NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
1 + 1 = 2, watanzania wengi tume focuss kwenye 2 kwamba Idd Amin alivamia Kagera na ndio chanzo, tunasahau kwamba Kuna 1 + 1 zilizosababisha ikawa hio 2 na hata ukienda Wikipedia nao hawajui chanzo kamili cha 1+1 kilichoanzisha vita ila ni wazi kabisa mtu aliefaidika kwa kupinduliwa Idd Amin alikuwa ni Israel,
Idd Amin alikuwa anaichukia sana na kufanya vitendo vya kuwashambulia indirectly na alifikia nia ya kuwashambulia directly, hii ulikuwa ni mwiba kwa Israel na wakamuona ni tatizo la kulitatua haraka kabla halijakuwa kubwa.
Mwaka 1976 Idd Amin aliwapa hifadhi magaidi pale uwanja wa ndege wa Entebbe, Magaidi waliteka abiria wa Israel na maombi yao yalikuwa ni Israel waachie huru wafungwa wa Palestine wenye kesi za ugaidi, Israel hawakukubabali haya maombi wakaenda kuuvamia huo uwanja bila ushirikiano wa Uganda, waliweza kuokoa abiria wa Israel japo kulikuwa na vifo vichache kwa makomandoo kama Kaka yake Benjamin Netanyahu, Operation haikuwa ya kitoto Ile, jeshi la Uganda ilibidi lianze kuwashambulia Israel lakini walitulizwa na vifaru vilivyotua na jeshi la Israel. Idd Amin alikuwa na hasira sana na Israel, hapa Israel walishaona wazi kabisa huyu mtu ni hatari Kwa usalama wa raia wa Israel na inabidi ashughulikiwe.
Vita ya Uganda na Tanzania ni ngumu sana kuujua ukweli wake lakini uki connect dots unaona Kuna uwezekano mkubwa Israel ndie alikuwa nyuma ya pazia kutamani Idd Amin atolewe madarani Kwa namna yoyote, Kuondoka Kwa Idd Amin ilikuwa Ahueni kwao