Nimekutana na Mchina aliyekuja kama kibarua Tanzania ila sasa yeye ni Big Boss

Kama ulipomuuliza ndo kakujibu hivyo basi kakuona wewe ndo ndo mjinga.... Kwa sababu gan? Kwa sababu hayo aliyoyafanya yeye ni kutokana na exposure aliyokuwa nayo kutokea nchini kwao alipotoka, Wenzetu wameshafundishwa sana masuala ya production by action wakati wewe unahangaika ku-copy notes za Mabala ze Fama pale shuleni kwenu Kitobokikubwa Secondary School... Hivyo sio akili tuu bali hata mazingira ya upatikanaji wa vitendea kazi huwafanya jamaa kujua afanye nini ili apate nini ndo sababu hata wenyewe kwa wenywe wanaaminiana na kuwezeshana.

Huwezi kuwalinganisha watu ambao wanajua maana ya Family co-operation in Business na sisi ambao tumetoka kwenye familia ambazo mzazi hajui kupanda ila anataka kuchuma, (Kila mzazi anawaza mtoto akue akajitegemee ili amtegemee) Mtoto kabla hujakua ushakuzwa na hali duni ya familia yenu.

Nilitegemea angekosoa mifumo yetu ya maisha na Hali duni tulizonazo kama sababu ya kutokufika mahali fulani lakini kama anasema sisi ni wajinga basi nafikiri alikuzungumzia wewe kimafumbo

Unaweza ukazungukwa na malighafi kibao ila usiweze kujua ni namna gani utayatumia kutengeneza bidhaa kutokana either na kutokuwa na ujuzi au kukosa vitendea kazi so, What Will you expect?
 
Huwezi kuwalinganisha watu ambao wanajua maana ya Family co-operation in Business na sisi ambao tumetoka kwenye familia ambazo mzazi hajui kupanda ila anataka kuchuma, (Kila mzazi anawaza mtoto akue akajitegemee ili amtegemee) Mtoto kabla hujakua ushakuzwa na hali duni ya familia yenu.
Daah Mungu aniepushe na hii dhahama
 
ww unaishi kwa shemej yako ukila ukishiba unahisi shemej yako anaokota ela , leo naweka umeme nakuta kodi yao wamepandisha na mshahara hawajapandisha huku mfumuko wa bei wa vyakula na usafiri , halaf unaandika utopolo wako , ENDELEA KUISHI KWA SHEMEJ YAKO IPO SIKU UKIANZA JITEGEMEA UTAPATA AKILI
Nunua solar acha kulaza vitukuu vyako gizani..karne hii unailalamikia serikali kwani wewe umefanyia nini hili taifa mpaka sasa
 
Jana kuna mchina nilikutanishwa nae ni CEO wa kiwanda cha uzalishaji wa marine boards, melamain boards, pliewoods na MDF ambacho wamekijenga pale Mafinga.

Nilimuuliza ABCs za maisha yake hapa Tanzania na akanambia yafuatayo.

1. Yeye alikuja Tanzania kipindi cha ujenzi wa uwanja wa mpira wa Benjamini Mkapa na alikuja kama kibarua wa kulipwa posho kwa siku.

2. ⁠Uwanja ulipoisha kwasababu alipokuwa kibarua alikua akijituma sana boss wake alimwamini na kumpa kazi ya kusimamia Makarasha Chalinze kama Foremen.

3. ⁠Walipomaliza mradi wa Chalinze yeye aliona kurudi china haiwezekani kwani kwa muda aliokaa TZ kaona fursa nyingi na utajiri mwingi.

4. ⁠Aliamua kumshawishi boss wake kwamba kama wao wanarudi china yeye anaomba abaki TZ aone fursa na ndipo alipoenda mafinga na kuona fursa iliyopo kwenye miti. Na akamwambia boss wake wafungue kiwanda yeye atakisimamia na atahakikisha mtaji unarudi na faida wanapata.

5. ⁠Boss Alikubali na sasa kile kiwanda ni kikubwa yeye ndo msimamizi na anamiliki billions of money .

NILIMUULIZA KWA MUDA ALIOKAA AMENIFUNZA NINI NDANI YA TANZANIA.

1. Alinambia nyie Watanzania ni watu wajinga sana kwasababu mnaamini kwenye miujiza kwakutumia muda mwingi kusali na kulala.

2. ⁠Fedha mlizotafuta kwa jasho mnachezea kamali/gulugulu alilotengeneza mchina mkiamini mtapata utajiri, akamalizia hakuna utajiri wa namna hiyo.

3. ⁠Hamjui matumizi ya simu, muda mwingi mnatumia simu kwa vitu vya kijinga akishangaa mtanzania anaweza kukupigia cm mara 20 mfululizo kama hupokei simu yake. Yeye Ana muda maalum wa kupiga cm na kupokea simu.

4. ⁠Mnaabudu na kuamini wanasiasa wanaweza tatua shida zenu kumbe wao ndo wanawategemea ninyi mtatue shida zao.

5. ⁠Mfumo wenu wa Elimu ni wa kijinga kwasababu haumuandai mtoto kuwa mbunifu na kutumia maarifa yake kubuni/ama kuzalisha bidhaa ili ziingie sokoni.
Anyway....
Haya maneno ni yako.
 
tunazungumiza kikwazo na sio chama kututoa kwenye matatizo , Mtu anafungua mradi ccmu wanataasisi hazihesabiki zinapita zinakusanya ela ukigoma wanakutungia kesi bila kusahau mahakama ni yao , kwa hali hii unajikwamuaje , hao wakina Mo na Bakhresaa ipo siku wataongea kama ccmu itatoka madarakan
Mbona siku za karibuni umekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wajinga?
 
Jana kuna mchina nilikutanishwa nae ni CEO wa kiwanda cha uzalishaji wa marine boards, melamain boards, pliewoods na MDF ambacho wamekijenga pale Mafinga.

Nilimuuliza ABCs za maisha yake hapa Tanzania na akanambia yafuatayo.

1. Yeye alikuja Tanzania kipindi cha ujenzi wa uwanja wa mpira wa Benjamini Mkapa na alikuja kama kibarua wa kulipwa posho kwa siku.

2. ⁠Uwanja ulipoisha kwasababu alipokuwa kibarua alikua akijituma sana boss wake alimwamini na kumpa kazi ya kusimamia Makarasha Chalinze kama Foremen.

3. ⁠Walipomaliza mradi wa Chalinze yeye aliona kurudi china haiwezekani kwani kwa muda aliokaa TZ kaona fursa nyingi na utajiri mwingi.

4. ⁠Aliamua kumshawishi boss wake kwamba kama wao wanarudi china yeye anaomba abaki TZ aone fursa na ndipo alipoenda mafinga na kuona fursa iliyopo kwenye miti. Na akamwambia boss wake wafungue kiwanda yeye atakisimamia na atahakikisha mtaji unarudi na faida wanapata.

5. ⁠Boss Alikubali na sasa kile kiwanda ni kikubwa yeye ndo msimamizi na anamiliki billions of money .

NILIMUULIZA KWA MUDA ALIOKAA AMENIFUNZA NINI NDANI YA TANZANIA.

1. Alinambia nyie Watanzania ni watu wajinga sana kwasababu mnaamini kwenye miujiza kwakutumia muda mwingi kusali na kulala.

2. ⁠Fedha mlizotafuta kwa jasho mnachezea kamali/gulugulu alilotengeneza mchina mkiamini mtapata utajiri, akamalizia hakuna utajiri wa namna hiyo.

3. ⁠Hamjui matumizi ya simu, muda mwingi mnatumia simu kwa vitu vya kijinga akishangaa mtanzania anaweza kukupigia cm mara 20 mfululizo kama hupokei simu yake. Yeye Ana muda maalum wa kupiga cm na kupokea simu.

4. ⁠Mnaabudu na kuamini wanasiasa wanaweza tatua shida zenu kumbe wao ndo wanawategemea ninyi mtatue shida zao.

5. ⁠Mfumo wenu wa Elimu ni wa kijinga kwasababu haumuandai mtoto kuwa mbunifu na kutumia maarifa yake kubuni/ama kuzalisha bidhaa ili ziingie sokoni.
Sasa anza kumuandaa mtoto wako si usha jua? si umejua tatizo ni mfumo wa elimu? anza sasa
 
Ni ukweli usiopingika elimu ya kukariri haitufai na tumeona mpaka viongozi wakiongelea sayansi ya kukariri maana unasikia kabisa kakariri
Wanajituma sana hata kama hela zimeingizwa au mashine zimekuja kutoka kwa mafia hatujali mradi wanaajiri watu
Ila na sisi tupeleke hela kwao sasa
tusha jua sasa badilika anza na watoto wako, acha kuwapeleka English medium daily wanapewa Homowrk, haziwasaidii
 
Sawa, tumezaliwa katika jamii isiyoona fursa na kusoma katika mfumo wa elimu wa kijinga lakini sasa tunatoka huko ujingani, tumeanza kujitafuta na kujitambua, hatutaki tena watoto wetu wawe na mentality mbovu za elimu kama tulivyosoma sisi. Nchi hii ina fursa na utajiri mwingi tuuone na tuumiliki
 
Back
Top Bottom