Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Hahahaha Jini huyo maskini kama mimi hanifai hela ndgo kiasi hicho!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] namim hilo kwakweli nimeliona, ukute miezi kadhaa inaisha ukimfuatilia jamaa na nyuzi zake, hapa ume komaa unaacha kufanya mambo ya msingi kumbe anacheza na saikolojia za raia kila siku mpaka episode zake zitakapo fika 1000,,,

Weakness yetu wabongo nikwamba kwenye muvi unakuta muhusika ambaye ni 1) jini mfano, analipisha gari barabarani,,,,
2) Jambazi anavua viatu kuingia ndani akotaka kupora mali etc.

Sasa namim huyu nmesha anza kuona weakness hapa kwenye episode zake,, et jini katuma laki320....... Hahahaha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba hiyo ni Live na siku nikiwa ofisin sina hata hela ya lunch ghafla Tigopesa inasoma..yani mbwa hawa wanajua kila kitu, mkibishana kwenye sms au ukimletea jeuri siku nzima inaharibika..hata ukiwa bar nilikua nahisi napigwa viwembe na kunyolewa nywele yani nakua uncomfortable mpaka naacha kunywa pombe, kumwambia mtu siwezi yani aarrghhh zile heka heka hapana kwakweli mpaka nikiwa club namuhisi basi naanza kumtukana kwamba flani acha mambo ya kis** nge maana sometimes unahisi **** inashikwa livee!
Kha!
 
Nimekupiga marufuku mtoto wa kiume kutumia maneno kama 7bu, hvy..una haraka gani au unawahi foreni ya kusuka?

Mwanaisha Mohamed anakuambia uoge..wewe na kidevu chako kilichochafuka zege la ndevu unasema unaogopa baridi..??rubbish!!

Niko na Z-Anto hapa anasema rudia hapo kwenye kupigwa busu kisha akakata simu. kitunguu swaumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio vizuri mtoto wa kiume kutumia maneno kama Foreni...ni Foleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati tuko high school kuna dada alishakutana na hao viumbe. Aliishi kwa shida sana shule. Alikua akipandisha maruhani yake utamuonea huruma. Sijui kama aliponaga maana mpaka tunamaliza form six alikua bado anazunguka kwa wachungaji amfukuze mume wake wa ujinini.
Kilichomponza alipewa Pete na huyu dada wa jini akajua Pete kweli kumbe ilikua Pete yake ya ndoa na huyo jini. Na mtoto walikua nae

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kwenye mtoto niache fire

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUKUSHAURI ILI ASIKUFATE TENA USIKU UNAPOLALA UJIPAKE MAFUTA YA NDIMU NA UWEKE KITUNGUU SWAUMU CHINI YA MTO HAJI TENA MAANA KHARUFU ZA MAFUTA YA NDIMU NA VITUNGUU SWAUMU VINAWAKERA SANA NA MAFUTA YA NDIMU HAKIKISHA UNAPAKA KILA MARA JAPO CHINI YA MAKWAPA ATAKIMBIA MWENYEWE
Dawa hapo ale noah aka mbuzi katoliki aka mnyama mtamu halafu tuone kama jini atabaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar zenu wadau. Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielew nifanye Nini.
Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.
Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba. Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali.
Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu...Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.
Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.
Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.
Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana[emoji847] Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.
************
Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?
Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? [emoji849][emoji50] Akawa anacheka[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?
Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hata hapa atakwambia naona umeenda kunisema jamii forums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Whaaaat?[emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwa miaka ya 2001 tulikuwa tunaendaga sana coco siku ya jumamosi na jumapili, mshikaji wetu akatuacha baada ya maongezi na huyo demu akamwambia anakaa mitaa ya Morocco (nanukuu) Kwa hiyo wakaamua watembee maana sio mbali walipokuwa wanakaribia karibia na kanisa wakati mshikaji anaendelea kuongea akajikuta yupo pekee yake

Mshikaji akajua labda yule mdada amesimama kuangalia vizuri haoni mtu.

Akajaribu kujiridhisha labda arudi kidogo kumuangalia hakuona mtu zaidi ya watu wengine waliokuwa wanarudi kutoka beach.

Mshikaji hakudumu na tokea hapo alikuwa ni mtu wa kuumwa mpaka 2003 mwanzoni tukampoteza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom