Wenzako walivyokuwa wanashushwa na magari ya njano ulikuwa unawaonea gere eeh, ushakuwa umeyaona sasa.
Mfano mdogo, Wengine toka udogoni tulitambua hali ya kweti, sikuwahi kumuona mama yangu kanifanyia dogo, mie vitu vingi saana nilikuwa naona ananifanyia kwa kujiumiza,
Nilikataa kununuliwa nguo za sikukuu nikiwa darasa la 4, nyumbani kuna watoto kibao, mara sijui wa mjomba, mara wa mama mkubwa, mara sijui wa nani, na wote anawajali kama wanae, hakuwa na ubaguzi, sikukuu moja nikamsikia anaongea na mama wa jirani sikukuu inakuja na hajui pakushika, jioni yale nikamwambia kuanzia leo, kuanzia sikukuu hii sitaki kabisa nguo za sikukuu, nikaulizwa kwaninj.
1. Sikukuu nguo zinauzwa kwa bei juu sana tofauti na uhalisia, hiyo pesa ikitumika siku za kawaida huwa napata nguo 3 mpaka 5 za kawaida na ni nzuri tu.
2. Siinjoi, kuvaa miguo ile na kuzurura kwangu ni kero, napenda kwemda beach niogelee tu.
Nikamshawishi akanielewa, kumbe lengo langu ni kumpunguzia gharama, ni bora nikose mimi lakini watoto wa ndugu zake wapate, mie mzaliwa siwezi kuwa na kinyongo.
Bimkubwa katulia kisteringi saaana, ukizingatia dingi alikata moto mapema.
Alikuwa na ajira yake ambayo kama si kuwa ndugu wengi huenda tungeinjoi kiadi kikubwa maisha, ila familia ilikuwa kubwa na katulea kwa upendo kiasi familia ikiwa kubwa watoto wa nyumba ile tunafurahi zaidi, ilikuwa ukija kwetu usiku jungu la wali linalopikwa hapo unaweza kusema kuna shughuli ndogo, nyumba yetu watu wachaache kabisa unakuta 15, nyumba ya vyumba vi4 lakini inafika pointi kuna watu wanalala sebuleni.
Mama yangu ni mtu special kuliko maelezo, ♥️♥️♥️