SEHEMU YA TATU: Nimekutana na mwanamke wa ajabu naanza kuingiwa na hofu walimwengu naomba mnisaidie.
Baada ya sms ile ya tigo pesa...nikajaribu kupiga ile namba iliyotuma pesa simu haikupokelewa. Mwishoni nikaamua kuacha nayo. Nikaona mambo yanazidi kuniwia magumu, nikaona kabisa Tatizo linaenda kuwa kubwa, ikabidi nichukue simu nimpigie mama yangu, nikamuelezea ilivyokuwa kuanzia mwanzo wa tukio mpk hatua tuliyofikia, kiukweli mama yangu aliogopa sana, ingawaje hakuonesha wazi zaidi ya kunitia Moyo na kuniasa nimuombe Mungu bila kuchoka lkn pia, nitafute mtumishi wa Mungu anifanyie maombi maalum.
Ila nilimuonya sana mama yangu, asije akamshirikisha hiyo ishu mtu yoyote mpk nitakapo mpa ruksa ya kufanya hvy, kwa 7bu anaweza ndio Akawa anaongeza Tatizo na sio kulipunguza.
Mama alinielewa, ila akanishauri si vyema kuendelea kukaa dukani kwa kipindi kile yanaweza kunikuta makubwa zaidi ya Yale. Siku hiyo ilikuwa ijumaa nilimpigia simu mdogo wangu anaeishi maeneo ya kigambon aje kunishikia Kuna dharula nimepata, Mara nyingi anakuwaga yy kipindi mm sipo nimetoka kwa mambo yangu mengine. Mpk kufikia mida ya saa 10 jion alikuwa ameshafika nikamkabidhi duka na kurudi zangu nyumban. Sikuwa na furaha siku Hy, nilikuwa nawaza mambo mengi nisiyokuwa na majibu nayo, nikiwa kwenye gari mdogo wangu akanipigia simu kuwa Kuna mgeni wangu pale dukani, nikamuuliza Ni wa kike au wa kiume, akanijibu ni wakike, nikastuka! Nikamuuliza amesema anashida gani, akasema amekuja kuchukua mzigo wake alikuachia ww Jana...akasema umtunzie atakuja kupitia.
Hapo ndio nikachanganyikiwa kabisa, inawezekanaje. Huyu dada atakuwa anataka nini. Niliishiwa pozi, nikakataa simu, baada ya muda kidogo simu ikaita Tena ila sikupokea. Ikumbukwe nguo anazohitaji ndio nimezivaa wakat huo, na niyeye ndie aliesema ameninunulia iweje aje na kuzidai Tena, ina maana Hawa Ni watu tofauti? Je huyu anae nipigia simu Ni Nan? Na maswala ya nguo kayafahamu vp! Nilibaki na mshangao, nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo, sms ikaingia kwenye simu yangu, kuisoma nakuta imeandikwa .." Nakupenda ila usisubutu kuniepuka, Kama unampenda mama yako, fwata nitakacho kwambia, kesho njoo feri saa 7 mchana upande wa kigamboni ukiwa umeziweka hizo nguo kwenye mfuko, uje kunikabidhi nimpelekee niliemkusudia.
Baada ya ujumbe huo, nikastuka sana hapo hapo nikampigia simu mama, nikamuuliza uko salama? Akasema ndio...akaniuliza Kuna nini, nikamjibu hakuna kitu, najua mama yangu anapresha pia ananipenda sana, hapendi kusikia nateseka...ila nikaendelea kumsisitiza juu ya Jambo nililomwambia kuhusu huyo mwanamke anayenifatilia asisubutu kumwambia mtu yoyote. Hii siku niliumia sana...tuwapende sana mama zetu mama alilia sana, akaniambia mwanangu kuwa makini wanataka kukuuwa, nikawa namwambia asijali hawawez niua, naamini Mungu yuko nami. Sikutaka kuendelea kusikia mama yangu akiangua kilio kwa ajili yangu. Niliwaza mambo mengi sana siku Hy, ki ukweli ilikuwa Ni siku mbaya kwangu. Nikamtumia sms mdogo wangu nikamwambia mwambie huyo dada aondoke nitawasiliana nae...akanijibu ameshaondoka muda mrefu amesema atakutafuta kwenye simu nikamjibu poa.
Nilifika nyumbani, nikaingia bafuni kaoga..nilivyorudi nikawa nimejilaza kitandani...nikapitiwa na usingiz mzito sana..nikiwa usingizini nikaota tupo kwenye ile ile bustani ya Jana tuliyokuwa tunalazimishana kuoga, Ila wakat huu haikuwa, hivyo wote tulikuwa tumevaa nguo nyeupe, mm nilivaa mavazi Fulani hv meupe mfano wa kaunda suit na yeye alikuwa amevaa Yale mavazi Kama ya kihindi ila nimeupe kabisa, tulikuwa tunakula na kunywa, yalikuwa ni matunda ndizi, apples, zabibu na vitu Fulani hv mfano wa tende ila ile juice ilikuwa Ni nyekundu Kama mvinyo hvy...
Tukawa tunacheka na kufurah sana, akaniambia Fulani....(Akataja jina langu) akasema Nilikuwa nakupenda kitambo...ila Fulani (Akataja jina la x girlfriend wangu) tuliekuwa tumeachana Kama miez nane iliyopita, kwamba yule ndie aliekuwa akiniekea vikwazo..nikamuuliza kwa nini, akasema alikiwa mtu wa dini sana, (Ni Kweli nikipata mdada alikuwa mlokole na mtu wa maombi sana yeye na kanisa kila wakati) hukumbuki hata sababu ya kuachana kwenu ilikuwa ni pombe alizokuwa anakukataza usinywe lkn pia ukawa unataka mfanye mapenz yy akasema hayuko tyr mpaka mpaka utakapo muoa? Na we ukamwambia hauko tayar kuoa kwa muda huo Ni heri muachane kuliko kuendelea kuwa na mpenzi jina mnaishi Kama kaka na dada, Nikawa nashangaa sikumjibu kitu.....Akacheka sana huku akinibusu kwenye paji la uso...akaniambia we ndio mume wangu mtarajiwa, ila kuanzia Sasa hata mm sitak unywe pombe...sitak uwe na mwanamke mke mwingine tofauti na mm...akaendelea kusema mpenzi mm Nina wivu sana, pia Nina hasira...na hasira zangu Ni mbaya sana, naweza kukuharibia kabisa maisha yako, tafadhali fuata nilichokuwa utanufaika na vingi sana. Sikumjibu kitu pia nikawa nimeshikwa na bumbu wazi akaniambia tusimame Kuna kitu nataka kukuonesha, tukatembea Kama mwendo wa dk tatu....Akaniambia unapaona kule...akanionesha kwa kidole kwa mbali nikamwambia ndio, kuna nyumba nzuri sana zimepakwa rangi Kama ya dhahabu, akaniambia kule Ni kwetu mpenz mm na wewe, tukishakuwa mke na mume tutaishi kwenye zile nyumba kule. Baada ya kuniambia hvy akanikumbatia huku akinibusu maeneo ya shingoni...nikastuta, kuangalia simu ilikuwa ni usiku sana mida ya Kama saa 8 hv usiku. Nikasali sana usiku ule nikalia sana, hafla nikasijikia kichefu chefu na tumbo kunivuruga sana, nikatapika vitu Fulani hv vyeusi sana vinatoa harufu mbaya mno.
Sikupata usingiz mpaka kunakucha, nikawa najiuliza ile ndoto ina maana gani hasa, ina maana nimeshafunga ndoa na jini? Nikaona hapana...alikuwa ananilisha Nini ambacho kilifanana na matunda kupelekea kutapika kiasi kile! Huwez amini nilishikwa na hasira Sana asubuhi ile.
Ikumbukwe siku hiyo ya J.mosi tarehe 29 ndio yule dada anataka tuonane feri nimkabidhi nguo zake ambazo tayari nilikwisha zivaa, tukutane pale saa 7 mchana, nilichoshangaa kwenye ndoto hakuzungumzia kabisa swala lile...nikajiapiza sitomwogopa Tena na tukionana nitamwambia sitaki anifwatikie Kama Ni ele zake sijatumia hata Mia, na Niko tayar kumrejeshea ili mradi aachane na maisha yangu niwe na amani.
Ilipofika mida ya saa 5 hv asubuh safar ya kwenda feri ikaanza nikiwa na mfuko niliweka zile nguo na Wala sikuzifua..nlipofika feri pale posta nikaa sehemu nasubir saa 7 ifike ili nipande panton...nikijaribu kupiga ile namba yake inaita lakini haipokelew, ilipofika Kama saa 7 kasoro dk8 hv, sms ikaingia nimefika njoo nakusubiria. Nikakataa ticket ya kupanda panton kwa ajili ya kuja upande wa pili wa kigamboni....Nilikuwa naangaza macho kila mahali kuangalia Kama yupo karibu yangu...sikumuona, tulipofika wakat tunashuka hamadi nakutana na gari nyeusi aina ya kulga inapiga honi mbele yangu naona mkono umetolewa nje upande wa dereva kuashiria nimpe kitu na Nilikuwa karibu nalo...kuchungulia hv, Ni yule yule mwanamke...alionesha ishara ya kuhitaj ule mzigo nilivyomkabidhi akafunga kioo(vilikuwa tinted)..gari ikaanza kutembea taratibu kuelekea kwenye panton, nilikaa pale getini wanapouzia viatu vya kike nikiwa nachungulia lile gari mpk linaingia kwenye panton, simu yangu ikaita Tena...kuangalia Ni yeye...alisema tu Ahsante mpenzi akawa anacheka, kabla hajakata simu nikamwambia aniache na maisha yangu...nilimtukana sana siku Hy sijui nilikumbwa na Nini, sikumwachia hata nukta ya kuongea..kuja kuangalia simu hv...muda mrefu ilisha katwa, Ni Kama nilikuwa naongea mwenyewe.
Kimbembe...siku ya tar 31 mkesha wa mwaka mpya, tulikuwa tumepanga kwenda mkesha uwanja wa taifa na rafiki yangu, mchana alipiga simu nyingi sikupokea...akatuma sms akaniambia najua unachotaka kufanya olewako uende huko unakotaka kwenda, nitakuonesha Mimi Ni Nani. Nikatuma sms mfululizo za kumtukana sana, nikamwambia asinitishe, asinipangie Cha kufanya...naweza kufanya Jambo lolote ninalijisikia...hakujibu kitu, ilipofika jion kichwa kiliniuma sana...naweza sema sijawah umwa kichwa kiasi kile jamaa tuliyepanga nae kwenda alikuwa anapiga simu sikuweza hata kupokea, nikiwa katika maumivu makali kuangalia hv mbele yangu namuona live...amechukia sana, nilipiga kelele lakini sauti haikutoka..nguvu ziliniisha...kuna mambo aliongea siwez kuweka hapa nahofia usalama wangu, Jamani nipo kwenye kiapo kibaya sana...Kama Kuna mtu anajiamini anaweza niepusha na haya majanga anisaidie tofauti na hapo, naweza potea Mimi, mama yangu pamoja na huyo atakaenisaidia endapo atashindwa nguvu na huyu jini. Siwez kuendelea kuelezea chochote, nipo kwenye kiapo kizito sana hapa ninapongea Nina alama kwenye paja langu la kushoto...wanaojua haya mambo nafikir wanafahamu hiyo alama ina maana gani kwenye jamii hz za majini. Nipo kwenye kitanzi sijui nachomokaje!
Nahitaji msaada wenu wa dhati ndugu zangu. Zile nguo nilizompa nilifanya kosa kubwa sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app