Nimekutana na gari la matangazo ya mnada nimeogopa mikopo toka taasisi za fedha

Nimekutana na gari la matangazo ya mnada nimeogopa mikopo toka taasisi za fedha

Lazima wanafahamu, hakuna jipya chini ya jua

Ila kuzidi kujulikana zaidi ndio tatizo
Na pia inawezekana isiwe biashara ya upande mmoja.

Kwa maana kwamba baadhi ya maafisa wasio waaminifu nao wanashiriki.
 
Issue inahusisha watu wa tathmini pamoja na loan officers.
Hapo sasa umenena maana mtathmini anaweza kua kikwazo ama anayeidhinisha mkopo.

Basi ni biashara kubwa Sana.

Nimekaa nasikitika hapa kumbe ni biashara za watu.

Mjini mipango.
 
Jibu ni moja tu uchumi wa JIWE au uchumi wa kati.
Leo asubuhi nikiwa nazurura zurura mtaani kama kawaida yangu.

Nimekutana na gari la matangazo ya mnada wa hadhara likitangaza uwepo wa mnada kwa mali za watu walioshindwa kufanya marejesho ya fedha walizochukua toka taasisi za kifedha kama mikopo.

Mali zinazouzwa ni majumba na magari.

Jambo hili liliniweka kwenye tafakuri ya kina kuhusiana na nini hasa kimewakuta wahanga wa huu mnada.

1. Je, ni riba kubwa??

2. Kutokuwa na mipango ya kueleweka?

3. Matumizi mabaya ya fedha (kutumia fedha nje ya malengo).

4. Kuharibika kwa biashara kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa mkopaji.

5. Hali ya uchumi.??

Nikikumbuka hilo gari la mnada, nimeziogopa taasisi za kifedha.

Tusaidiane namna ya kukwepa aibu kama hizi kama mtu akichukua mkopo pale itapobidi.
 
Sio kila anaeshindwa kulipa mkopo bank ana Hali ngumu wengine ndio biashara zao hizo.

Nasema hivi " Hizo ndio biashara za watu wengine" mjini hapa.
Ni kweli mkuu, niliwahi sikia kuwa bwana mmoja alikopa akanunua coaster akapiga mishe fasta akajenga na akachana na marejesho
 
Sio kila anaeshindwa kulipa mkopo bank ana Hali ngumu wengine ndio biashara zao hizo.

Nasema hivi " Hizo ndio biashara za watu wengine" mjini hapa.
Kuna mtu alikopea nyumba zake zote lkn hakua na nia ya kulipa huo, akachukua hizo hela akajenga ukumbi matata sana na zingine akawekeza kwenye miradi mingine, akawachia bank wskahangahika kupiga mnada hizo nyumba huku yeye anaendelea na maisha mapya. Mwisho wa siku ana miradi na hadaiwi na bank japokua nyumba zimeenda.
 
Sio kila anaeshindwa kulipa mkopo bank ana Hali ngumu wengine ndio biashara zao hizo.

Nasema hivi " Hizo ndio biashara za watu wengine" mjini hapa.
Sijaelewa hapa... kwamba ndo biashara zao wenye madeni (wadaiwa) au wadeni (wadai)
 
Kuna mtu alikopea nyumba zake zote lkn hakua na nia ya kulipa huo, akachukua hizo hela akajenga ukumbi matata sana na zingine akawekeza kwenye miradi mingine, akawachia bank wskahangahika kupiga mnada hizo nyumba huku yeye anaendelea na maisha mapya. Mwisho wa siku ana miradi na hadaiwi na bank japokua nyumba zimeenda.
Ndicho namaanisha
 
Hapo sasa umenena maana mtathmini anaweza kua kikwazo ama anayeidhinisha mkopo.

Basi ni biashara kubwa Sana.

Nimekaa nasikitika hapa kumbe ni biashara za watu.

Mjini mipango.
Hahahaha mjini kila kitu ni frusa ki ukwel Leo ndio nimepewa mwanga nilikua sijui chochote
 
Sometimes wakopaji wanafanya michongo na watu wa tathmini.

Labda nyumba ya 30M yeye anakukadiria ina thamani ya 60M. Hivyo ukikopa hiyo 60M lengo linakuwa siyo kurejesha bali ndio imetoka hiyo, wao watauza hiyo nyumba.

Na kuna watu kila wakijaribu kuuza nyumba zao wanakwama, wanaamua kuzichukulia mikopo
Reference ;Tai five Mwanza
 
Mwingne anajenga nyumba kwa 50M labda alaf anaenda kuvuta mkopo wa 80M na anajidai kashindwa kulipa hiyo ni biashara kwa wengine na kwa wengine ni matatizo kweli
 
Kufilisika hakujawahi kua AIBU.

Nasaheshimu Sana watu wanaofilisika
 
Back
Top Bottom