa pembeni au tembeza BAKURI.
Hizo ni jezi nyingi sana. Kwa Tanzania target ile jezi 100,000.
Hapo unapata 3bn na profit margin kuwa 30%, hukosi 1bn kwa mwaka.
Mfumo nzuri ungekuwa wa kuwapa vunja bei contract badala ya gsm.
Ungetengeneza jezi China, leta makontena kisha, uza kwa 15,000. Hapo usingekosa kuuza hata 500,000 kwa mwaka.
Hizi za GSM zitatengenezwa fake muda si mrefu.
 
naongelea kwa msimu mzima, Hizi timu Yanga na Simba zingekuwa na marketing strategies nzuri tangu miaka hiyo zisingekuwa zinaomba omba - kama MO asingewekeza na kuweka hamasa unafikiri Simba ingefikia hapa? Uwekezaji wa MO ndiyo umefanya na Yanga wanaibuka sasa.

Kama hujui Mpira una nguvu kubwa sana kuliko hata haya makanisa... Mpira ni zaidi ya imani...
Nimekuelewa sana Kiongozi. Hata mimi napenda iwe hivyo lakini ukweli ubaki kuwa ukweli.
Potential buyers wa hizo jezi ni middle class. Huwa ni consumers wazuri popote pale. Tunao wakutosha? Soko liko hapo.
Kupenda mpira ni kitu kimoja. Kuwa na uwezo wa kununua jezi ni kitu kingine.

Inabidi ifanyike market survey ya uhakika. Kwa mfano kuna hili ya uanchama kwa kwa njia ya mtandao kwa kutumia App. Wangapi wana simu janja ili watumie hizo App zenyewe?
 
wewe unayejua elimu ya biashara endelea kubisha kwamba huwezi kuuza jezi 50,000 kwenye Taifa lenye watu milion 60. Biashara ya vitabuni inawatesa watanzania sana na wewe ni mfano tosha.
Hukusema kwenye taifa zima hiyo 50000 kwa msimu,ulichosema nikatika kila mkoa na ndiomana ukazidisha 20x50000x3000.Angalia bandiko lako
 
,,
unataka kuniambia jezi 50,000 haziwezi kuuzika kwa msimu mmoja?

Swali dogo tu, Je unakubali kwamba washabiki na wanachama Simba leo wapo 60,000 pale Taifa? Kama unakubali hivyo sasa hizo jezi 50,000 unashindwaje kuziuza kwa msimu mzima?
Sawa mkuu but hapo uwanjani wote wana jezi ya team? Unadhani wote wana uwezo wa kununua jezi mkuu au wote wanapenda kuvaa jezi ata kama ndio ni mpenzi/ shabiki wa team? Au unawaza kama watawala wetu kwamba ata korosho ikikosa wanunuzi soko la nje, basi soko la ndani la tosha kwa kila mtanzania kununua na kula kilo moja ya koro shoo!! Hahaaaaa
 
Tanzania ni nchi masikini sana bro angalia majority ya watu wanaishi VP usijiangalie wewe!30,000 ni nyingi sana kwa watu wengi hats jezi 10,000 kwa mkoa hazifiki!!
 
acha ubishi wa kijinga, hivi kabla ya hamasa ya Simba Day kubuniwa ulitegemea kwamba washabiki wa Simba au Yanga wanafikia 60,000 wa siku moja wakajaza uwanja?
Tatizo lako mkuu una generalize, sio wote unawaona hapo wamejaza uwanja ndo mashabiki wa simba kisa ni simba day. NO. Ingekuwa ni rahisi hivyo unavyowaza basi leo ambayo ndo kama sherehe ya simba ungeona uzi mwekundu tupu nadhani
 
Mtoa mada hakujua alichopost... maana alisema 50,000 kila mkoa hapo ndipo watu wanapokataa yaani mauzo ya jezi 1,500,000 kwa SIMBA PEKEE na wale YANGA nao wakiuza zao ziwe jumla 3M ya jezi...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mie namuunga mkono mtoa post.
Lazima uanze na mahesabu kabla ya kuanza business.
 
Back
Top Bottom