Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nafikir ww unaweza kunielewa Ni kitu gani nazungumzia Ni wiki mbili tu, ila mambo ninayo kutana nayo...sijapata kuona maishani mwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yep hayo kama ni Mazur kula maisha acha woga umependwa na mtoto wa kitajiri. Kula mzigo fasta zari hilo la. Mentali lisije hamia kwangu ila.mi nmeoa labda atakua mkw mdogo

(Pambana na hali yako) ..# Kwetu Mwanza Nyegezi#
 
ungeweka full mkasa ingependeza mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezeakana zimwi lenyewe limefungua ID humu linasoma tu komenti haha. Inawezekana hicho kidada kinachojifanya jini ni wale waganga matapeli anakuvuruga halafu baadae mwenzake anatokea akupe tiba ya majini.

On a serious note nenda kawaone viongozi wa kiroho. Tatizo lako inawezekana ni kubwa sisi tunafanya utani hapa
 
Sasa wewe muda wote unalialia tu niko kwenye wakati mgumu,wakati mgumu. Mimi sijaona jini alipokuweka kwenye wakati mgumu au mazingira hatarishi,ila ni wewe mwenyewe unajihatarishia. Kuna shida gani wewe ukiolewa na jini? Hakuna mahala amekufanyia vibaya,wala kukutukana,ila wewe unamtukana. Kweli cha moto unaweza ukakiona ksbb unamtukana,kama kumchokoza. Mshana (nafikiri) slishawahi kuna majini wazuri na wabaya. Huyo jini mzuri kabisa huyo,unamuogopa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Mkuu kwa mkasa huu. Haya mambo yapo Sana Tena sana.

Kuna makosa kadhaa umeshayafanya tayari na yatakukusababishia fadhaa na mateso zaidi km hutachukua ushauri wa moto uliopewa na wadau.

Makosa hayo ni pamoja na kukubali kuvaa zile nguo ulizopewa zawadi kwa sababu rahisi ya umeme na mikunjo ya nguo zako.
(Tayari zilisharogwa kupitia manukato uliyoyahisi/nusa)

Pili kukubali kuzipeleka kwake ukiwa tayari ulishazivaa(zikiwa na jasho lako). Ni rahisi kwa mshirikina yeyote kukufanyia lolote kupitia jasho hilo.
Tatu kuendelea kuzishikilia zawadi unazopewa za pesa (zirudishe kwa namna yoyote), ikishindikana kazitoe zaka na sadaka tena bila tamaa ya moyoni. Na uwe tayari kuzilipa km utadaiwa baada ya kuzitoa sadaka.

Nne ni kuwa naona unapuuza ushauri ya kufanya maombi maalumu ya kufunga hata kwa kushirikisha watumishi/ wamwabuduo BWANA MUNGU kwa roho na kweli.
(Hapa niwe serious kidogo) epuka mambo ya roho ya uponyaji na jamii ya waabuduo miujiza kama silaha ya UKRISTO - utaongezewa mapepo huko.

Jitahidi kuwaza na kutenda km unavyokusudia pasipo hofu hata km atakuingilia katija Kila hatua ya kujiondoa kwako kwake.(huyo jini)

Nne hakuna mwanadamu anayeweza kupambana na jini/shetani kwa nguvu zake/zetu wenyewe. Ni ubatili kuita mtu mwenye nguvu aje akusaidie.
(Wenye nguvu ni wale wanaomtegemea BWANA MUNGU PEKEE)

TANO NA MWISHO.
Usiendelee kutoa muendelezo wa mashindano yako na jini kwa sasa. Kwani kupitia haya unayoyaandika ndivyo unavyojianika udhaifu wa roho yako (siyo moyo wako). Na hivyo adui akatumia fursa hii.

Jitahidi kuiokoa nafsi yako kwa gharama KUU YA DAMU YA YESU KRISTO. Tumepewa fursa ya uhai na MUNGU MWENYEZU si kwa bahati mbaya mkuu. Uzima na uhai ni jukumu letu kuvilinda na kuvitunza kwa nguvu na bidii zote.


HAKUNA BAYA LINALOMSHINDA BABA MUNGU MUUMBAJI KUPITIA YESU KRISTO

BWANA MUUNGU NA AKUKINGE KWA UOVU HUU UNAOKUAMBATA KWA SASA NA HATA MILELE. NAKUOMBEA HAYA KATIKA JINA LA YESU KRISTO. AMINA.
 
Nashukuru kwa ushauri wako mzuri mkuu, kwanza nipende kubainisha hili mm Ni mkristo kamaili naamini katika Yes kristo, hv ninavyoongea naendelea na huduma ya maombezi kwa Hali niliyokuwa nayo mwanzo nisingeweza hata kuandika uzi huu, Maombi ndio yamenipa ulinzi na nguvu juu ya Vita kubwa niliyonayo kwa Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Mkuu una mengi ya kutueleza
 
Mungu akusaidie na ulete mrejesho ukiwa mzima kabisa
 
nikakuta jamaa ananiangalia kwa utulivu na hata alipojua nimemuona hakuondoka nilipopiga kelele hakuondoka nikaduwaa siamini baada ya dk tatu akaondoka mwenyewe

Hapo ndio umejua kusolve vitu kistaarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…