Nimekumbuka zamani!!

Nimekumbuka zamani!!

si siku moja tumecharazwa sana na baba, marehemu rashid kawawa alitembelea nyumbani na sie tukawa tunabembea nje kwenye miti huku tukiimba maneno kawawawawawaaa kama vile tunaendesha magari. lo, bakora zilizofuatia hapo! ilikuwa balaa
 
Tuliosoma shule za kata tuna mengi ya kukumbuka.
Nakumbuka kuna mwanafunzi eti alimkuta mbuzi anasoma gazeti chooni.
Nakumbuka tulipokuwa tunalazimishwa kununua mifagio ya chelewa kama adhabu kwa kuchelewa kuwahi namba.
Nakumbuka nilipokuwa monitress nilikuwa na kibarua kizito cha kuandika majina ya wapiga kelele. Nisipoandika nachapwa mimi, nikiwaandika wakati wa kutoka wananivizia wanipige.
Sitosahau tulipompiga mwalimu na yai viza maana alikuwa mnoko sana.
Yote kwa yote nakumbuka nilikuwa nakaa nyumba ya pili kutoka shule hivyo nilikuwa sipewi hata sh kumi ya kwenda nayo shule.
Jamani mambo ya shule ya msingi....mmmh

Hahahhahahah!!!Alafu kabla hujaanza kuandika unawaambia marafiki zako kabisa...nyamazeni naanza kuandika wasumbufu!!Maana wakisumbua alafu usipowaandika wale wanaoandikwa lazima waseme....mwl. hata fulani na fulani walikua wanaongea ila hawajaandikwa!!!
Alafu ukiwa kiranja wa darasa lako mwenyewe unashindwa kuwapangia kazi kwasababu wengi wanakua ni marafiki...mi nlikua navizia wale watoto wengine wanaochelewa sana nawaambia wafagie au nimwambie mwl. walivyochelewa!Lolzzz

Siku ya kufunga shule ndo ilikuaga wavulana wanajificha vichakani....wengine juu ya mti kumvizia ticha mnoko!!!

Mvua ikinyesha kuna watu walikua wanaacha wanyeshewe makusudi ili wasikae darasani....mwl. akimuona mtu maji yanamtiririka anamwambia aende jikoni akakaushe nguo zake!!!
 
si siku moja tumecharazwa sana na baba, marehemu rashid kawawa alitembelea nyumbani na sie tukawa tunabembea nje kwenye miti huku tukiimba maneno kawawawawawaaa kama vile tunaendesha magari. lo, bakora zilizofuatia hapo! ilikuwa balaa

Hahaahah....mnasumbua wakubwa wakiongea sio?Sisi ilikua wageni wakiongea ndo tunapata mwanya wa kwenda kucheza kwa jirani kwa kisingizio kwamba hatukutaka kusumbua!!Siku hizi wakubwa wakiongea watoto nao wanakaa hapo hapo kuwakodolea macho!
 
hahaha...very funny, ulikuwa hauendi shulen na mahindi yaliyokaangwa, yakachemshwa then ukayaweka sukari? halaf marafiki wanakuwa wengi maana umekuja na mahindi.maembe je?
Ehhhh sana tu.....bila kusahau ya kuchoma!!Maembe...machungwa....zambarau....alafu kuna mengine tulikua tunayaita elimu sijui kwa kiswahili kinachoeleweka yanaitwaje!!!
 
wewe bado hujaamka tuu:horn:

Nakumbuka tulikuwa tunasoma na Vince kwao walifuga sungura waliokuwa na uwezo wa kucheza karata,basi Vince alikuwa na marafiki wengi kwa kuwa kwao kulikuwa kama zoo ya kwenda kucheki wanyama japo walikuwepo sungura tu........

Nakumbuka siku moja Vince alinidanganya tukaenda nyuma ya nyumba akaniambia vua sketi yako,ile naanza vua,mama yake akatokea,Vince akakimbia,mama yake akanipeleke home,nlipofika tu mama yangu akanivua chupi.....sijui ili aone nini????
Vince alipigwa sana lakini bado akawa anaendelea na tabia yake,na vile kwao walikuwa wana sungura wacheza karata na nilipenda kuwaona nilikuwa nakubali tu kuvua........lol
 
mlikumbuka kutumia protection?
 
Hahaaa umenimbusha mbali sana, nakumbuka darasa la tano nilikua na bana siendi shule naenda kuogele na rafiki zangu, tunaenda kuteleza kwenye mawe mpaka sketi inaisha mtakoni, rafiki zangu wa shule wakaenda kushtaki nakacha vipindi, nlivofika home nikala, maza akaniuliza mwalim flani hajambo nikajibu ndio anakusalimia, kuombwa madaftari sijaandika kama wiki hivi, nikafungwa kamba miguu na mikono kwenye makochi kibano mbaya. Nakumbuka mi narafkiangu tulienda kuogelea tukakimbizwa na likaka ka kisukuma likubwa ila halikutupata. Nakumbuka nilikua napenda kuogelea sichagui hata kwenye ma bwawa mpata nikapata kichocho.
 
Mie yooooooooote UCHOKOZI ndo imenigusa bila kupigana siku haiishi nakwambia halafu sijawahi kupigwa hata siku moja. Nilikuwa mgomvi mie aaahhh mpaka aibu kwa sasa nikikutana na wale tuliosoma nao. Walinitungia jina NINJA ilikuwa ni balaa ila siku hizi nimekuwa wajameni. Ila sio siri utoto raha nyie acheni tu
 
Baada ya likizo ndefu ya mwisho wa mwaka tukafungua shule, basi zile siku za mwanzo tu nikachaguliwa kuwa monitor. Siku moja ktk wiki ya pili akaingia mwalimu mmoja alìyekuwa mnoko hasa darasani kwetu akakuta kelele za kufa mtu, akaita ma-monitor mbele, kuulizwa hatuna majina ya wapiga kelele! Viboko tulivyopata siku hiyohiyo nikajiuzulu umonitor! kwa hiyo nilikuwa monitor kwa kama wiki moja hivi!!
Shule mojawapo ya primary niliyosoma kulikuwa na imani ya ajabu kuhusu mmea fulani hivi, kwamba ukifukia kijiti chake mlangoni lazima watu wapigane! Basi mara nyingi walikuwa wanafukia kwa siri kwenye ofisi za waalimu au darasa la 6 au la 7. varangati lake si mchezo. Sasa hivi natamani mtu akaweke kijiti kile mahali baraza la mawaziri la bongo linapofanyia vikao!!!
 
Heheheh! Jamani mm nilisoma shule moja Monduli huko na wakaka wamasai wanatokomea term nzima, nilikuwa nawaandikia barua zao nyingi za mapenzi coz hawajui kusoma na kuandika! Nakumbuka I was full of mischief nawaandikia uongo ninaotaka mimi na kuwasomea tofauti pia ! Kuna kijana mmoja darasani alikuwa anatoka na mke wa polisi nakumbuka nilikuwa namwandikia uongo jamani kuliko kijana anachoniambia,halafu na mke wa polisi hajui kusoma shurti nimsomee..loh si bure shule ile nilifaulu peke yangu kwenda form 1
Mhandisi
 
Hahaahah....mnasumbua wakubwa wakiongea sio?Sisi ilikua wageni wakiongea ndo tunapata mwanya wa kwenda kucheza kwa jirani kwa kisingizio kwamba hatukutaka kusumbua!!Siku hizi wakubwa wakiongea watoto nao wanakaa hapo hapo kuwakodolea macho!

Sisi kuwe na wageni, halafu ujikalishe sebuleni, kuna jicho mumy atakukata utainuka mwenyewe, nakupotea.
 
Jamani rede ya mchanga na kumbolela lol,
 
Back
Top Bottom