Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

puker

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
1,001
Reaction score
2,010
Habar zenu wadau

Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielewi nifanye nini. Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.

Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba.

Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali. Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu. Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.

Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.

Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.

Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana[emoji847] Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.

************

Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?

Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? [emoji849][emoji50] Akawa anacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?

Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza

Sehemu ya Pili


Sehemu ya Tatu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha niliwahi vagaa mrembo kariakoo kitimtimu kwenye kulala baada ya wiki..nikataka kuzima taa nilichokiona sitokaa nisahau mpaka nakufa..haya mambo yapo jamani..omba sana mungu, naona dalili za kufilisika kwako' be very careful..mm huyo msichana hata sijui ilikuaje ila nilikutanishwa na mtu ambae akataka kunitambulisha kwa huyo bi dada mwenye maduka kariakoo..ili tufanye joint venture..nimeteseka mnooo kuanzia 2016..ipo siku ntakuja na mkasa wake, ila naona downfall yako..si mtu mzuri huyo!
 
Anavunja nazi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha niliwahi vagaa mrembo kariakoo kitimtimu kwenye kulala baada ya wiki..nikataka kuzima taa nilichokiona sitokaa nisahau mpaka nakufa..haya mambo yapo jamani..
Nafikir ww unaweza kunielewa Ni kitu gani nazungumzia Ni wiki mbili tu, ila mambo ninayo kutana nayo...sijapata kuona maishani mwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwaje mkuu....
 
Watu wa aina yenu kwenye jamii hamkosekani, hvy sishangai ila nivyema kuangalia content ya mtoa mada kuliko hvy vitu vingine haviwez kukusaidia kitu...zaidi Ni kudhihirisha namna gani una upeo mdogo wa kufikir

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikir ww unaweza kunielewa Ni kitu gani nazungumzia Ni wiki mbili tu, ila mambo ninayo kutana nayo...sijapata kuona maishani mwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora hata wewe umestuka mapema, mm nimnywaji wa pombe yani story yako zinaendana somehow na yangu..mpaka usingizi umekatika..nilikua kila nikikaa nae jionj nikitoka kibaruani naona mauza uza ya kishenzi..siku alipotaka tukalale tukapiga kinywaji akasema muda umeenda twende kwangu ulale asubuhi uamke uende kazini..

aiseee! Pombe ilikata..nikakurupuka nikawa naanza kuvaa nguo..ardhi ya mule chumbani ikawa ina cheza cheza..inshort nilipotaka taa izimwe alinyoosha mguu na mpaka switch ilipo ni parefu kwenye kale kagiza nilimuona akibadilika uso mara sura hii mara ile nikawasha taa..alinibadilikia..nikalazimisha kuondoka kwani nilifika mbali sasa? Kitu cha fisi wawili wananifuata..giza totoro..milio ya wanyama..hapo ni mikocheni b dsm..

ukiwa kijana una kipato na una muonekano flani ni shida sana..mungu akutangulie brother, natamani tuonane ! Hapa nahema nikiwaza nilivoteseka, kazi nikapoteza na aliniapia wakati namkataa nilimwambia sikuelewi..yani dahh nakuonea huruma..af hua wana access na simu wanajua unawasiliana na nani..
 
kuna sehemu yeyote imeandikwa Wanaume tusitumie emoji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…