Nimekutana na Mchina aliyekuja kama kibarua Tanzania ila sasa yeye ni Big Boss

Ni ukweli, Mchina yuko sahihi. Watanzania wengi akili zao zinawaza;
1. Mapenzi
2. Mapenzi
3. Mapenzi
4. Wizi
5. Wizi...
 
kama kuna kitu kizuri nimekipata leo hii basi ni hiki.
kuna baadhi ya vitu tunahitaji kufanyia kazi.
huwa najiuliza mara nyingi tunalalamika ni kweli kabisa hatuwezi kutoka tuliko?
nimekuwa najitolea kuwaelekeza watu wanaofikiri wao ni maskini kwa kuwafundisha tu na baada ya muda labda mika mitatu wanafanikiwa na wengine wananiuliza Mwalimu unakwama wapi?
ni swali fikirishi sana lakini ifike wakati tulifanyie kazi.
najiuliza tu kwa kadri ya taaluma zetu ni kweli tunaweza kukosa watu 200 wa kuchanga mtaji wa 500,000 kila mmoja? na tukapata 100,000,000/-
  1. tukiwekeza kwenye gv bond face value itakuwa 110,727,624.44
  2. tutapata gawiwo kila mwaka la faida 13,398,042 na kufanya jumla ya gawio kwa miaka 20 kuwa 267,960,851.14
  3. tukichukua hizi bond kama security tukakopa 50,000,000 kwa riba ya 18% kwa kila mwaka (reducing) kwa miaka 5 rejesho linaweza kuwa 15,400,000 kwa mwaka ikiwa kupon rate itachangia 13,398,000 je mradi untashindwa kumudu kuchangia rejesho la 2,002,000?
  4. kama tunafikiri inawezekana au hawezekani karibuni kwa mawazo zaidi hata tusipofanya sisi basi tushiriki kwa kutoa michango ya mawazo wengine wafanye na sisi watutume na tuendelee kulalamika
  5. sasa nini cha kufanya:-
    1. tufikirie nini kinaweza kufanyika (mradi rahisi kwa mtaji wa 50m) ambao baada ya kutoa gharama za mradi unaweza kuingiza 20%
    2. jinsi ya kuutekeleza ikiwa ni pamoja na mipangilio ya utekelezaji na jinsi ya kusimamia.
 
'wanasiasa hawawezi waletea maendeleo'-kauli ya kijinga waipendayo CCM.

Unadhani China bila uongozi wa kisiasa wa kina Deng, wasingefungua milango ya uchumi, wasingewekeza kwenye umeme na miundombinu kama reli, wasingewekeza kwenye elimu ya ufundi na kuwabeba wabunifu wa ndani ingekua hapa ilipo leo?

Japan miaka ya nyuma walikuwa wakisemwa kuwa ni wavivu, lakini baadae miundombinu ya viwanda ilipokua kubwa, hoja ya uvivu Ikafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…