Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Leo asubuhi nikiwa nazurura zurura mtaani kama kawaida yangu.
Nimekutana na gari la matangazo ya mnada wa hadhara likitangaza uwepo wa mnada kwa mali za watu walioshindwa kufanya marejesho ya fedha walizochukua toka taasisi za kifedha kama mikopo.
Mali zinazouzwa ni majumba na magari.
Jambo hili liliniweka kwenye tafakuri ya kina kuhusiana na nini hasa kimewakuta wahanga wa huu mnada.
1. Je, ni riba kubwa??
2. Kutokuwa na mipango ya kueleweka?
3. Matumizi mabaya ya fedha (kutumia fedha nje ya malengo).
4. Kuharibika kwa biashara kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa mkopaji.
5. Hali ya uchumi.??
Nikikumbuka hilo gari la mnada, nimeziogopa taasisi za kifedha.
Tusaidiane namna ya kukwepa aibu kama hizi kama mtu akichukua mkopo pale itapobidi.