Nimekutana na Mchina aliyekuja kama kibarua Tanzania ila sasa yeye ni Big Boss

Nimekutana na Mchina aliyekuja kama kibarua Tanzania ila sasa yeye ni Big Boss

Ni ukweli, Mchina yuko sahihi. Watanzania wengi akili zao zinawaza;
1. Mapenzi
2. Mapenzi
3. Mapenzi
4. Wizi
5. Wizi...
 
Jana kuna mchina nilikutanishwa nae ni CEO wa kiwanda cha uzalishaji wa marine boards, melamain boards, pliewoods na MDF ambacho wamekijenga pale Mafinga.

Nilimuuliza ABCs za maisha yake hapa Tanzania na akanambia yafuatayo.

1. Yeye alikuja Tanzania kipindi cha ujenzi wa uwanja wa mpira wa Benjamini Mkapa na alikuja kama kibarua wa kulipwa posho kwa siku.

2. ⁠Uwanja ulipoisha kwasababu alipokuwa kibarua alikua akijituma sana boss wake alimwamini na kumpa kazi ya kusimamia Makarasha Chalinze kama Foremen.

3. ⁠Walipomaliza mradi wa Chalinze yeye aliona kurudi china haiwezekani kwani kwa muda aliokaa TZ kaona fursa nyingi na utajiri mwingi.

4. ⁠Aliamua kumshawishi boss wake kwamba kama wao wanarudi china yeye anaomba abaki TZ aone fursa na ndipo alipoenda mafinga na kuona fursa iliyopo kwenye miti. Na akamwambia boss wake wafungue kiwanda yeye atakisimamia na atahakikisha mtaji unarudi na faida wanapata.

5. ⁠Boss Alikubali na sasa kile kiwanda ni kikubwa yeye ndo msimamizi na anamiliki billions of money .

NILIMUULIZA KWA MUDA ALIOKAA AMENIFUNZA NINI NDANI YA TANZANIA.

1. Alinambia nyie Watanzania ni watu wajinga sana kwasababu mnaamini kwenye miujiza kwakutumia muda mwingi kusali na kulala.

2. ⁠Fedha mlizotafuta kwa jasho mnachezea kamali/gulugulu alilotengeneza mchina mkiamini mtapata utajiri, akamalizia hakuna utajiri wa namna hiyo.

3. ⁠Hamjui matumizi ya simu, muda mwingi mnatumia simu kwa vitu vya kijinga akishangaa mtanzania anaweza kukupigia cm mara 20 mfululizo kama hupokei simu yake. Yeye Ana muda maalum wa kupiga cm na kupokea simu.

4. ⁠Mnaabudu na kuamini wanasiasa wanaweza tatua shida zenu kumbe wao ndo wanawategemea ninyi mtatue shida zao.

5. ⁠Mfumo wenu wa Elimu ni wa kijinga kwasababu haumuandai mtoto kuwa mbunifu na kutumia maarifa yake kubuni/ama kuzalisha bidhaa ili ziingie sokoni.
kama kuna kitu kizuri nimekipata leo hii basi ni hiki.
kuna baadhi ya vitu tunahitaji kufanyia kazi.
huwa najiuliza mara nyingi tunalalamika ni kweli kabisa hatuwezi kutoka tuliko?
nimekuwa najitolea kuwaelekeza watu wanaofikiri wao ni maskini kwa kuwafundisha tu na baada ya muda labda mika mitatu wanafanikiwa na wengine wananiuliza Mwalimu unakwama wapi?
ni swali fikirishi sana lakini ifike wakati tulifanyie kazi.
najiuliza tu kwa kadri ya taaluma zetu ni kweli tunaweza kukosa watu 200 wa kuchanga mtaji wa 500,000 kila mmoja? na tukapata 100,000,000/-
  1. tukiwekeza kwenye gv bond face value itakuwa 110,727,624.44
  2. tutapata gawiwo kila mwaka la faida 13,398,042 na kufanya jumla ya gawio kwa miaka 20 kuwa 267,960,851.14
  3. tukichukua hizi bond kama security tukakopa 50,000,000 kwa riba ya 18% kwa kila mwaka (reducing) kwa miaka 5 rejesho linaweza kuwa 15,400,000 kwa mwaka ikiwa kupon rate itachangia 13,398,000 je mradi untashindwa kumudu kuchangia rejesho la 2,002,000?
  4. kama tunafikiri inawezekana au hawezekani karibuni kwa mawazo zaidi hata tusipofanya sisi basi tushiriki kwa kutoa michango ya mawazo wengine wafanye na sisi watutume na tuendelee kulalamika
  5. sasa nini cha kufanya:-
    1. tufikirie nini kinaweza kufanyika (mradi rahisi kwa mtaji wa 50m) ambao baada ya kutoa gharama za mradi unaweza kuingiza 20%
    2. jinsi ya kuutekeleza ikiwa ni pamoja na mipangilio ya utekelezaji na jinsi ya kusimamia.
 
'wanasiasa hawawezi waletea maendeleo'-kauli ya kijinga waipendayo CCM.

Unadhani China bila uongozi wa kisiasa wa kina Deng, wasingefungua milango ya uchumi, wasingewekeza kwenye umeme na miundombinu kama reli, wasingewekeza kwenye elimu ya ufundi na kuwabeba wabunifu wa ndani ingekua hapa ilipo leo?

Japan miaka ya nyuma walikuwa wakisemwa kuwa ni wavivu, lakini baadae miundombinu ya viwanda ilipokua kubwa, hoja ya uvivu Ikafa.
 
Back
Top Bottom