Kuna watu mnachukulia haya mambo Kimasihara na utani, juzi nilikuwa Morogoro kuna binti yuko 20 yrs namfahamu ingawa si kwa undani sana, basi nikawa nimemwomba nimtoe jioni akale ice cream pale kwenye jengo la Nssf. Tumekaa pale tunabadilishana mawiki matatu, katika stori zetu ikafikia mahali akanisimulia mambo makubwa yaliyopata kumtokea. Kiufupi alikuwa ana jini ambalo lilipelekea hata kuanza kumbadili hata mwonekano wake hasa sura alinionesha hadi picha ambazo alipiga akiwa na mwonekano tofauti, nilikataa kuwa sie yeye, maana sura tofauti kabisa, mrembo balaa. Picha zingine kapiga na nduguze yeye sura inaonekana kiza tupu ila ndugu zake wanaonekana vizuri. Sasa anasema anaendelea na tiba kwa kutumia mashehe na anasema amepona kwa kiasi kikubwa.
Kwa kweli hata kukaa nae ilinitisha mana alisimulia mambo mengi yakutisha ikiwa pamoja na kupenda kujikwaruza na kitu chenye ncha kali kwenye mwili ili damu itoke!!!