Nimekuta namba yangu ya Tigo niliyotumia miezi mitatu iliyopita imebadilishwa usajili, whatsapp yangu imebadilishwa ?

Nimekuta namba yangu ya Tigo niliyotumia miezi mitatu iliyopita imebadilishwa usajili, whatsapp yangu imebadilishwa ?

Usipotumia line yako miezi 3, hasa usipokuwa hewani na kuweka vocha mara kwa mara inaondolewa hewani. Nimeona line zangu za mitandao mitatu tofauti zimekufa.
 
Mfano akaunti yangu ina kiasi cha shilingi 2000, bado wataifungia!? Kama wataifungia, nini itakuwa hatima ya fedha yangu!?
Hata kama ina milioni wataifunga ili kuepusha mpewaji mpya kuikuta laini mpya ikiwa na hela.
Kuhusu hatma ya fedha yako utaipata kama ukifatilia kwa wakati kwa sababu taarifa zako zinahifadhiwa.
Ukichelewa sana kufatilia fedha inataifishwa inakuwa mali ya serikali coz watajua mhusika atakuwa alishafanyiwa sub na Mungu.
 
Jambo hili linapaswa kutazamwa tena upya kutokana na unyeti wake.

Ni lazima kabisa Serikali kupitia TCRA iweke Wazi kabisa kuhusu HAKI na WAJIBU wa Wamiliki hao tofaufi wa SIM Card kuhusiana na masuala haya ya kubadilisha Mmiliki wa SIM Card za simu kwa sababu suala hili linahusisha Usalama wa Taifa. Tukumbuke kwamba, suala la Usalama wa Taifa zima linaanzia na Usalama wa mtu mmoja mmoja katika Jamii.
Mfano mtu kakamatwa yupo ndani lockup kwa miezi yote mitatu, na simu kawaida wanakaa nazo polisi muda mwingine,kwahiyo akitoka lockup na laini zake anakuta zishapewa mtu mwingine,au mwingine yupo ndani amekosa kukamilisha masharti ya dhamana ya mahakama kwa kipindi chote cha miezi mitatu, inamaana akitoka simcard zake anakuta kapewa mtu mwingine, au ikitokea mtu kasafiri.
 
Kwakweli hili linapaswa kuangaliwa upya
Jambo hili linapaswa kutazamwa tena upya kutokana na unyeti wake.

Ni lazima kabisa Serikali kupitia TCRA iweke Wazi kabisa kuhusu HAKI na WAJIBU wa Wamiliki hao tofaufi wa SIM Card kuhusiana na masuala haya ya kubadilisha Mmiliki wa SIM Card za simu kwa sababu suala hili linahusisha Usalama wa Taifa. Tukumbuke kwamba, suala la Usalama wa Taifa zima linaanzia na Usalama wa mtu mmoja mmoja katika Jamii.
 
Pole sana.. Jitahidi kuziweka line zako hewani angalau mara moja kwa wiki hata kwa dakika 2 tu kisha ondoa kwenye simu...

Ukinunua Line kumbuka ile sio mali yako kwa 100%
 
ni muongozo wa tcra mkuu kufuta inactive numbers miez mitatu ni mingi mno mno kwa mfanya biashara next time soma maelezo kwenye kile kikadi baada yakununua line utajua wenye mtandao wamejipa haki zote juu ya line yako
 
Usipotumia line yako miezi 3, hasa usipokuwa hewani na kuweka vocha mara kwa mara inaondolewa hewani. Nimeona line zangu za mitandao mitatu tofauti zimekufa.

Nafikiri line isipokuaa hewani kwa muda wa miezi 3 au zaidi ndiyo inaweza kubadilishiwa Mmiliki wake, lakini siyo kutokuwa na salio.

Kwa uzoefu unaonyesha kwamba hata kama line haina salio lakini ipo hewani, huwa hapewi mtu mwingine.
Mathalani, kuna line mbili za SIM Card za Tanzania zipo nje ya nchi kwa muda wa zaidi ya miaka minne hadi Sasa lakini hazijafungiwa, huwa zipo hewani huko nje ya nchi. Aidha, lne hizo zimekuwa zikipokea SMS kutoka katika mitandao ya simu ya Tanzania na kutoka kwa mitandao ya simu iliyopo katika nchi hiyo, isipokuqa haziwezi kupiga wala kupokea miito ya simu except for EMERGENCY CALLS ONLY and calls from the SOS numbers.
 
Back
Top Bottom