Nimekunywa dawa za minyoo aina ya Albendazole. Naweza kunywa vibia viwili au vitatu baadae jioni?

Binafsi kwa elimu yangu ndogo nakushauri ukapime vidonda vya tumbo kwanza kwasababu pombe ni moja ya sababu kubwa ya vidonda hivyo na wanywaji wengi huwa hawapendi kula chakula /hula kidogo sana na wakikosa hamu ya chakula huanza kuhisi wanaminyoo tumboni na huanza kutumia dawa kama albendazole , mebendazole ni ushauri tu kabla tatizo halijawa tatizo gumu na lisilotibika
 
Shukran mkuu kwa majibu yenye weledi
 
Wanywa pombe hua ni kama mmetekwa
 
Usinywe bia tafuta spirit moja amazing upige ile chupa kubwa "Captain Morgan" itafaa sana na ukimaliza malizia na kitu chepesi aina ya "Vodka" kale kachupa kadogo
Utakuja kutushukuru hapa kesho asubuhi na mapema
 
Ukifa tukuzike wapi
 
So ukikutana nao tu kupiga vyombo lazima, Daah...huwezi ukakutana nao na wakakununulia ila ukaacha?

Msimamo ni muhimu kwenye afya na Maisha yako
 
Usitumie pombe, utaipa shida figo na ini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…