Mfumo wa chakula wa binadamu aka digestion system hufanya kazi yake sahihi na utaona matokeo kama unapata haja kubwa na haja ndogo kwa wakati sahihi yaani isiwe kila masaa au inapita siku nzima hujajamba kabisa au siku nzima kwa maana ya masaa 24 hujakojoa wala kupata haja kubwa.
Vivyo hivyo kuna vyakula hufanya mfumo wa kumeng'enya chakula utoe gesi kwa wingi aka kujamba na vyakula vingine hufanya mtu akose haja kubwa kwa siku kadhaa na vyakula vingine hufanya mtu aende haja mara kwa mara aka kuhara.
Mfano, ukila vyakula vinavyochacha haraka kama maziwa, mtindi na samaki kwa asilimia kubwa ni rahisi kuhara au tumbo kuchafukwa.
Mfano pia ukila mikate kwa wingi hasa ile ya kiarabu isiyitiwa mafuta ama mapera sahau kwenda choo kwa siku kadhaa.
Mfano wa vyakula ambayo ukila tumbo hujaa gesi na kujikuta unajamba mara kwa mara ni maharage, mayai ya kuchemsha, mahindi ya kuchemsha, kabichi, viazi vitamu, viazi ulaya, mboga mboga zilizopikwa na mboga za majani.
Mtoa mada, kuna msemo wa kiswahili husema, dalili ya mvua ni mawingu.....
Pia, dalili ya kupata haja kubwa ni mashuzi......
Yaweza kuwa viazi vitamu na maziwa uliyokunywa vimejaza gesi tumboni na baada ya hapo gesi haina namna zaidi ya kukutoka kwa kujamba, ni hali ya kawaida sana tena ni afya....
Usipojamba unaweza kulazwa maana tumbo litakuunguruma na utaumia maana gesi itavimbiana huko tumboni ikitafuta pa kutokea.
Pia jiandae kupata haja kubwa maana dalili ya kushusha magogo na kutoa gesi...
Hata watu wakisema hapa ndivyo isivyo, ila tambua si jambo la ajabu kutoa gesi japo kutoa gesi mbele za watu ni fedheha... walau utoe gesi isiyoambatana na sauti.... ikiambatana na sauti na uko mbele za watu ni fedheha zaidi.
Ila ni vyema ukishikwa na ushuzi kuuachia utoke kiafya kuliko kuubana ili usifedheheke..
Ukitaka kujua kujamba mbele za watu ni fedheha, ngoja ushikwe na ushuzi mbele ya wakwe na hujui ukiuachia utatoa sauti ama utatoka kimya ila harufu itakuwa kali kuliko panya aliyekufa.....
Afya njema mtoa mada.