Na ukilijua hili mapema, mtoto utaishi kwa amani saana. Ukipewa 50 ya shule hewala, ukikosa sawa, ukipewa 200 sherehe, siku ukipewa 30 burudani pia.
Nakumbuka bimkubwa mara nyingi asubuhi alikuwa akipenda tuongozane, tukifika kigamboni pale kabla ya kuoanda pantoni ananinulia biscuit flani hivi zilikuwa zinaitwa mabrooq kama sikosei, akinipa na shilingi 100 yangu au 200 ya noti aah, enzi hizo nauli ni 20 ama 30 kwa mwanafunzi kama sikosei.napanda mabasi mawili kwenda shule na mawili kurudi, so nikija nae mpaka feri maana yake daladala la kwanza anakuwa kanilipia, hapo Naenda shule naamani kabisa.
Mapumziko nikijibless mihogo na ka SUNVITA kangu, siku hiyo ni muruwa kabisa.
Siku 1😂 nipo feri, tayari gari la kwanza nishalipiwa, kaninunulia biscuit na kanipa 200 yangu, nakutana na watoto wamenitolea buku, wananiomba chenji nikawajibu sina, nina 200 tu, wakaniuliza unaenda shule na 200, nikajibu ndio, aah, walicheka saana, moyoni nikajisemea hawa maKUMER nini, sasa kinachowachekesha nini, wakati mie mwenyewe hapa naenjoy.. Nikipewa buku si ninaweza gongwa na gari kwa kuwehuka. 😂🤣