Hii kwenye saikolojia huwa tunaiita Trauma. Unamkumbuka mtu aliyekufanyia mambo mabaya kwenye nyakati muhimu za maisha yako. Kiukweli, mtu afanyiwe ubaya wakati mwingine lakini siyo kipindi cha makuzi (Adolescence/Puberty), huwa hasahau kabisa kwasababu ndicho kipindi ambacho hutengeneza tabia atakazoenda nazo ukubwani. Kuna mambo mtu anaweza kuhisi kawaida, lakini kuchangiwa na ofisi nzima ya walimu kwa kosa hujafanya au kudhalilishwa mbele ya shule nzima ni vitu ambavyo mtu wa kawaida huwezi kuvisahau kabisa kwasababu vinaathiri afya ya akili ya mtu.
Japo sasa mkuu
Poker , jambo kama hili unaliachia tu, litakutesa wewe zaidi kuliko yeye kwasababu unalikumbuka na linakuteletea uchungu. Halafu hapohapo linakupa furaha ya muda mfupi kuona yeye anateseka (Sadism). Wenzetu wazungu haya mambo huwa wanayatilia sana mkazo kwasababu yaanathiri afya ya akili ya mtu, kama hatakuwa makini.