PutinV
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 1,046
- 1,643
KUNA mtu ametongoza hapo au ni shughuli na maongezi ya kawaida
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuwaje6mkuuDaah, izi mambo ni kweli aseee mi imenikuta mwaka Jana kutongoza tongoza ovyo kidogo niwe chizi , nilipo anza kusali ndio ikawa pona pona yangu
Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha sana.Ilikuwa miaka ya 2001 tulikuwa tunaendaga sana coco siku ya jumamosi na jumapili, mshikaji wetu akatuacha baada ya maongezi na huyo demu akamwambia anakaa mitaa ya Morocco (nanukuu) Kwa hiyo wakaamua watembee maana sio mbali walipokuwa wanakaribia karibia na kanisa wakati mshikaji anaendelea kuongea akajikuta yupo pekee yake
Mshikaji akajua labda yule mdada amesimama kuangalia vizuri haoni mtu.
Akajaribu kujiridhisha labda arudi kidogo kumuangalia hakuona mtu zaidi ya watu wengine waliokuwa wanarudi kutoka beach.
Mshikaji hakudumu na tokea hapo alikuwa ni mtu wa kuumwa mpaka 2003 mwanzoni tukampoteza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo apo wanakuazibu mpk unajutia kuumbwaDawa hapo ale noah aka mbuzi katoliki aka mnyama mtamu halafu tuone kama jini atabaki
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mkuu, kuna wengine walevi zaidi ya binaadamuKitimoto na pombe ndio adui wao...kama yanayosemwaga ni kweli lakin
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeanz kutumia hivi vitu tangu 98 lkn nilikutana na haya mamboKitimoto na pombe ndio adui wao...kama yanayosemwaga ni kweli lakin
Sent using Jamii Forums mobile app
Trust Me hii ni PAUKWA PAKAWA inshort nimesoma kidogo haya masuala ya majini kiimani kuna vitu fulani vinaonekana wazi ni tungo za mwanabalaghaBaada ya kujaribu kupiga ile simu Mara kadhaa bila mafanikio, wakati huo Nilikuwa nimekaa nje ya duka na machinga (wanaopanga bidhaa chini) tukipiga story mbili tatu, hvy wakati ile simu naongea nayo wote walikuwa wananisikia, walivyoona nimebadilika Sina furaha tena ikabidi waniulize kulikoni? Sikuwa na haja ya kuwaficha nikaweka wazi kila kitu kilivyokua juu ya Lile sakata.
Basi nikaibua mjadala mzito kila mtu anasema lake, baadhi yao walisema mwanangu Hy Ni bahati ya mtende...we utakuwa umependwa na jini na Mara nyingi majini wa hv, ukienda nao sawa watakupa utajiri wa kufa mtu. Nikabaki nashangaa...wakaendelea kusema, watu wanakesha kwa waganga na kuvaa mipete 10 kwenye vidole ili wawaite majini Hawa, ila ww amekufwata mwenyewe kazi kwako baba. Baada ya kusikia hvy ndo walizidi kunivuruga, walitegemea nitafurah badala yake ndio wameniongezea hofu.
Lakini mmoja alikuja na wazo tofauti na wengine hili kidogo lilinitia Moyo. Akasema huyo msichana itakuwa anakujua vzr na anakufwatilia kitambo, hz anazokufanyia Ni drama tu. Kutakuwa Kuna mtu wako wa karibu Ana mpa taarifa zako muhimu tegemea vingi baadae, nimapema sana kusema Ni jini maana kwa alichokifanya hata binadamu wa kawaida anaweza kukifanya Ni Jambo la kujipanga tu.
Sikutaka kuendelea kuwasikiliza, nikarudi zangu dukani. Muda wa kufunga ulipofika nikawa nafunga, Kuna jamaa mmoja akaniuliza hz nguo alizonunua umeziacha humo dukani nikamjibu ndio, akashauri Ni vyema ukazitoa maana Kama Ni jini Kweli zinaweza kuwa 7bu ya biashara yako kuharibika.
Nikafanya Kama alivyoshauri. Nikiwa kwenye gari kuelekea nyumbani, sio Siri Nilikuwa na mawazo sana, Kama Kweli itakuwa Ni jini kwa Nini aje kwangu? Ikiwa sinaga tabia ya kwenda kwa waganga ya kiufupi mm Ni mkristo kamili sijawah fanya shriki katika maisha yangu..na atakuwa anataka Nini hasa.
Nikafika nyumbn nikafanya majukumu yangu Kama kawaida nikaingia kulala...ila usiku nilipolala nikaota njozi za mwanamke yule yule aliekuja dukani na kununua nguo, hlf hz nguo alizoninunulia ndio Nilikuwa nimezivaa ndotoni..tupo kwenye bustani kubwa nzuri ya mauwa pembeni Kuna mifereji ilikuwa inatiririsha maji masafi sana ila yalikuwa na ubaridi sana, Akawa ananilazimisha tuoge nikamwambia siwez kuoga maji ya baridi hvy, akaniambia utazoea tu, maana hapa tulipo ndio maji tutakayokuwa tunatumia siku zote. Alinilazimisha sana nikakataa...akawaananikimbiza ili niingie humo ndani ya maji,....nikastuka kutoka usingizini Moyo ulikuwa unanienda mbio mno, nimewah ota ndoto nyingi za kutisha lkn ile niliamka Ikiwa Kama Kweli mtu aliyetoka kukimbia nimechoka na mapigo ya Moyo yako juu.
Siku lala tena nikaamka kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zangu maana ilikuwa mida ya Kama saa 12: 40 alfajir na sio kawaida yangu kuamka mapema hvy. Labda niwe na Jambo maalum nataka kufanya. Ile natoka bafuni naangalia simu nakutana na sms namba Ni ile ile ya Jana.
" Pole sn mme wangu najua umechoka, Leo vaa zile nguo nilizonunua Jana najua utapendeza, nitafurah ukiniitii, asubuhi njema mume, nakupenda".
Nikastuka sana, nikapiga ile namba ili Ni mwambie kwa Nini anafanya vitu vya ajabu hvy...na ile pole alionipa ni ya nini? Simu ikawa haipatikan...kiukweli sikutaka kabisa kuvaa zile nguo...nikawa nachagua nguo nyingine kwenye kabati ili nizipasi nivae niondoke..sijamaliza zoez umeme ukakatika. Nikapigwa na butwaa...nilijaribu kuwaza inaweza kuwa ni michezo yake pia...ila nafsi ina kataa kila nguo ninayo iangalia imejikunja haifai...nikawa Sina jinsi, nikavaa zile nguo nilizokuja nazo Jana yake. (Yan alizonunua)
Hapa ndio mateso yakipoanzia...ilikuwa tarehe 28 nakumbuka siku ya ijumaa. Baada ya kuvaa zile nguo...mm huwa natumia perfume inaitwa Michagany kwa wale mnaoifahamu nakumbuka kabisa nimetoka nimejipulizia perfume yangu ya siku zote, ila nilipofika kwenye gari najisikia nanukia harufu tofauti kabisa..Tena Kali, nikawanajiuliza imetoka wapi? Na nikirudisha kumbukumbu ile ile anayotumia yule binti. Hapa ndipo nilipojua Kweli yule sio mwanadamu wa kawaida.
Sikutaka kumshirikisha yoyote juu ya kinachoendelea, siku Hy biashara haikuwa nzur kabisa, mida ya Kama saa 7 hv mchana, akaja mbaba mmoja akanunua nguo za Kama laki mbili na nusu hv...Tena alionekana anaharaka Kama mtu anaetaka kusafir nae hakuomba discount baada tu ya yule baba kuondoka, simu yangu inaita..siku tazama namba kwa makini nikapokea Mara nasikia sauti ya yule mwanamke.
Hakunipa nafasi ya kuongea, alisema hv..." Nimefurah sana Leo mme wangu umependeza sana mpk nataman niwe pembeni yako muda wote nisije nikaibiwa...huku anacheka.. akaendelea kusema nakutumia zawadi yako soon...akanibusu Kisha akakata simu. Kumbuka maneno yote hayo anaongea hakuna hata moja nimejibu, nimebaki kuduwaa tu. Baada ya hapo simu ikawa haipatikan. Jasho lilikuwa linanitiririka Kama maji Ikiwa ofisi yangu ina feni zaidi ya moja na zina nguvu za kutosha. Baada ya Kama dk 5 hv...sms ya tigo pesa ikaingia kwenye simu yangu. Nimetumiwa 320,000 jina la alienitumia Ni Mwanaisha Mohamedi...namba Ni tofauti na ile inayonipigia...kupiga ile namba inaita tu...haipokelew.
Vioja Ni vingi sana...kasheshe ilikuwa tarehe 31 Dec siku ya mkesha wa mwaka mpya. Narudi wacha nipumzike kidogo.
Inaendelea.......
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huwa napata tabu kumuelewa kijana tena anaejitanabaisha kuwa wa kiume..
kwanza, akitumia emoji katika maandishi yake
Pili, kukatisha maneno eti '7bu'..sasa hako ndio kakitunguu swaumu gani?
Anyway..hapo njia panda unafanya nini saivi? Au ndio unakula mavitunguu swaumu ili uje uendelee?
Mtike mghenji kwa mghanga areighwa mbingu ya vurinji ijeni lithiremkome thala,, kwa mtu asiejua mambo ya dunia na visa vya viumbe wake anaweza kupuuzia lakini mshkaji anapitia kipindi cha maumivu moyoni kuliko kuachwa na demu unaempendaIsanga lina vywasi...
POLE sana Mkuu, katika yote MOLA ndio mlinzi na mpiganaji wetu, vita hii ni ya Kiroho zaidi, wengine wataona movie ila ugumu unaopitia ni changamoto tuu, hakuna marefu yasiyo na mapana yasiyo na mwisho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtike mghenji kwa mghanga areighwa mbingu ya vurinji ijeni lithiremkome thala,, kwa mtu asiejua mambo ya dunia na visa vya viumbe wake anaweza kupuuzia lakini mshkaji anapitia kipindi cha maumivu moyoni kuliko kuachwa na demu unaempenda
Sent using Jamii Forums mobile app
Iliwahi kunitokea saa nane usiku nimelala usingizi mzito Pazia la dirisha sikulishusha ila vioo Nimefunga sasa nikazinduka ghafla usiku nikakuta jamaa ananiangalia kwa utulivu na hata alipojua nimemuona hakuondoka nilipopiga kelele hakuondoka nikaduwaa siamini baada ya dk tatu akaondoka mwenyewe
TrueHuwa napata tabu kumuelewa kijana tena anaejitanabaisha kuwa wa kiume..
kwanza, akitumia emoji katika maandishi yake
Pili, kukatisha maneno eti '7bu'..sasa hako ndio kakitunguu swaumu gani?
Anyway..hapo njia panda unafanya nini saivi? Au ndio unakula mavitunguu swaumu ili uje uendelee?