Nimekuta alama za masanduku la wajerumani chini ya ardhi shambani kwangu

Mtu wa leo

Member
Joined
Apr 21, 2023
Posts
75
Reaction score
97
Wakuu za Usiku huu
Leo katika Harakati za Kilimo wakati Jembe la Trekta linapita kuna sehemu likakutana na Jiwe gumu sanaa na kuna alama ya zege la kutisha baada ya Kuuliza wazee wakaniambia Hapa pana Sanduku la Mjerumani na kwa maelezo yao Masanduku hayo yanakuwa na vitu vya thamani so kama kuna wataalam humu nicheck pm nikupe location mje mfanye utafiti
Manyara-Hanang
 
Achana na huo ujinga, utakuja kufukuwa mabomu, nani mjinga afukie mali hivi mnadhani Wajerumani walikuwa maboya kama nyinyi?

Yani wakuibie mjusi wa Dianasor wapeleke kwao halafu ndio wakuachie mali chini ya ardhi?
 
Yalishachukuliwa kilichobaki ni hayo mazege
 
Tunaomba picha
 
Kwa niaba ya wizara ya ardhi, wizara ya kilimo, TRA, wizara ya biashara na viwanda NAOMBA UNITUMIE LOCATION halafu nitakupa ushauri wa nini cha kufanya 🤔
 
Masanduku ya Mjerumani ni biashara kichaa ya mji wa Morogoro iliyowaliza wengi.
Ahahahahh 🤣 🤣 🤣
 
Mimi nimeipata Red mercury
 

Attachments

  • 20250117_073640.jpg
    326.2 KB · Views: 4
  • Screenshot_20250117-072954.png
    71 KB · Views: 5
Mmetuma magerifrendi kutupata wameshindwa, sasa mnatuwekea mtego wa mali.

Kaa nazo mwenyewe, umeona wapi mtu kaokota gunia la pesa kisha akautangazia umma?
 

January hii watu wakiona jiwe la njano tu wanajua ni dhahabu
 
Mkuu,Manyara ni jina la Mkoa na Hanang ni jina la Wilaya na Mlima; hivyo tujulishe ni Kijiji gani?
 
Acha kuwavutia watu utapeli wa kipuuzi, fanya kazi... Tapeli wewe.... Hakuna asiyejua aina hiyo ya utapeli... na kama nakuonea ni kweli basi picha piga kama maelezo yako yalivyo weka humu, ikithibitika nipigwe ban na ukishindwa mods wakufungie maisha kuepusha utapeli wa mara kwa mara humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…