Nimekumbuka zamani!!

Nimekumbuka zamani!!

kulikua na wizi wa wino wa bic...

HAHAHAHHAHAAHHHHHH!!!!Mtu anaiba wino alafu baadae unavujia kwenye mfuko!!!Au wengine tulikua tunaweka alama kalamu zetu....mtu akiiba anatupa bomba anachukua mrija tu!!!Yani umenifurahisha kweli!!!
 
Nakumbuka kila jumatano nilikuwa siendi shule sababu ya table (orodha) mwl wa hesabu alikuwa hatari hasa table ya 7 na ya 9. Darasa la tano nilikuwa namuuzia mwl vibagia basi navila halafu nasingizia watoro wamekopa, mwl alivyojua nikaacha kwenda shule , bibi akanidunda then akalipa deni. Kuna nyimbo za kuruka kamba kama anayeingia tumfanye wakwanza manu amanuliwe kamba ikikukwama unavutwa juu juu, hadi unachaniwa chupi. Those days bana achaa.

Dah ulikua mtundu wewe....basi wakati wa kukopa mtu atakavyooomba akopeshwe!!!
 
HAHAHAHHAHAAHHHHHH!!!!Mtu anaiba wino alafu baadae unavujia kwenye mfuko!!!Au wengine tulikua tunaweka alama kalamu zetu....mtu akiiba anatupa bomba anachukua mrija tu!!!Yani umenifurahisha kweli!!!
Dah wizi wa wino tena.
 
oooohhhh my dear lizzy
umenikumbusha mbali sana
mie ninacho kumbuka zaidi ni

  1. ufuta
  2. gubiti
  3. kashata
  4. sambusa na vitumbua
  5. mihogo na viazi vitamu ( hapo na chachandu au siki mmhhh)
nway hivyo viazi vitamu ndo sintakaa nivisahau..
ilikuwa mapumziko ya saa nne..
najitafunia zangu viazi vitamu wacha kengele ya kurudi madarasani igongwe
nikawa nakimbia na viazi mdomono wacha ninyogwe mmhh
nilitaka kunywa maji yaliyo simama barabarani
uzuri nilikohoa sana vikatoka vyote vingine na pua
halafu nikachelewa darasani fimbo tatu
nani ambiwa nikapige magoti nje ya darasa niite mvua
mpaka hicho kipindi kiishe ..
nilikosa hamu ya maisha
hahah lol
 
unaweka kioo chini ya dawati la msichana and then una-look naniiiii!
 
Dah wizi wa wino tena.

hahah mie nili nunua ice cream
asubuhi asubuhi..
nikashindwa kuimaliza kabla ya kusimama mstarini..
nika iweka mfukoni..
ikaanza kuyeyuka..
mmmhh kilicho fuatia we acha tu ndugu yangu...
 
Lizzy
Nakumbuka kuna rafiki yangu baba yake alijinyonga!Nampitia asubuhi tuongozane nakuta kwao kumejaa watu.....kumbe baba wa watu kajinyonga...tena kisa mapenzi!!

AD
hapo umenikumbusha rafiki yangu mmoja baba yake alifanya hivyo hivyo na kwa ajili hiyo hiyo
huyo kija jina lake linaanziwa na A na baba yake ni B
A alikuwa mtumikizi kanisani na mimi
na baba yake alikuwa mpiga kinanda mzuri sana kanisani...
kweli umenikumbusha mengi sana my dear ..
 
Nimeipenda hii thread.
nakumbuka zamani..nakumbuka kwa mara ya kwanza kuanza kuona sinema kwenye video ilikuwa ile Threaller ya Michael Jackson,maeneo ya keko polisi ufundi kulikuwa kuwa Bar inaitwa majimaji..
Nakumbuka enzi hizo sinema za kihindi zikiwa juu kina Mithun Chakalaboth..
Nakumbuka tulikuwa tunaruka ukuta kwenda kutazama mpira uwanja wa Taifa (ule wa zamani)
Nakumbuka primary tukiwa tunakimbia mchaka mchaka na somo la sayansi kimu...
Nakumbuka tobo baya..mnacheza na mpira ukiupitisha katikati ya miguu ya mwenzenu mnaanza kumpiga
Nakumbuka kipindi cha mama na Mwana na kuomba kuwa mwanachama na watangazaji kina Deborah mwenda..
Nakumbuka wakati tunaanza kwenda kuangalia sinema kwenye theatres "Empress,Avalon,Odeon,Empire,New Chox" na kule Drive Inn msasani..
Nakumbuka siku ya sikukuu especially "Idd El fitri" tunakwenda kutembea ilikuwa maeneo ya feli wakati huo kunafikika na hapa karibu na kituo cha posta ya zamani pale chini palipowekewa fensi enzi tunajaaa na koni,mihogo basi wacha tuu..
 
oooohhhh my dear lizzy
umenikumbusha mbali sana
mie ninacho kumbuka zaidi ni

  1. ufuta
  2. gubiti
  3. kashata
  4. sambusa na vitumbua
  5. mihogo na viazi vitamu ( hapo na chachandu au siki mmhhh)
nway hivyo viazi vitamu ndo sintakaa nivisahau..
ilikuwa mapumziko ya saa nne..
najitafunia zangu viazi vitamu wacha kengele ya kurudi madarasani igongwe
nikawa nakimbia na viazi mdomono wacha ninyogwe mmhh
nilitaka kunywa maji yaliyo simama barabarani
uzuri nilikohoa sana vikatoka vyote vingine na pua
halafu nikachelewa darasani fimbo tatu
nani ambiwa nikapige magoti nje ya darasa niite mvua
mpaka hicho kipindi kiishe ..
nilikosa hamu ya maisha
hahah lol

Hehhehe....AD maakuli mbele ehh!!!

Uwiiiii jamani eti kuita mvua....nimecheka mpaka basi wee!!!Sisi ilikua unapiga magoti mbele ya darasa.....yani full aibu wenzio wanasoma we unaita mvua!!Alafu wenzako walichoandika kesho ukikutwa hukuandika unalo!!!Dah kweli tulikua na kazi!!!
 
Lizzy
Nakumbuka kuna rafiki yangu baba yake alijinyonga!Nampitia asubuhi tuongozane nakuta kwao kumejaa watu.....kumbe baba wa watu kajinyonga...tena kisa mapenzi!!

AD
hapo umenikumbusha rafiki yangu mmoja baba yake alifanya hivyo hivyo na kwa ajili hiyo hiyo
huyo kija jina lake linaanziwa na A na baba yake ni B
A alikuwa mtumikizi kanisani na mimi
na baba yake alikuwa mpiga kinanda mzuri sana kanisani...
kweli umenikumbusha mengi sana my dear ..

Dah...Mungu awapumzishe....wangu jina lake lilikua linaanza na H...baba yake R!!

OffTopic.....kuna sehemu kuleeee kwenye utani nimeona zile herufi C na S nna ndugu zangu wawili mnashea hiyo kitu!!!
 
Hehhehe....AD maakuli mbele ehh!!!

Uwiiiii jamani eti kuita mvua....nimecheka mpaka basi wee!!!Sisi ilikua unapiga magoti mbele ya darasa.....yani full aibu wenzio wanasoma we unaita mvua!!Alafu wenzako walichoandika kesho ukikutwa hukuandika unalo!!!Dah kweli tulikua na kazi!!!

hahahahah lol
ndo maana nilikuwa na penda sana mapumziko ya saa nne dear ..

duuhh halafu hapo unaita mvua magoti yamesha anza choka ile mbaya
unajaribu kuvua malapa uweke magotini lakini hauruhusiwi..
cheki mikoni ilivyo choka sasa hahahah lol
 
oooohhhh my dear lizzy
umenikumbusha mbali sana
mie ninacho kumbuka zaidi ni

  1. ufuta
  2. gubiti
  3. kashata
  4. sambusa na vitumbua
  5. mihogo na viazi vitamu ( hapo na chachandu au siki mmhhh)
nway hivyo viazi vitamu ndo sintakaa nivisahau..
ilikuwa mapumziko ya saa nne..
najitafunia zangu viazi vitamu wacha kengele ya kurudi madarasani igongwe
nikawa nakimbia na viazi mdomono wacha ninyogwe mmhh
nilitaka kunywa maji yaliyo simama barabarani
uzuri nilikohoa sana vikatoka vyote vingine na pua
halafu nikachelewa darasani fimbo tatu
nani ambiwa nikapige magoti nje ya darasa niite mvua
mpaka hicho kipindi kiishe ..
nilikosa hamu ya maisha
hahah lol

Hahaaa gubiti, ufuta na malosti, nyie mnanichekesha, je ma bumunda na pipi za kijiti za sukari ilounguzwa, ooh my gundness mmenikumbusha mbali kishenzi.
 
Dah...Mungu awapumzishe....wangu jina lake lilikua linaanza na H...baba yake R!!

OffTopic.....kuna sehemu kuleeee kwenye utani nimeona zile herufi C na S nna ndugu zangu wawili mnashea hiyo kitu!!!

yeah tuyaache mbali hayo kwani leo ni siku ya raha sana
na hii topiki yako hahah lol

nway ngoja nikachungulie huko kwenye utani my dear
haha lol
 
Hahaaa gubiti, ufuta na malosti, nyie mnanichekesha, je ma bumunda na pipi za kijiti za sukari ilounguzwa, ooh my gundness mmenikumbusha mbali kishenzi.

duuu mabumunda
mama yangu thats the best thing ever..
nilipewa jina la "kulakula "
maana masaa yote nilikuwa natafuna tu..

mabumunda makubwa bei rahisi kama si kosei ilikuwa shilingi hamsini...lol
 
Kuna mwalimu wetu wakiume alikuaga mkali huyo, akitaka kukuchapa anakuuliza, unataka sita kali au nne moto, eti mtu anachagua sita kali hahaaa.
 
Back
Top Bottom